Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,498
- 7,065
Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo, amedai kuwepo kwa harufu ya upigaji fedha katika Ujenzi wa Jengo la Utawala Arusha. Akiwasilisha hoja yake leo, Jumatano Aprili 16, 2025, wakati akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa mwaka wa fedha 2025/26, Gambo amesema vipimo vya mradi huo vinatofautiana na vile vilivyopo kwenye orodha ya manunuzi ya vifaa (BOQ), jambo linaloashiria uwepo wa ubadhirifu wa fedha.
Gambo ameeleza kuwa jengo hilo lina gharama ya jumla ya Shilingi bilioni 9, kiasi alichokitaja kuwa kikubwa kuliko kawaida, akimtaka Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, kutuma timu maalum kufanya uchunguzi juu ya matumizi ya fedha hizo. Aidha, amesema kuwa kuna mkataba mwingine wa Shilingi bilioni 6.2 ambao pia una mapungufu, kwani baadhi ya vipengele vilivyoorodheshwa kwenye BOQ havijatekelezwa kama ilivyopangwa.
Mbunge huyo amesema kutokana na tofauti kati ya maandishi ya mkataba na utekelezaji halisi wa kazi, gharama za ujenzi zimeongezeka kwa zaidi ya Shilingi bilioni 8 bila maelezo ya kina. Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa Serikali kuchukua hatua haraka ili kujiridhisha na kuhakikisha kuwa fedha za umma zinalindwa dhidi ya matumizi mabaya.
Kuhusu TARURA, Mrisho amezungumzia TSh. 3.4 bilioni ambazo amezitilia shaka na kutaka TSh. 1.6 bilioni zingeweza kutumika kumaliza kero zingine kwa Wananchi wa Arusha. Spika Tulia amtaka Waziri Mchengerwa kuandaa taarifa fupi ya tuhuma hizo ili kuiwasilisha mwishoni mwa bajeti yake ya Ujenzi wa jengo la Utawala.
Tuhuma hizo zimemuibua Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson aliyemtaka Waziri wa Tamisemi, Mohammed Mchengerwa kufuatilia tuhuma hizo alizoziita ‘nzito’ na kuagiza kuja na ripoti fupi.
Mchengerwa akijibu baada ya mchango wa Gambo na maagizo ya spika amesema: "Nimelipokea jambo hilo na tutawasilisha taarifa hiyo wakati wa kuhitimisha. Hili la kusema fedha hii ingefanya hivi na siyo vile, ni vyema tukakumbushana kuwa mipango ya maendeleo, haipangwi na Tamisemi ila ni vikao maalumu katika mabaraza ya madiwani ambayo sisi sote ni wajumbe."