Mbalamwezi
JF-Expert Member
- Sep 30, 2007
- 800
- 172
Hakuna tofauti ya ulaji wa mafuta kati ya injini mbili zenye ujazo sawa wa 2000 lakini tofauti ni idadi ya cylinder. Faida moja tu ya kuwa na cylinder nyingi kuliko chache ni kwamba kishindo kinachotokea baada ya mlipuko wa injini (impulse) kwa kila mzunguko wa injini (engine revolution) kinakuwa kidogo zaidi na hivyo kuifanya injini isiwe na kelele ukilinganisha na cylinders chache. Kuelewa hilo, linganisha mlio wa injini yenye cylinder moja (baadhi ya pikipiki, mashine za nafaka vijijini) na injini zenye cylinder nyingi kama pikipiki za polisi zile kubwa, au gari zenye cylinder 4 linganisha na zenye 6 au 8. Kimsingi, cylinder nyingi zinafanya injini iwe tulivu na smooth ride.
Mambo yanayoweza kusababisha hata injini yenye cc chache ikala mafuta mengi ni haya: air cleaner chafu, plug zimechoka, upepo wa matairi mchache, matairi mazito (kutegemea na ubora au mapenzi ya mtengenezaji), mzigo mzigo kwenye gari, non wheel alignment, oil nzito, bodi ya gari imeongezewa takataka zaidi ( bulkbars, na mapambo yasiyotoka kiwandani) na vingine vingi.