Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,884
- 31,943
FUTARI NA FUTURU NA BALOZI DR. RAMADHANI DAU NA YANGA KIDS WATOTO WADOGO WALIONG’ARISHA SOKA LA TANZANIA MIAKA YA 1970
Kuna mshairi alikuwa anatunga shairi na mwanzo wa ubeti akajiuliza, ‘’Wapi ninaanza kueleza historia hii?’’
Akaendelea kuandika, ‘’Wapi ninaanza kueleza historia hii, historia iliyojaa majonzi na furaha?’’
Najiuliza wapi nitaaza kueleza historia ya vijana wenzangu niliwajua kwa miaka mingi toka utotoni wengine kwa karibu na wengine kwa mbali?
Na wengine hatuko nao wametangulia mbele ya haki.
Bado najiuliza wapi naanza kueleza historia ya Yanga Kids.
Naanza na Kocha Victor Stanslaus?
Leo Balozi Dr. Ramadhani Dau alitualika futari nyumbani kwake Kigamboni.
Niliyoshuhudia kwa macho yangu na kuyasikia kwa masikio yangu hayajapata kunipitikia hata kwa mbali katika fikra zangu.
Baraza ya mbele ya nyumba ya Balozi Dau ilikuwa Majlis ya aina yake.
Balozi Dau alikuwa mchezaji wa Yanga Kids.
Leo nduguze wamemwitika na Balozi karudi udogoni yuko Jangwani na Adolf, Kassim Manara, Mkweche, Godian Mapango, Carlos Mwinyimkuu, Mohamed Selugendo, Juma ‘’Mensah’’ Pondamali na marehemu Tostao.
Sunday ‘’Computer’’ Manara yuko kaka pembeni ya Sunday lakini yeye wakati ule tayari ni ‘’Senior Player.’’
Wanakumbushana kelele za Kocha Victor anawapigia kelele Yanga Kids wakiwa na mpira kuhama sehemu moja ya uwanja wafanye mashabulizi kutoka upande mwingine.
Kocha Victor anapiga kelele, ‘’Change,’’ yaani mpira uondoshwe huko uende kwengine.
Hapa wanamwiga Kocha Victor Stanslaus.
Mohamed Selugendo na Balozi Dau nimewasikia wakikumbushana maelezo ya Kocha Victor kuwa pasi itolewa baada ya kuangalia inapigwa kwa nani ili izae matunda.
Mohamed Selugendo yeye akicheza Winger na anakumbuka sana pasi alizokuwa kimdondoshea Kassim Manara juu kwa kufunga magoli ya kichwa.
Walikuwa hawa ndugu zangu wamerudi utotoni kabisa.
Baraza ya mbele ya nyumba ya Balozi Dr. Dau ilikuwa sawa na Bunge la wacheza mpira na takriban wote walikuwa nyota kwanza katika timu ya Yanga Kids, timu ya watoto wadogo wa Yanga kisha wakacheza timu ya wakubwa kwa kiwango kilekile cha weledi na wakacheza na baadae wakiwa wakubwa kushiriki katika mashindano makubwa ya makombe ya Afrika.
Katika ya haya wengi wao walivaa jezi za Taifa Stars.
Hata hivyo huu haukuwa ndiyo mwisho wao.
Walivuka mipaka ya Tanzania na kucheza soka la kulipwa Ulaya na kwengineko.
Utapenda kumsikia Juma ‘’Mensah’’ Pondamali anavyoeleza mechi ya mwaka wa 1980 waliyocheza Ndola siku Taifa Stars ilkipocheza na Zambia ilivyoshinda kucheza fainali la Kombe la Mataifa ya Afrika, Nigeria.
Rais Kaunda yuko uwanjani mkono wake wa kulia ameshika kitambaa cheupe na uwanja umejaa mashabiki wanaishangilia timu yao, Pondamali anatueleza.
Utapenda kumsikiliza Juma Pondamali akieleza kipigo cha mashuti makali alichokipata kutoka kwa washambuliaji wa Zambia na jinsi alivyokuwa anapangua mashuti ambayo kwa hakika yangekuwa magoli.
‘’Nilikuwa nahema kama mchezaji wa ndani na kipindi cha mapumziko nikamuomba Mahadhi aje anisaidie maana nilikuwa na hofu nitafungwa tu.’’
Juma Pondamali anasema Mahadhi alikataa.
Aliyoyaona kwa Pondamali yaliyokuwa yanamkuta mlinda mlango mwenzake yalimtosha.
Taifa Stars ilikuwa inahitaji ushindi wa goli moja tu kuingia kwenye fainali za Kombe la Afrika.
Ilikuwa katika kuelemewa kama huku alikoeleza ndipo Juma Mensah anasema alidaka mpira wachezaji wa Zambia wakiwa wamewaelemea wamejazana golini kwao na yeye kwa haraka baada ya kudaka tu akampigia mpira mrefu Peter Tino katikati ya Uwanja.
Peter Tino alipoupokea mpira ule hakusubiri akaupeleka mbele kwa kasi na ghafla akajikuta amewaacha walinzi wa KK 11 nyuma yuko yeye analiangalia goli la Zambia.
Yaliyobakia ni historia.
Pondamali anazungumza kwa nguvu na hisia kiasi unajiona kama uko uwanjani unaangalia pambano.
Adolf Rishard utafurahi na utacheka kumsikiliza akieleza changamoto alizokuwa akikitananazo kama nahodha wa ama katika Timu ya Taifa au kwenye club.
Adolf anaongea kwa utulivu na taratibu na anapanga vyema maneno yake kwa staili ya kukufanya wewe ucheke vipi Pondamali anafukuzana uwanjani na waamuzi.
Anaeleza shida iliyokuwa ikimkuta kumtuliza Pondamali asifanya jambo likasababisha matatizo kwake na kwa hiyo kuathiri timu nzima.
Pondamali anamweleza Adolph, ‘’Umeona Sabu na Masimenti wamenikumba wameniingiza kwenye nyavu na wamefunga goli.’’
Captain Adolph anamjibu mlinda mlango wake kuwa, ‘’Tulia hazipiti dakika tano tutarudisha hili goli.’’
Hakika goli linarudishwa.
Bila kuambiwa na mtu nimeshuhudia mapenzi ambayo bado yangalipo kati ya nyota hawa miaka mingi baada kumaliza kucheza soka.
Mbali na tulipokuwa tunazungumza barazani nimeona tulipokuwa ndani tumekaa tunafuturu wanavyosemezana wenyewe kwa wenyewe.
Nimewasikia pale Majlis Kassim Manara akilaumu kitendo cha uongozi wa Yanga kuivunja Yanga Kids kwa kuwatoa wao kidogo kidogo na kuwatia timu kubwa kinyume na maelekezo ya Kocha Victor kuwa timu hiyo iachwe kama ilivyo hadi ifikie upeo kuwa sasa timu yote imekuwa ndiyo timu ya Yanga.
Adolph anaeleza mechi sasa wametoka Yanga baada ya mgogoro wa mwaka wa 1975 wako Pan Africa walizocheza Afrika ya Magharibi na kwengineko kwa fasaha utadhani anasoma kutoka kitabuni.
Adolph na Juma Mensah wana uzoefu mkubwa wa soka la Afrika na siasa zake kuanzia kupata wachezaji hadi vipi timu na viongozi wa soka Afrika wanavyoendesha mambo ya mpira.
Wawili hawa wamecheza soka pamoja toka wakiwa makinda na hakuna wasichokijua.
Mwili utakusisimka ukiwasikia wakieleza saikolojia ya uchawi katika mpira na nafasi yake katika kupatikana ushindi hali kadhalika nafasi ya hongo.
Yapo mengi sana yanayotangulia mechi ndani ya uwanja kabla mpira haujaanza.
Sikuwanajua kuwa wachezaji wanajuana vizuri sana kiasi wanajua nani anafaa kumkaba nani na wakamweleza kocha na kocha anakubali ushauri.
Captain Adolf kaeleza mengi na vipi Taifa Stars walikuwa wanafanya uchaguzi katika mabeki kama watatu hivi kati ya Kajole, Amasha na mwingine nani acheze.
Halikadhalika kuficha uwezo wa washambuliaji kwa mabeki ili wasitishike na yeye.
Alieleza vipi Mayanga mshambuliaji hatari wa Zaire alivyotulizwa na kijana mdogo Ahmed wa Pan Africa juu ya sifa zake nyingi za kutisha.
Adolph anaeleza changamoto za nyakati hizo za wachezaji kuzuiwa kutoka nje ya mipaka kucheza soka la kulipwa na jinsi walivyokuwa wakinyang’anywa pasi za kusafiria kwa kuogopa wasitoroke.
Adolph ana kisa cha kusisimua cha yeye kukamatwa Uwanja wa Ndege Nairobi.
Balozi Dau siku zote yeye ‘’adui’’ yake ni Sunday Manara.
Kila mtu akifika akikaribishwa na kukaa kitako swali lake kwake litakuwa, ‘’Hebu tumalizie ubishi huu Kassim Manara na Sunday nani alikuwa na mpira mkubwa?’’
Balozi atacheka sana akisikia jibu kuwa Kassim ngoma yake ilikuwa nzito kuliko ya Sunday kaka yake.
Kassim anasema Timu ya Uholanzi ya Kombe la Dunia walikwenda Austria kufanya mazoezi na wakacheza na timu yao.
Kassim alipangwa kucheza Sunday alikuwa kakaa kwenye bench.
Nimewaona waandishi wa michezo wakihangaika na camera zao wakifanya mahojiano na Sunday na Kassim Manara.
Naamini watatuletea vipindi vya kuburudisha kutokana na waliyoyasikia katika mkusanyiko huu na katika mahojiano hayo.
Wakati wa kufturu nilibahatika kukaa na Carlos Mwinyimkuu na katika mazungumzo alinifahamisha kuwa ana maktaba nyumbani kwake ya picha nyingi za mpira alizozihifadhi vizuri.
Alinifahamisha kuwa amehifadhi pia historia yake ya mpira.
Anasema kacheza mechi 16 za mashindano makubwa zote kacheza dakika 90.
Sunday Manara yeye kanifahamisha kuwa mshabiki wake mmoja amemuuzia hazina kubwa ya picha kutoka magazeti ya zamani ambayo alikusanya miaka ile.
Sunday amehifadhi picha hizi baada ya kuzifanyika ''scanning.''
Hizi ni habari nzuri sana kwa TFF ikiwa watataka kutengeneza maktaba yake ya mpira wa Tanzania.
Halikadhalika pia hizi ni taarifa nzuri kwa waandishi wa michezo na vyombo vya habari kwa ujumla.
Nimesikitika sana sikuweza kumpata Kassim Manara kwa tete a tete hata ya nusu dakika kwani baada ya kufuturu hakukaa sana aliondoka kutokea hapo kukimbilia uwanja wa ndege kwa safari ya kurejea Austria.
Mbele anaetazama camera sharti jeusi na jeupe ni Juma ''Mensah'' Pondamali na kuliani kwake ni Carlos Mwinyimkuu, wa kwanza kulia kanzu ya blue ni Mbaraka Dau na anaefuatia ni Balozi Dr. Ramadhani Dau kulia kwake ni Mshike na kushoto aliyetupa mgongo kanzu nyeupe ni Kassim Manara
Kulia aliyetupa mgongo ni Adolph Rishard akipeana gonga na Kassim Manara na pembeni ya Kasim ni Mohamed Selugendo Juma Mensah anaeleza mechi ya Zambia na Taifa Stars Ndola 1980