Fungu gani nimuweke Maalim Seif ahesabike?

Deogratias Mutungi

Senior Member
Oct 1, 2019
140
181
FUNGU GANI NIMUWEKE MAALIM SEIF AHESABIKE?

Na, Deogratias Mutungi

Kisiasa unaweza kusema hizi ni nyakati za jioni na hivyo giza linaanza kuingia na ni vema kuanza kujiandaa kurejea majumbani tayari kwa kusubiri siku nyingine, Huu ndio ukweli ambao upo wazi kuwa Bwana Maalif Seif Shariff Hamad mwanasiasa mkongwe na anayeheshimika hapa nchini Tanzania nyakati zake kisiasa zipo upande wa machweo (Magharibi), Maalim amechoka kisiasa na umri umemtupa mkono katika medali za kisiasa hivyo anahitaji kupumzika na kubaki mshauri wa masuala ya kisiasa na si kukimbizana majukwaani na vijana wenye mawazo mapya na hili halina ubishi kisiasa.

Kisiasa Zanzibar bila Maalim Seif Shariff Hamad inajengeka na inasonga mbele wapo wanaoamini Maalim ndo kila kitu katika siasa za upinzani ndani ya Zanzibar lakini wanasahau kuwa kila jambo na wakati wake na huu ni wakati wa zama mpya na rika la tabaka la watu wanaopendelea kuona mabadiliko zaidi yanayogusa matamanio ya walio wengi, Siasa za umimi zimepitwa na wakati na sasa ni siasa jumuishi yaani fursa sawa kwa wote kisiasa.

Inawezekana msomaji wa makala haya asielewe mantiki ya andiko hili endapo nitashindwa kufafanua kwa kina ninapojenga hoja ya kuchoka kwa Maalim Seif kisiasa hili hoja hii inoge na kufana au kueleweka vyema ni sharti nifafanue kwa kina na ndio dhana halisi ya uchambuzi huu dhidi ya mzee wangu Maalim Seif

Tukubaliane Siasa uendana na nyakati ikiwa ni pamoja na umri mantiki hapa ikiwa ni nguvu na ushawishi katika uwajibikaji kwa umma kwa mantiki ya maendeleo ya watu, kwa muktadha huo nadriki kusema kuwa Maalif Seif Shariff Hamad amechoka kisiasa na anahitaji kustaafu siasa za ulingoni na badala yake abaki kuwa mshauri ndani ya chama chake, kuendelea kusimama kama mgombea wa nafasi ya urais kwa miaka nenda rudi bila kuandaa watu wengine ni tafsiri ya tamaa na uchu wa madaraka na huo ndio utambulisho wa viongozi wa siasa za upinzani wanaojenga hoja za demokrasia huru wakati wao hawawezi kuzitekeleza ndani ya vyama vyao, tabia hizi kwa lugha za kisiasa ujulikana kama “Unafiki wa kisiasa”

Japo kwa Afrika kinachofanywa na Maalif Seif si kitu kigeni katika ulingo wa siasa bali ni sehemu ya desturi na tamaduni za siasa za Kiafrika kuwa na viongozi ambao ni viganganizi wa madaraka kitu ambacho kisiasa ni dhambi na si dhamira njema katika ustawi wa taifa lolote lile kimaendeleo, viongozi wa namna hii uamini wao ndio zaidi kuliko wanachama wengine, Tabia hii kwa vyama vya siasa Tanzania ipo ndani ya mifumo ya siasa za upinzani kuwa na ubinafsi mwingi kuliko itikadi na maslahi ya chama na ndipo ugumu wa kupambana na CCM unapoanzia hapo.

Tayari Maalim Seif ametangaza rasmi nia yake ya kugombea kiti cha urais wa Zanzibar kupitia chama chake kipya cha ACT-Wazalendo, Baadhi ya wachambuzi wa siasa za ndani wanasema na kutabiri ujio wa Maalim kama kama tishio kubwa katika uchaguzi wa mwaka huu wa 2020, Sijui ni kipimo kipi wanatumia au pengine ni mahaba yaliyopitiliza kwa Maalim Seif, Lakini ukweli wa kimantiki ni kuwa Maalim ni Yule wa siku zote kinachomutofautisha ni chama tu na itikadi yake vinginevyo mvinyo ni uleule tofauti ni chupa tu.

Makala haya yanapingana na dhana hiyo ya utabiri unaofikriwa na baadhi ya wachambuzi wetu wa ndani badala ya kujenga hoja kwa nini uchaguzi utakuwa mgumu kwa Chama Cha Mapinduzi wanaishia kusema “Maalim ni mwamba wa siasa za visiwani” Ukweli wa kisiasa ni kwamba Maalim Seif Shariff si mwamba tena katika siasa za Zanzibar kutokana na Wazanzibar kuchoshwa na hoja zake za kila nyakati za uchaguzi kuwa zilezile.

Kwa Maalim hakuna jipya wala lolote lile lenye tija katika siasa za usasa na mambo leo hata kama amebadilisha chama chenye itikadi tofauti na chama chake cha zamani CUF Maalim atabaki kuwa Maali Seif Shariff Hamad ambaye kwa nyakati hizi siasa zake zimekuwa za kuonewa huruma, Kisiasa mwanasiasa anapofikia hatua ya kuanza kuendesha siasa za namna hii ni dalili rasmi ya mchoko katika medali za kisiasa na ni heri kustaafu kuliko kutaka huruma ya umma.

Ndio maana makala haya yanapata taabu ya kumuweka fungu gani Maalim aweze kuhesabika, Kisiasa na hasa katika siasa za uchaguzi wa mwaka huu Maalim angeweza kuhesabika yupo fungu lipi endapo tu angemtaguliza mwanasiasa mwingine badala yake kusimama kugombea kiti cha urais kupitia chama chake, kuendelea kusimama yeye kana kwamba wengine hawana uwezo wa kusimama katika nafasi hiyo ni udhaifu kisiasa na ni vigumu kupata fungu la kumuweka Maalim.

Pengine Maalim akipata fursa ya kupitia andiko hili atujulishe ni kwanini amekuwa akijiona yeye anafaa zaidi kuliko wanachama wengine, Je bila yeye hakuna mbadala, kisiasa na kidemokrasia haya ni maswali ya msingi ambayo wanachama na wakereketwa wa chama cha Maalim yawapasa kujiuliza mara mbili mbili kutofanya hivyo ni uzembe wa kifikra kisiasa na ni vigumu kuaminika kwa wapiga kura wa Zanzibar.

Kwa mantiki ilivyo kisiasa ni wajibu wa wachambuzi na wale wote wenye fikra kuwa uchaguzi wa mwaka huu kwa upande wa Zanzibar utakuwa mgumu kuliko nyakati zote, Jibu kwa fikra za namna hii zinajibiwa kuwa “si za kweli” Uchaguzi wa Zanzibar utakuwa mwepesi kuliko siku zote kwa sababu sera, falsafa, mitizamo, fikra na mawazo ya mgombea wa chama cha upinzani yanafahamika hata kabla ya kipyenga kupulizwa na dhana hii ipo wazi wa Wazanzibar wenyewe.

Kwa lugha rahisi kabisa uchaguzi katika dhana ya ushindi kwa Chama Cha Mapinduzi CCM utakuwa mteremko kuliko ule wa kitonga na huu si ushabiki wa CCM wala kupendelea upande Fulani bali ndio ukweli wa kimantiki unavyoonyesha kwa sasa katika medali za kisiasa, Hoja zipo wazi moja kuu kati ya zote ni watu kutaka mawazo na fikra mpya kutoka kwa mgombea ambaye itakuwa mara yake ya kwanza kusimama kama mgombea katika nafasi ya urais.

Aidha kupitia gazeti hili toleo lililopita niliandika na kuchambua juu ya uwezo na umahiri wa Dk. Hussein Mwinyi ambaye ameingia katika tano bora ya wagombea wa kiti cha urais upande wa Zanzibar, Bila shaka kwa uwezo wa Dk. Mwinyi chama chake kitampa ridhaa ya kusimama na kupambana na Maalim Seif ambaye kisiasa ni mchovu na mwanasiasa asiye na mawazo mapya ya kushawishi wapiga kura wa Zanzibar, Maalim wa enzi za mwaka 2000 akiwa na umri wa miaka 57 sio huyu Maalim wa sasa wa miaka 76 zama za Maalim zimepitwa na wakati na sasa hizi ni zama mpya za watu wapya na wenye mawazo mapya.

Kwa mantiki hiyo Wanzibar watapendelea kumsikiliza zaidi mgombea ambaye ni mpya katika nafasi hiyo ya urais na kutaka kusikia ana mapya gani ya kuwavusha Wanazanzibar katika shughuli za kimaendeleo kisiasa na kiuchumi ambayo Maalim pengine hana uwezo wa kuyatatua kwa sababu nyakati fulani aliwahi kuwa kiungo muhimu ndani ya serikali ya umoja wa kitaifa na pengine hakashindwa kuyatatua matatizo ya Wazanzibar.

Nia na dhumuni la makala haya si kumchomea utambi Maalim Seif Shariff Hamad kwa Wazanzibar bali ni uchambuzi unaosimama katika uwazi na mantiki ya kuonyesha nani ni bora zaidi katika kipindi hiki tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu hapo Oktoba na wala sio ubaguzi wa rangi kwa mgombea wa aina yoyote ile kama ilivyokuwa wakati wa chama cha ZNP maarufu kwa jina la Hizbu, Kwa nukta hiyo ni jukumu la Wazanzibar wenyewe kupima na kuona nani ni bora zaidi katika ustawi wa Wazanzibar na maendeleo yake.

dmutungid@yahoo.com
 
Tatizo ni pale Mwandishi anaposhindwa kutofautisha mapambano ya kudai Uhuru wa nchi ya Zanzibar dhidi ya Ukoloni uliojificha.

Maalim Seif ni nembo ya kudai haki kwa Zanzibar na si vyenginevyo.

Unapochambua kwa muktadha wa Madaraka na ubiinasfsi itakuwa umejipofua makusudi na kuacha dhima aliyopewa Maalim seif na wazanzibari.

Huyu mtu ni level nyengine. Anaaminiwa na anajiaminisha.

Mengine hayo ni porojo.
 
Seif hata akitembelea mkongojo tutamchagua tu.Huna hujualo katika siasa za Zanzibar rudi kwenu Bukoba mnyauko umeisha sasa hivi.
 
Katika maelezo yako umemuelezea maalim peke yake hujaelezea wapiga kura natume
Ili andishi lako linoge na kutamanika jaribu tena kuchambua kupitia sehemu hizo 3
Elewa maalim anapata jeuri ya kugombea kupiti wapiga kura hao wanauwezo wa kumpitisha mgombea yeyote mwenye maslahi na wazenji lakini umesahau tume ndio yenye mamlaka ya kumteua mgombea wanaemtaka kwa mantiki hiyo hata maalim angekuwa na umri wa 100 tume na wazenji vikiwa sawa atashinda
 
Katika maelezo yako umemuelezea maalim peke yake hujaelezea wapiga kura natume
Ili andishi lako linoge na kutamanika jaribu tena kuchambua kupitia sehemu hizo 3
Elewa maalim anapata jeuri ya kugombea kupiti wapiga kura hao wanauwezo wa kumpitisha mgombea yeyote mwenye maslahi na wazenji lakini umesahau tume ndio yenye mamlaka ya kumteua rais wanaemtaka kwa mantiki hiyo hata maalim angekuwa na umri wa 100 tume na wazenji vikiwa sawa atashinda
 
FUNGU GANI NIMUWEKE MAALIM SEIF AHESABIKE?

Na, Deogratias Mutungi

Kisiasa unaweza kusema hizi ni nyakati za jioni na hivyo giza linaanza kuingia na ni vema kuanza kujiandaa kurejea majumbani tayari kwa kusubiri siku nyingine, Huu ndio ukweli ambao upo wazi kuwa Bwana Maalif Seif Shariff Hamad mwanasiasa mkongwe na anayeheshimika hapa nchini Tanzania nyakati zake kisiasa zipo upande wa machweo (Magharibi), Maalim amechoka kisiasa na umri umemtupa mkono katika medali za kisiasa hivyo anahitaji kupumzika na kubaki mshauri wa masuala ya kisiasa na si kukimbizana majukwaani na vijana wenye mawazo mapya na hili halina ubishi kisiasa.

Kisiasa Zanzibar bila Maalim Seif Shariff Hamad inajengeka na inasonga mbele wapo wanaoamini Maalim ndo kila kitu katika siasa za upinzani ndani ya Zanzibar lakini wanasahau kuwa kila jambo na wakati wake na huu ni wakati wa zama mpya na rika la tabaka la watu wanaopendelea kuona mabadiliko zaidi yanayogusa matamanio ya walio wengi, Siasa za umimi zimepitwa na wakati na sasa ni siasa jumuishi yaani fursa sawa kwa wote kisiasa.

Inawezekana msomaji wa makala haya asielewe mantiki ya andiko hili endapo nitashindwa kufafanua kwa kina ninapojenga hoja ya kuchoka kwa Maalim Seif kisiasa hili hoja hii inoge na kufana au kueleweka vyema ni sharti nifafanue kwa kina na ndio dhana halisi ya uchambuzi huu dhidi ya mzee wangu Maalim Seif

Tukubaliane Siasa uendana na nyakati ikiwa ni pamoja na umri mantiki hapa ikiwa ni nguvu na ushawishi katika uwajibikaji kwa umma kwa mantiki ya maendeleo ya watu, kwa muktadha huo nadriki kusema kuwa Maalif Seif Shariff Hamad amechoka kisiasa na anahitaji kustaafu siasa za ulingoni na badala yake abaki kuwa mshauri ndani ya chama chake, kuendelea kusimama kama mgombea wa nafasi ya urais kwa miaka nenda rudi bila kuandaa watu wengine ni tafsiri ya tamaa na uchu wa madaraka na huo ndio utambulisho wa viongozi wa siasa za upinzani wanaojenga hoja za demokrasia huru wakati wao hawawezi kuzitekeleza ndani ya vyama vyao, tabia hizi kwa lugha za kisiasa ujulikana kama “Unafiki wa kisiasa”

Japo kwa Afrika kinachofanywa na Maalif Seif si kitu kigeni katika ulingo wa siasa bali ni sehemu ya desturi na tamaduni za siasa za Kiafrika kuwa na viongozi ambao ni viganganizi wa madaraka kitu ambacho kisiasa ni dhambi na si dhamira njema katika ustawi wa taifa lolote lile kimaendeleo, viongozi wa namna hii uamini wao ndio zaidi kuliko wanachama wengine, Tabia hii kwa vyama vya siasa Tanzania ipo ndani ya mifumo ya siasa za upinzani kuwa na ubinafsi mwingi kuliko itikadi na maslahi ya chama na ndipo ugumu wa kupambana na CCM unapoanzia hapo.

Tayari Maalim Seif ametangaza rasmi nia yake ya kugombea kiti cha urais wa Zanzibar kupitia chama chake kipya cha ACT-Wazalendo, Baadhi ya wachambuzi wa siasa za ndani wanasema na kutabiri ujio wa Maalim kama kama tishio kubwa katika uchaguzi wa mwaka huu wa 2020, Sijui ni kipimo kipi wanatumia au pengine ni mahaba yaliyopitiliza kwa Maalim Seif, Lakini ukweli wa kimantiki ni kuwa Maalim ni Yule wa siku zote kinachomutofautisha ni chama tu na itikadi yake vinginevyo mvinyo ni uleule tofauti ni chupa tu.

Makala haya yanapingana na dhana hiyo ya utabiri unaofikriwa na baadhi ya wachambuzi wetu wa ndani badala ya kujenga hoja kwa nini uchaguzi utakuwa mgumu kwa Chama Cha Mapinduzi wanaishia kusema “Maalim ni mwamba wa siasa za visiwani” Ukweli wa kisiasa ni kwamba Maalim Seif Shariff si mwamba tena katika siasa za Zanzibar kutokana na Wazanzibar kuchoshwa na hoja zake za kila nyakati za uchaguzi kuwa zilezile.

Kwa Maalim hakuna jipya wala lolote lile lenye tija katika siasa za usasa na mambo leo hata kama amebadilisha chama chenye itikadi tofauti na chama chake cha zamani CUF Maalim atabaki kuwa Maali Seif Shariff Hamad ambaye kwa nyakati hizi siasa zake zimekuwa za kuonewa huruma, Kisiasa mwanasiasa anapofikia hatua ya kuanza kuendesha siasa za namna hii ni dalili rasmi ya mchoko katika medali za kisiasa na ni heri kustaafu kuliko kutaka huruma ya umma.

Ndio maana makala haya yanapata taabu ya kumuweka fungu gani Maalim aweze kuhesabika, Kisiasa na hasa katika siasa za uchaguzi wa mwaka huu Maalim angeweza kuhesabika yupo fungu lipi endapo tu angemtaguliza mwanasiasa mwingine badala yake kusimama kugombea kiti cha urais kupitia chama chake, kuendelea kusimama yeye kana kwamba wengine hawana uwezo wa kusimama katika nafasi hiyo ni udhaifu kisiasa na ni vigumu kupata fungu la kumuweka Maalim.

Pengine Maalim akipata fursa ya kupitia andiko hili atujulishe ni kwanini amekuwa akijiona yeye anafaa zaidi kuliko wanachama wengine, Je bila yeye hakuna mbadala, kisiasa na kidemokrasia haya ni maswali ya msingi ambayo wanachama na wakereketwa wa chama cha Maalim yawapasa kujiuliza mara mbili mbili kutofanya hivyo ni uzembe wa kifikra kisiasa na ni vigumu kuaminika kwa wapiga kura wa Zanzibar.

Kwa mantiki ilivyo kisiasa ni wajibu wa wachambuzi na wale wote wenye fikra kuwa uchaguzi wa mwaka huu kwa upande wa Zanzibar utakuwa mgumu kuliko nyakati zote, Jibu kwa fikra za namna hii zinajibiwa kuwa “si za kweli” Uchaguzi wa Zanzibar utakuwa mwepesi kuliko siku zote kwa sababu sera, falsafa, mitizamo, fikra na mawazo ya mgombea wa chama cha upinzani yanafahamika hata kabla ya kipyenga kupulizwa na dhana hii ipo wazi wa Wazanzibar wenyewe.

Kwa lugha rahisi kabisa uchaguzi katika dhana ya ushindi kwa Chama Cha Mapinduzi CCM utakuwa mteremko kuliko ule wa kitonga na huu si ushabiki wa CCM wala kupendelea upande Fulani bali ndio ukweli wa kimantiki unavyoonyesha kwa sasa katika medali za kisiasa, Hoja zipo wazi moja kuu kati ya zote ni watu kutaka mawazo na fikra mpya kutoka kwa mgombea ambaye itakuwa mara yake ya kwanza kusimama kama mgombea katika nafasi ya urais.

Aidha kupitia gazeti hili toleo lililopita niliandika na kuchambua juu ya uwezo na umahiri wa Dk. Hussein Mwinyi ambaye ameingia katika tano bora ya wagombea wa kiti cha urais upande wa Zanzibar, Bila shaka kwa uwezo wa Dk. Mwinyi chama chake kitampa ridhaa ya kusimama na kupambana na Maalim Seif ambaye kisiasa ni mchovu na mwanasiasa asiye na mawazo mapya ya kushawishi wapiga kura wa Zanzibar, Maalim wa enzi za mwaka 2000 akiwa na umri wa miaka 57 sio huyu Maalim wa sasa wa miaka 76 zama za Maalim zimepitwa na wakati na sasa hizi ni zama mpya za watu wapya na wenye mawazo mapya.

Kwa mantiki hiyo Wanzibar watapendelea kumsikiliza zaidi mgombea ambaye ni mpya katika nafasi hiyo ya urais na kutaka kusikia ana mapya gani ya kuwavusha Wanazanzibar katika shughuli za kimaendeleo kisiasa na kiuchumi ambayo Maalim pengine hana uwezo wa kuyatatua kwa sababu nyakati fulani aliwahi kuwa kiungo muhimu ndani ya serikali ya umoja wa kitaifa na pengine hakashindwa kuyatatua matatizo ya Wazanzibar.

Nia na dhumuni la makala haya si kumchomea utambi Maalim Seif Shariff Hamad kwa Wazanzibar bali ni uchambuzi unaosimama katika uwazi na mantiki ya kuonyesha nani ni bora zaidi katika kipindi hiki tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu hapo Oktoba na wala sio ubaguzi wa rangi kwa mgombea wa aina yoyote ile kama ilivyokuwa wakati wa chama cha ZNP maarufu kwa jina la Hizbu, Kwa nukta hiyo ni jukumu la Wazanzibar wenyewe kupima na kuona nani ni bora zaidi katika ustawi wa Wazanzibar na maendeleo yake.

dmutungid@yahoo.com
Maelezo mengi upuuzi mtupu
 
Fungu LA nyanya chungu

hivi kwanini makada wa CCM munaumia sana Maalim Seif kugombea uraisi kwa chama ambacho sio chenu?
 
Muungano hautakiwi Zanzibar na mwenye uthubutu wa kulisimamia hili kwa sasa ni Maalim Seif tu. Akifariki au kuchoka kiafya atapewa mwengine kijiti ila kwa sasa bado anaweza.
 
Back
Top Bottom