Freeman Mbowe, tueleze CHADEMA mlipompeleka Ben Saanane

Hizi habari bado zinaibua maswali mengi kichwan mwangu,,

Heshima kwa serkali ni vema iendane na heshima kwa sualama wa watanzania
 
Sasa naanza kupata picha Mlinzi Mushi wa Mbowe alimgesa Mlinzi wa Dr. Slaa . Nakumbuka tangu Dr. Slaa aondoke Chadema, BEN alikuwa kimya sana na nakumbuka aliwahi andika andiko la kuendelea kumtambua Dr. Slaa kama Hero wake. Hakika sasa napata picha taratibu
 
PAMOJA NA CHADEMA KUJIVUA KWENYE SAKATA LA KUPOTEA KWA BEN SAANANE, HILI LA MASHINJI KUGAWA VYETI MSITUNI HUKO BAGAMOYO LINAZUA MASWALI MENGI

Najua leo tutakuwa na Press Conference na waandishi wa Habari kueleza pamoja na mambo mengine tukio la kupotea kwa Ben Saanane pamoja na kuokotwa miili saba ya watu kwenye kingo za mto Ruvu huko Bagamoyo.

Binafsi nachukua fursa hii kuwapa pole ndugu jamaa na marafiki wanaoumia kutokana na kupotea kwa Ben Saanane. Pia nawapa pole ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza ndugu zao saba ambao chanzo cha vifo vyao hakijulikani na hata majina ya marehemu hayajulikani. Taarifa za awali kutoka kwa Serikali zinaonesha kuwa matukio hayo yanaweza kuhusishwa na wahamiaji haramu pamoja na ugaidi na kwamba imeahidi kutoa taarifa kamili baada ya uchunguzi kukamilika.

Hata hivyo, kuna kila harufu ya matukio hayo kubebwa na ajenda za kisiasa. Ukisoma mitandao ya kijamii, wanaonyooshewa vidole kutokana na matukio yote mawili ni CHADEMA na Serikali. Hii maana yake ni kwamba suala hili tayari limeshanajisiwa kwa manufaa ya kisiasa. Ukisoma comments nyingi za wafuasi wa CHADEMA hasa kwenye kurasa zao za facebook, anayenyooshewa kidole kwa wingi ni Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe kuwa ndiye mhusika mkuu wa tukio la kupotea kwa Ben. Kwa vyovyote vile, naungana nao makamanda kumnyooshea kidole Mbowe pamoja na uongozi mzima wa CHADEMA kutokana na kutuacha kwenye taharuki wafuasi wake tusijue nini kinaendelea.

Najua tamko letu la leo tutajivua kabisa kuhusika na matukio yote mawili. Hata hivyo, polisi wakifuatilia kwa kina, CHADEMA hatutakwepa kuhusika na matukio hayo. Kwa nini nasema hayo? Hebu tutulize akili zetu na tuanze kufikiri critically.

Novemba 10, 2016, CHADEMA kupitia kurugenzi ya Ulinzi na Usalama ya chama tulipeleka makamanda wetu 10 Bagamoyo kwenye shamba letu la ekari 108.

Novemba 24, tulipeleka makamanda wengine 12 ambao waliungana na wale 10 wa awali

Desemba 6, makamanda wengine zaidi ya 30 walienda kwenye shamba hilo kwa maelezo kuwa wanaenda kufanya maandalizi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa kilimo. Makamanda hao walienda bila ya zana zozote za kilimo ambapo zana hizo walizikuta huko shambani zinawasubiri. Makamanda walipelekwa shambani huko mara baada ya familia ya Ben kutoa taarifa polisi juu ya kupotea kwa Ben.

Makamanda karibu wote waliopelekwa kwenye shamba hilo ni wafanyakazi kwenye kurugenzi yetu ya Ulinzi na Usalama.

Taarifa nilizonazo ni kwamba, kaeneo ambako watu hao walilima hakazidi hata mita 20.

Baada ya hapo, Jumamosi Desemba 10, 2016, makamanda walikabidhiwa vyeti huko huko msituni. Ninaita msituni kwa sababu hilo linaloitwa shamba ni pori tupu ambapo hakuna mazao yoyote ya msimu wala ya kudumu. Mbaya zaidi, eneo ambalo limelimwa lipo katikati ya shamba hilo ili majirani zetu wasijue nini kinaendelea.

Kwa hakika hii inatia shaka sana na inakuwa ni vigumu kujivua na hivi vidole tunavyonyooshewa kutokana na kupotea kwa Ben. Kutokana na mazingira haya, najiuliza maswali yafuatayo.
1. Kwa nini miili ya watu ipatikane huko Bagamoyo tena umbali mfupi kutoka lilipo shamba letu?

2. Makamanda wetu waliopelekwa kwenye shamba hilo na kukaa kwa zaidi ya siku 20 msituni walikuwa wanafanya kazi gani? Kama ni kwa sababu ya kilimo, mbona eneo lililosafishwa halizidi hata mita 20? Kuna nini hapo?

3. Katibu Mkuu wa CHADEMA, Vincent Mashinji anaonekana anagawa vyeti huko msituni kwa makamanda wetu. Je anaweza kutuambia hivyo vyeti ni vya mafunzo yepi? Na kwa nini vitolewe msituni kwenye shamba letu ambako tuliweka maturubai ya kutosha kuhakikisha kuwa shughuli inafanyika kwa ukamilifu wake?

4. Kwa nini Mashinji agawe vyeti huko msituni kipindi ambacho chama kina taharuki kubwa ya kupotea kwa Ben Saanane?

5. Kwa nini matukio haya yamefuatana? CHADEMA kupeleka makamanda msituni shambani kwetu, kupotea kwa Ben Saanane na kupatikana miili saba umbali mfupi kutoka kwenye shamba letu?

6. Kwa nini Katibu Mkuu, Mashinji ametoa maelekezo kwa wapambanaji wetu mitandaoni tuache kutoa hoja zinazoweza kuihusisha CHADEMA na kupotea kwa Ben? Kwa nini Mashinji amemwamuru Malisa atoe bandiko lake kwenye ukurasa wake wa facebook lililoshutumu kitendo cha Tanzania Daima kutoipa kipaumbele taarifa ya Umoja wa Kizazi cha Kuhoji, UTG?

Maswali ni mengi ambayo sina hakika kama nitapata majibu yake. Nimalizie kwa kuiomba Serikali kupitia Jeshi la Polisi ambalo linaendelea na uchunguzi wa tukio la kupotea Ben Saanane kufanya yafuatayo;

1. Imhoji Hilda Newton Msigala ambaye ni swahiba mkubwa wa Ben Saanane na inadaiwa kuwa wana uhusiano wa kimapenzi tangu Julai 2016. Hilda Newton ndiye Novemba 26, 2016 aliyeutangazia Ulimwengu kuwa Ben Saanane yupo Afrika ya Kusini na ndiye aliyetutoa hofu kutokana na kupotea kwa Ben kabla hajabadilika tena Desemba 6 baada ya ndugu wa Ben kuripoti polisi tukio la kupotea kwa Ben. Huyu ni mtu muhimu sana kwa sababu ni swahiba wa Ben, ni Red Brigade ambaye ameshiriki kusafisha shamba letu na amepewa cheti msituni kwa kazi hiyo. Huyu ana siri kubwa sana juu ya Ben Saanane.

2. Polisi wamtake Katibu Mkuu wa CHADEMA atoe maelezo ya nini kilikuwa kinafanyika kule msituni kwenye shamba letu na vile vyeti alivyokuwa anagawa ni vya mafunzo yepi.

3. Kwa kuwa Mwenyekiti wetu anajua nini kilikuwa kinaendelea shambani kwetu, naye ahojiwe.

4. Polisi wailazimishe CHADEMA iwapeleke shambani kwao ili ikafanye ukaguzi ili kubaini iwapo Ben amefichwa msituni huko au kama amefariki basi atakuwa amezikwa msituni huko. Najua viongozi wangu wakisoma bandiko hili wanaweza kufanya lolote, ila naamini kuwa hawatafanikiwa kuficha kila kitu.

Niwaombe sana makamanda wenzangu. Huu ni wakati mgumu sana. Kikulacho Ki Nguoni mwetu. Tutafakari na tuchukue hatua. Tuache kulalamika

FROM Kada wa CHADEMA
 
Kwa mtizamo wangu bado naamini Mabosi wa Ben wanajua alipo huyu kijana kuliko kumnenea tu mabaya ndo maana mabosi hao hawahajahangaika kumtafuta hadi habari zimetanda kwenye mitandao.

Huenda ameshindwana na Mabosi wake akaamua kujificha kusikojulikana. Je akijitokeza atakuwa na kosa la kujificha, kisheria?
 
Endlelea kua na mtzamo huo.Kama ni kweli hvo CCM na serikali kwa ujumla wana kaz ya kuuthibitshia umma CDM ni waongo.
 
Atakuwa amezira baada ya mkuu kumkanyaga mpenzi wake Hilda newton waliyeanza mahusiano Nov 2016
 
Kwa mtizamo wangu bado naamini Mabosi wa Ben wanajua alipo huyu kijana kuliko kumnenea tu mabaya ndo maana mabosi hao hawahajahangaika kumtafuta hadi habari zimetanda kwenye mitandao.

Huenda ameshindwana na Mabosi wake akaamua kujificha kusikojulikana. Je akijitokeza atakuwa na kosa la kujificha, kisheria?
hata kwa Mwangosi ulianza hivyohivyo kwa kusema ameuwawa na kitu kilichotupwa kutoka kwenye kundi la wapenzi wa chadema p

hata kwa Mwangosi ulianza hivyohivyo kwamba,ameuwawa na kitu kilichotupwa kutoka kwa wanachama wa chadema picha zikakuumbua na Ulimboka ulija hivyohivyo kwamba,ametekwa na chadema bahati hakufa akaeleza yaliyompata ukaumbuka na leo unakuja hivyohivyo utaumbuka tu,
 
yaani chadema wanatumia kivuli cha polisi na ccm kutekeleza uhalifu wao kila wakati. Chacha Wangwe, Alfonce Mawazo, Mabomu Soweto, na huyu kijana tena!
 
Kwa mtizamo wangu bado naamini Mabosi wa Ben wanajua alipo huyu kijana kuliko kumnenea tu mabaya ndo maana mabosi hao hawahajahangaika kumtafuta hadi habari zimetanda kwenye mitandao.

Huenda ameshindwana na Mabosi wake akaamua kujificha kusikojulikana. Je akijitokeza atakuwa na kosa la kujificha, kisheria?
Suala la Max kukamatwa unajua undani wake?
Still mmefail kuuficha ukweli.
JF bado ipo na mkiifutia leseni itakuwepo pia
 
Back
Top Bottom