Foleni ya masaa sita yawatesa wakazi wa Mbagala, watembea kwa miguu

Sio lazima kupanua barabara. Kinachotakiwa ni kuwa na gari za uokoaji zenye uwezo mkubwa. Ingekuwa gari dogo limepata ajali, hata kama halikuziba njia, lingechukuliwa na gari za uokoaji zinazokaa karibu na wanapokaa maaskari wa usalama barabarani. Kilichokosekana hapo ni uwezo wa mtambo wa uokoaji wa kuliondoa lori hilo barabarani haraka.
Ingawa yale magari ni gharama sana kuyanunua kwa wakati mmoja ila ukinunua yanadumu muda mrefu sana kwani ajali za hivyo sio za mara kwa mara.Tuiongezee serikali uwezo wa kukusanya mapato yake ikiwemo kodi kwa kuendeleza utaratibu wa kudai risiti kila tunapofanya manunuzi/malipo ili ipate uwezo wa kununua hayo magari hata nchi nzima.
 
Wananu nua magari ya maji washawasha kwa wingi ili kunyanyasa raia lakini magari muhimu kama haya, ambulance, zimamoto kwao hayana kipaumbele.

Sio lazima kupanua barabara. Kinachotakiwa ni kuwa na gari za uokoaji zenye uwezo mkubwa. Ingekuwa gari dogo limepata ajali, hata kama halikuziba njia, lingechukuliwa na gari za uokoaji zinazokaa karibu na wanapokaa maaskari wa usalama barabarani. Kilichokosekana hapo ni uwezo wa mtambo wa uokoaji wa kuliondoa lori hilo barabarani haraka.
 
Serikali ingepaangalia mbagala kwa jicho lengine kabisa. Maana mbagala Na sehemu zake kuna idadi kubwa ya watu wanaoitegemea kilwa road Kama barabara yao kuu ya uchumi. Naishauri selikali ijenge reli ya mwendo kasi pengine hata adha ya usafiri itapungua Kama sio kuisha
 
Tatizo la Kilwa road kuanzia mtongani sijui kwa aziz ally zaidi ya hio main road hakuna njia ingine ya pembeni. Ukiziba main road tu basi labda upite kongowe utokee kigamboni.
upo sahih kabisa mkuu hakuna njia mbadala kuanzia pale mtongani maana hata yale mabas ya kusn yalikuwa njian tu mitaa ya mtongan na aziz ali mpaka njia ilipofunguliwa
 
kuna haja kubwa ya kuchonga ile barabara ya kilungule mpaka kwenye ile road inayokwenda buza ili kilwa road ikiwa na majanga kama jana bac watu wahamie huko
 
Wananu nua magari ya maji washawasha kwa wingi ili kunyanyasa raia lakini magari muhimu kama haya, ambulance, zimamoto kwao hayana kipaumbele.
Naona uzidi kuonyesha ulivyokariri, yule mbunge wenu kapigwa ban kwa sababu hizo hizo za kukariri mambo.
 
Mwendokasi mbagala lini wakuu.. mateso ya jana si mchezo.
 
Yaani tupo ndani ya Taifa ambalo watu wote wenye mamlaka hawafikiri zaidi ya ubinafsi
Mpaka leo barabara yenye ongezeko la watu inachukua gari moja tu?Na watu wanaibuka kujisifia wameleta maendeleo
 
Back
Top Bottom