Freeman Mbowe mwanasiasa, mfanyabiashara na mkulima asiye ogopa hasara

Hebu kamateni hiyo msimuone mtu ni wa kisport wa njaa za ruzuku.
Freeman Aikaeli Mbowe amezaliwa 14 Septemba 1961 Wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro ni mwanasiasa Mtanzania, mwanachama na mwenyekiti wa Chama cha kisiasa cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Alikuwa mmoja wa waasisi wa CHADEMA mwaka 1992. Freeman Mbowe alikuwa mbunge wa Jimbo la Hai lililopo mkoa wa Kilimanjaro tangu mwaka 2000 hadi 2020.

Familia ya Mbowe
Freeman Mbowe alizaliwa na wazazi Aikael Alfayo Mbowe na Mama Aishi Ephraimu Shuma akiwa mtoto wa 10 kwa baba yake na mtoto wa 9 kwa Mama yake, ivyo yeye kuwa mtoto wa mwisho kwa baba na Mama.

Freeman Mbowe alibatizwa 09,12,1961 siku ya Uhuru wa Tanganyika na kupewa jina Freeman maana yake mtu huru. Baba wa Ubatizo wa Freeman Mbowe alikuwa Mwalimu Nyerere.

Nilizaliwa mwaka 1961 mwaka ambao nchi yetu ilipata uhuru tarehe 14/9/1961 na nikabatizwa siku ya 9/12/1961 siku bendera ya mwingereza yaani (Union Jack) inashushwa na mimi nikabatizwa siku ya uhuru kwa maana 1961 nikapewa maji ya uzima ya ubatizo na ndio sababu nikapewa jina la Freeman ikiwa na maana mtu huru kwa sababu nilibatizwa siku ya uhuru baada ya kuzaliwa mwaka wa Uhuru.Alisema Mbowe kwenye kipindi cha Speaking out with Tundu Lissu

Uhusiano wa Mwalimu Nyerere na familia ya Freeman Mbowe ulianzia wapi?

Kwa mujibu wa Freeman Mbowe kwenye Mahojiano kati ya Tundu Lissu na Freeman Mbowe yaliyofanyika katika kipindi cha Speaking out with Tundu Lissu, alisema kuwa Julius Kambarage Nyerere na Aikael Alfayo Mbowe walikuwa na mahusiano ya karibu sana na mahusiano yao yalianzia kwenye harakati za kutafuta uhuru wa Tanganyika.

Lissu: Hebu tuambie Mzee Mbowe alikuwa na connection gani na Mwalimu Nyerere au na mambo ya kisiasa, siasa za TANU?

Mbowe:Kwa kweli nikiri tu kwamba wakati Mzee anaanza kufanya mambo ya siasa na akina Mwalimu na wazee wenzake mimi nilikuwa bado ni mtoto mdogo sana lakini historia nimeikuta simulizi nimezipata maandiko nimeyakuta, Mzee alikuwa na mahusiano ya karibu sana na Mwalimu Nyerere na mahusiano yao yalianzia kwenye harakati za kutafuta uhuru wa Tanganyika.

Mzee Mbowe alikuwa na umashuhuri katika Tanganyika kanda ya Kaskazini katika mikoa ya Kaskazini ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara na alikuwa na uhusiano na watawala wa kiasili, kuanzia Mangi Maruma wa Rombo, Mangi Shangali wa Machame, alikuwa karibu nao kutokana na umashuhuri wake kabla ya uhuru.

Katika mazingira kama hayo baba alikubaliana na wenzake kadhaa kuhamasisha harakati za kutafuta uhuru wa Tanganyika katika kanda ya Kaskazini kwa kuwa watawala wa jadi walikuwa na nguvu sana na walihitaji mtu ambae alikuwa na ushawishi mkubwa sana na waliweza kuingiza TANU kanda ya kaskazini hasa sehemu ya Kilimanjaro na hapo ndio mahusiano ya familia ya Mwalimu ilipoingia kwenye familia yetu na alikuwa na ukaribu hata na Oscar Kambona na wazee wengine kadha wa kadha ambao walishiriki katika harakati za uhuru wa nchi kwa hiyo historia ya Mwalimu na baba ilikuwa hivyo.

Picha mnayoona hapo huyo mwenye koti refu akisalimiana na Nyerere ni mzee Aikaeli Mbowe.Baba mzazi wa FreeMan Mbowe.Hapo ametembelewa nyumbani kwake Machame Kilimanjaro na rafiki yake mkubwa Raisi Nyerere.Angalieni huo mjengo hapo upo kijijini
 

Attachments

  • mbowe.png
    mbowe.png
    321.3 KB · Views: 3
Harakati ngumu na nzito zipi ?!!

Kuwa mwanasiasa wa chama kikuu cha upinzani ?!!

EL COMMANDANTE CHE GUEVARA aliacha ukwasi wa familia yake pamoja na UDAKTARI wake wa binadamu kusonga mstari wa mbele na kushika silaha si tu bara la amerika kusini bali mpaka misitu minene ya KONGO...

Mh.Mbowe hajamaliza shahada yake ya chuo kikuu.....hajawahi kuingia msituni na makundi Kama yale ya ERNESTO......

Nionavyo ni "passion" tu....kwani hata hayati Nyerere alitokea katika familia ya KICHIFU ambayo Mbowe hajatokea huko.......

Sijajua kule Ujerumani na wale "CDU" ukimuacha SABODO...walikuwa wanapata mapesa kiasi gani kuisimamisha demokrasia.....

Ujaji wa hayati Lowassa Chadema:

Mbowe si tajiri wa kihivyo....si tu msimamo wake wa kusema hayati Lowassa amekuja CDM na *assets" bali MAPESA...

Baada ya yule mshenga....gia akaibadili angani.....ndicho kipindi ambacho CDM ilipata magari mengi kwa ajili ya kampeni ,wakaungwa mkono na matajiri wengi ,mwishowe wakaingiza WABUNGE WENGI pale Dodoma.....

"Aliporejea kwao CCM"....kilio kikubwa kikasikika pale UFIPA

Hayati Lowassa alichoka KUKAMULIWA....mh.Mbowe alijua kweli "kuitumia ile asset"

Mh.Mbowe anakuzwa kuliko alivyo.....

#Nchi Kwanza
Dah ! watu bana sasa mbowe ashike BUNDUKI ya nini ashike wapi sasa kwa ajili ya nini

Mkuu SILAHA PESA KISU MZIGO
Mtu yoyote SMART msingi kwake ni maneno
 
Una uhakika na unachokisema ?huyu mwenyekiti angekuwa na huyo utajiri wa huku Jamii forum basi


✅✅✅✅
kama umezaliwa baada ya uhuru na hukuona bendera ya union jack you have got no right to speak however you can comment and be corrected.
 
Una uhakika na unachokisema ?huyu mwenyekiti angekuwa na huyo utajiri wa huku Jamii forum ingekuwa ni hatari sana.
Wewe ukoo wenu mzima mkijikusanya hamuwezi fikia utajiri wa Mbowe siasa ni damu tu na tena usije shangaa huyu Mbowe unayemuona akawa ni Pro-CCM

Wewe ukoo wenu mzima mkijikusanya hamuwezi fikia utajiri wa Mbowe siasa ni damu tu na tena usije shangaa huyu Mbowe unayemuona akawa ni Pro-CCM
kama umezaliwa baada ya uhuru na hukuona bendera ya union jack you have got no right to speak however you can comment and be corrected.
You are trying to overate Mbowe Farmily of which I have the righty to question.
 
Miaka 64 iliyopita familia moja ya kitajiri mkoani Kilimanjaro ilipata mtoto wa mwisho wa kiume ikamuita "Freeman" kwa maana ya mtu huru. Jina lake na mazingira yake ya malezi na makuzi ndiyo kitu kinachovutia watu wengi kutaka kumfahamu zaidi.

1.Imewezekanaje mtoto wa familia ya akitajiri,ambayo ilikuwa na kila kitu cha muhimu anachohitaji binadamu yeyote na kuridhika navyo kuingia katika harakati ngumu na hatari?

Freeman alilelewa maisha ya kawaida sana kwa kusoma shule za vijijini Machame kama Rambo Primary Kolira Secondary school, Kibaha Secondary school na kidato cha tano na kidato cha sita akamalizia Ihungo high school

2.Familia nyingi zinasomesha watoto ili wapate kazi au fedha za Kujikimu ktk maisha yao,na wakisha pata vitu hivyo hujihesabia kuwa wameridhika ama hujiona kufanikiwa kimaisha.

Lakini ni tofauti na Freeman ambaye hakuridhishwa na utajiri wa kipekee wa familia yake,umaarufu wa biashara za Baba yake tangu enzi za mkoloni, ingali amezungukwa na masikini kila kona, anajiunga nao na kuamua kuanzisha vuguvugu la safari ya madaliko kupitia siasa.

3.Kama ilivyo kwa familia nyingi, kama Baba yako angekuwa ni mtu wa karibu na Rais na kutengeneza familia hizi mbili kuwa rafiki kiasi cha Rais Nyerere kukubali kuwa Baba wa ubatizo wa watoto wa Mzee Aikael Mbowe au Nyerere kumtuma Mzee Aikael Mbowe kwenda kutoa posa ya ndoa ya mtoto wake Makongoro Nyerere Mkuu wa Mkoa Rukwa wa Sasa) kwa niaba yake

Ingetarajiwa ukaribu wa Baba yako na viongozi wa nchi ungeathiri mlengo wa kisiasa kwa kutaka usaidiwe kuwa mwanasiasa kwa Jina la Baba yako kupitia Chama tawala. Tofauti na Freeman ambaye ukaribu wa Baba yake na Rais Julius Kambarage Nyerere haukumtamanisha au kuvutiwa na siasa za chama tawala kwa mseleleko wa jina na heshima ya Baba yake kwa Rais Nyerere.

4.Miaka ya Mwanzoni mwa 1980 baada ya kumaliza masomo Freeman Mbowe kuruta wa JKT kutoka Ruvu 32KJ na Lugalo kupitia operesheni Imarisha. 1982 aliajiriwa Benki Kuu kama Afisa wa Benki haikumfanya awe mtumwa wa ajira na kuona kama fadhila kutoka kwa chama tawala,aka acha kazi na kwenda kujitafutia maisha kwa kuanzisha biashara zake binafsi.

5.Miaka ya 1980 utajiri wa Familia ya Freeman Mbowe na Mohamed Dewji ulikuwa karibuni unalingana au Familia ya Freeman Mbowe ilikuwa tayari familia ya Wafanyabiashara wenye mafanikio zaidi kuliko ya Dewji.

6.Mwaka 1985 akiwa Kijana wa miaka 24 tu kupitia Idara ya Fedha za nje (foreign exchange) ya Benki Kuu tayari Freeman Mbowe alikuwa na exposure ya biashara ya Kimataifa, uthubutu na ubunifu wa hali ya Juu.

Aliamua kuacha Kazi Benki Kuu na kwenda kusoma akiwa tayari ana kampuni zake za biashara za kuingiza na kusafirisha bidhaa kupitia F&M Export Company LTD mwaka 1985 kampuni ya uvuvi wa samaki aina Kamba na Kamba kochi akiwa anamiliki boti moja ya kwake binafsi aina ya MV RSVP

Na baadae Freeman Mbowe akianza kupeleka Matunda nje ya nchi Kwa kutumia shirika la ndege la Gulf Air na baadae kuanzisha Kampuni ya "KILI VAGE" Kwa ajili ya kuuza Mbogamboga nje ya nchi.

7.Freeman Mbowe akiwa tayari mfanya biashara Mkubwa akaingia katika biashara ya majumba (Real estate) kwa kuingia ubia wa miaka 90 na Msajili wa Nyumba/ National Housing kwa kukiendeleza kiwanja namba 725 na 726/11 vya mtaa wa Mkwepu na Makunganya kwa asilimia 75 za Mbowe na 25 za National Housing palijulikana kama Club Billcanas.

Freeman Mbowe akajitanua na kununua nyumba za biashara ya kupangisha (apartments) London Uingereza,Nairobi Kenya, Johannesburg South Africa, Dubai na kumiliki na kuendesha Hotel ya Aishi Protea Hotel, Machame.

New Palace Hotel ilikuja kujulikana kama Mbowe Hotel
kwa sababu New palace Hotel alipatiwa Mzee Aikael Mbowe na serikali baada ya serikali kutaifisha kiwanja na Hotel yake ya SPLENDID HOTEL mali ya Mzee Aikael Mbowe iliyokuwa Mtaa wa Samora kwa sasa ndipo ilipo Twiga Banckorp

Katika Kujichanganya makundi mbali mbali ya Jamii, amewahi kuwa mfadhili wa Club ya Dar Young Africans (Yanga) kupitia biashara yake ya Club billcanas .

8.Freeman Mbowe akaonyesha uthubutu kuwa mtu binafsi na mfanyabiashara wa kwanza kuleta wanamuziki wa kutoka DR Congo kufanya maonyesho ya muziki kabla ya mtu yeyote.

9.Freeman Mbowe akiwa na miaka 29 tu akawa muasisi kijana wa CHADEMA, na akawa kijana wa kwanza kufanya kazi kubwa ya kuongoza "wing" ya vijana ndani ya CHADEMA

Mwaka 2004 baada ya kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA alianza kuwekeza nguvu na akili zake CHADEMA kwa kufanyia maboresho ya katiba, rangi Kadi, bendera, muundo wa CHADEMA kutoka mikononi kwa wazee wake Edwin Mtei na Bob Makani

10.Mwaka 2005 akiwa Mwenyekiti Kijana, akiwa na mwaka mmoja ofisini alilazimika kuingia katika kinyang'anyiro cha ugombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na mshindani wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Freeman Mbowe alipata idadi ya Kura 668,756 sawa na asilimia 5.88%,Wabunge watano wa majimbo na viti Maalum 6 (wabunge 11) na madiwani 103 lakini alifanikiwa kukitangaza sana chama chake cha CHADEMA na kukifanya kiwe midomoni mwa Watanzania

Staili yake ya pekee ya kutumia usafiri wa Helicopter na muasisi staili na aina hiyo katika kampeni za 2005 na vazi lake gwanda la kaki zilivutia sana na kumfanya yeye na CHADEMA kujulikana sana nchi nzima.

10.Kuanzia mwaka 2005 Freeman Mbowe amekuwa Kiongozi ,mfadhili na mwanamageuzi mkubwa wa kutafuta vijana wenye vipaji vya siasa kuwalea na kuwakuza. Mifano katika eneo hili ipo mingi sana na kujivunia.

John Mrema (UDSM), Zitto Kabwe (UDSM, Halima Mdee (UDSM), John Mnyika (TYVS), Benson Kigaila (UDP), Msafiri Mtemelwa (NCCR), Kitila Mkumbo (UDSM), David Kafulila (UDSM), David Silinde (UDSM), John Heche (SAUT), Juliana Shonza (UDSM), Joshua Nassari (UDSM), Salum Mwalimu (VODACOM), Boniface Jacob (UDSM), Deogratius Munisi (UDSM), Patrobas Katambi (SAUT), Godlisten Malisa (SAUT) Emmanuel Ntobi (NBC),Catherine Ruge (NBC),Vincent Mashinji (Chama cha Madaktari) na wengine wengi.

11.Freeman Mbowe amekuwa kiongozi mwenye ushawishi mkubwa wa kuwavutia wanasiasa wengine kuhamia CHADEMA kutoka vyama vingine vya siasa. Wapo wanasiasa wengi walitoka katika vyama vyao na kuhamia CHADEMA na kuwa wanasiasa wakubwa na mahiri sana.

Dr. Aman Walid A. Kabourou (USA), Dr.Wilbroad Peter Slaa (CCM), Erasto Tumbo (UDP), Antony Komu (NCCR), Msafiri Mtemelwa (NCCR), Prof Mwesiga Baregu (NCCR), Tundu Lissu (NCCR), Prof Abdallah Safari (CUF), Mabere Nyaucho Marando (NCCR), Wilfred Lwakatare (NCCR), Godbless Lema (TLP), Ester Bulaya (CCM), Arcado Ntagazwa(CCM), Makongoro Mahanga (CCM),Razaro Nyalandu (CCM) PM-Frederick Sumaye (CCM),PM-Edward Lowasa (CCM).

12.Freeman moja ya sifa yake ni pale anapo ona kipaji cha mtu ktk siasa hana wivu wala haogopi kuwekeza kwake.

Alipomuhitaji Dr.Wilbroad Peter Slaa Kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA hakuogopa Kumnunulia nyumba ya Kuishi Mbweni na kumtafutia gari aina ya Landcruiser V8 double exhaust,Diesel engine apige kazi nchi nzima kukuza na kuenezea CHADEMA.

Ukiondoa mwaka 2005 alipogombea yeye binafsi Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini chaguzi zingine 3 ametafuta na kushawishi wagombea Urais kwa ticket ya CHADEMA na Kuwekeza nguvu na fedha kwa wagombe wake katika michakato ya kampeni

Mwaka 2015 ukiondoa umashuhuri na ukubwa mgombea urais wa CHADEMA Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowasa aliyehamia CHADEMA tarehe 28 July 2015,ikiwa ni wiki mbili tu kabla ya kampeni.

Freeman alikuwa ameshajipanga kwa uchaguzi na kuagiza vifaa vya Kampeni kama vile bendera,Skafu,Vitambaa,Magari,Stage na PA system
za kampeni kutoka Guangzhou,China baada ya kuuza moja ya nyumba yake binafsi April 2015 ya nchini uingereza kupitia kampuni ya Artetra World Wide Limited yenye anuani S.L.P 293816 ktk Jengo la World Trade Center, Mtaa wa Sheikh Zayed,Dubai.

13.Pamoja na kukuza na vipaji vya vijana na kuwatengenezea mazingira mazuri vijana wadogo katika siasa za Tanzania. CCM imekuwa ikiwinda vijana wake na kuwachukua kwa ahadi ya kuwapa madaraka au fedha

Wengine Wamekuwa na shukrani za Punda pale wanapopata majina na umashuhuri huanza Kuona CHADEMA na Freeman Mbowe ni gunia la mazoezi la matusi na udhalilishaji kwa minajili ya kujitengenezea thamani kwa CCM wanapoamua kuhamia huko.

Pamoja na yote hayo Freeman Mbowe ni Mwanasiasa, mfanyabiashara na mkulima asiyeogopa hasara. Ameendelea kutengeneza vijana wengine kila siku bila kuchoka wala kujali kama ipo siku na wao wataondoka CHADEMA kwa matusi na kejeli kubwa kwake au CHADEMA.

Ukiwa mtu unayeogopa hasara huwezi kuwekeza katika biashara, ukiwa mtu unayehofia hasara huwezi kuwa mkulima, ukiwa unaogopa matusi na udhalilishaji huwezi kuwa mwanasiasa,mahiri, bora na mkubwa.

Heri ya Kuzaliwa Freeman Aikaeli Mbowe

Salamu kutoka kwa Mlinzi wako wa zamani..

Boniface Jacob
Ex-Mayor Kinondoni na Ubungo
0712 239 595
Diwaniubungo@gmail.com

Pamoja na tofauti za siasa hakuna anayebisha Mbowe ni Husler
 
Back
Top Bottom