Fikra za Mwalimu: Hizi hapa.. mzikubali au mzipinge!

Hongera Mzee Mwkjj kwa kuleta hoja nzuri hapa!
Naona maoni mengi mazuri na ninakubaliana na wale wanaosema ya kuwa political na economic reality ya Nyerere katika miaka ya 60 na 70 ilikuwa tofauti na ya sasa.
We are nostalgic kwa wale ambao tulipata kuishi wakati huo for oe reason or another. Wengine wanalilia 'usawa'kwamba kulikuwa hakuna ufisadi na viongozi walifuata maadili, wengine wanalilia stability, etc. Lakini memories are always molded kufuatana na individual.
Nyerere made his mark on this country no denying and not necessary for the better! Hebu niangalie hii essay aliyoiweka hapa Mwkjj, Mwalimu alizungumzia change ambayo tunajua ni zaidi ya kishosalisti. But i think that it is not a consensus and he knows:

THE NEED TO CHANGE:​

The only certain thing is that if we forget any of our principles, even when we are ignoring or breaking them, then we shall have betrayed the purpose of our revolution and Africa will fail to make its proper contribution to the development of mankind.

But the opportunity is before us provided we have to courage to sieve it. For the choice is not between change or no change; the choice for Africa is between changing or being changed – changing our lives under own direction, or being changed by impact of forces outside our control.

In Africa there no stability in stagnation in this twentieth century; stability can only be achieved through maintaining balance during rapid change.

Tanzania has chosen to ride and try to harness the whirlwind which is sweeping through this continent. We know that some human dislocation is inevitable in this process, but we believe that much more would ultimately be involved in doing nothing. For we recognize that to try to maintain the status quo is to try to ignore the world.

We prefer to participate in the shaping of our own destiny, and we believe that we have the resolution and the ability to overcome difficulties and build the kind of society we want. For those with courage to aspire, to believe, and to work, Tanzania is a challenging and exciting land. It is my privilege and my happiness to dedicate myself to its future.[/B]

SWALI: Je fikra hizo za Mwalimu kuhusu haja ya Africa na Tanzania kubadilika zimepitwa na wakati na tusiziangalie tena. Je hoja yake kuhusu haja ya Afrika and hence Tanzania kubadilika ina makosa gani?

Jamani hebu angalieni contradiction in this essay, hivi Nyerere hakujua ya kuwa forceful dislocation of people will lead to dicontentment? Alifanya mashauriano na hawa watu kabla ya kuwahamisha na kuwalazimisha kuishi katika mazingira magumu? Anaposema 'we'anawazungumzia akina nani?
The problem with Nyerere was hata kama with good intentins lakini aliamua ya kuwa he knows best na alifanya alichotaka na hakuchukua ushauri. I like the fact that he after all did take responsibility lakini that does not absolve him of the fact that he ruined the lives of hundreds of thousands if not millins of Tanzanians. No, the change that Nyerere speaks about has no place or role in current Tanzania. Hatuwezi kurudi kwenye Azimio la Arusha.
 
Kwanza hoja za kutumia mifano ya Yesu alivyo fanya siikubali. Sio wote wanaamini Yesu ni mfalme wa wayahudi. Hususan wakuu wa Makuhani!

Pili, tunajadili mawazo ya Nyerere, sio Watanzania walivyo kubali mawazo yake. Hilo jadala lingine.

Tatu, 'Preventive Dentention Act' ya nchi nyingine ninayo ijua mimi ni ya USA. (We utanambia unayo ijua wewe na inavyo fanya kazi). Hiyo sheria haipingani na sheria mama yao. Katiba yao hairuhusu mtu kufungwa bila kushitakiwa isipokuwa kama ni mwanajeshi wa adui. Sasa cheki basi: Ukiambiwa wewe ni mjeshi wa adui, katika katiba yao una haki ya kufungua kesi kupinga hilo.

Sheria ya Nyerere haikuwa na hiyo. Alikuwa anawasweka wanao mpinga pinga kituo cha Oysterbay, halafu kila Jumapili anapita kwenda kusali Saint Peters, mita chache tu toka aliko wafunga watesi wake wa kisiasa bila hatia.

Mwisho, ndugu yangu uliyeorodhesha mabaya ya viongozi wengine ambayo Nyerere hakuyafanya, hiyo hoja nyanya. Ukimuongelea Nyerere kwa kutuambia matusi ya Malecela hiyo haituambii chochote kuhusu wasifu wa Nyerere. Kutotukana ni wajibu. Wewe huwa unapata zawadi ukiwa unazingatia muda wa kufika kazini kila siku? Unapata mshahara. Lakini ukifanya kazi zaidi ya ulivyotakiwa ndio unapewa posho, au sivyo?

Nikisema Nyerere kaharibu, unajibu hakuna aliyekamilika. Ndio. Hicho ndicho ninacho kisema. Nyerere kaharibu. Sijasema Nyerere mtakatifu, au kuna mtakatifu, au alitakiwa awe mtakatifu. Nilikuwa natumia tasnifa. Na kama ukisema hakuna aliyekamilika kwa hiyo tusikosoane, basi hatungeanzisha huu mjadala. Ushanielewa?

Kwa hiyo usijibu hakuna mtakatifu. Unanisaidia kusema ninacho taka kusema. Nyerere kaharibu!
 
Yes Mwl JKN hakuwa malaika lakini hakufikia kiwango cha kutuambia

1.You can go to hell
2. Kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe (Elimu)
3. Mtakula Nyasi...ndege ya Rais lazima inunuliwe
4. tuuze rasilimali + mashirika yetu (yes mengine yalistahili kuuzwa lakini sio yote)
5. Kuruhusu upuuzi wa mikataba ya Madini unaoendelea hadi sasa
6. Mikataba ya ajabu ajabu............youname it

and on and on

Running a country is not a one man show or a show of few selected.............One need to have an idea and appreciate it (borrowing ideas its not a bad thing), sell the idea and then put it into practice.......for the benefit of all

hata mawazo ya kibepari nayo tumekopa pia........ona sasa tunavyopelekeshana na UFISADI......kila leo ukigeuka kila kona ni UFISADI!!

The point is one has to appreciate the sera/idea prior to its implementation phase.

Na huu UTITIRI wa shule binafsi mnaoupigania hapa na usio na udhibiti sijui mnataka kutujengea Taifa la aina gani............one need to come out and substantiate his/her arguments kuhusu benefits ya huu UTITIRI wa shule binafsi against what we had before (ambazo mpaka leo ndio zinazofanya vizuri kielimu)...............hata hivyo mbona shule binafsi zilikuwepo

Ogah: unataka kuniambia kwamba state controlled economy is the solution?
UFISADI: Naomba kukubishia: ufisadi na ubepari are not correlated, kwani unataka kuniambia Jittu Patel alijenga lini nyumba yake Masaki? Unafikiri enzi za Nyerere, Mkono hakuwa tajiri? You know the difference, they didn't flaunt their wealth! Unafikiri huko North Korea (the last stance of communism) hakuna mafisadi? WAPO! Mimi nadhani ufisadi ni matunda ya culture of ujamaa na unafiki tuliyorithi from enzi za Nyerere. CCM has ruled for more than 40 years without much challenge, wamejisahau. Pia wanaCCM wenyewe kwa wenyewe wanaogopana na hawaelezani ukweli. Na wananchi pia tunaonea haya viongozi wetu tunawaona kama miungu mtu kama Nyerere.

ELIMU: mfumo wa elimu wa Tanzania ni lazima uwe wa kujitegemea. Mimi sijaona kama Kenya kuna so much government subsidy in education au in some Asian countries like Phillippines, Thailand etc lakini utakuta family inasacrfice ili watoto waende shule. Na kuhusu ada za shule binafsi in Bongo, it is demand and supply. Kama wazazi wako tayari kulipa ada kubwa sana it is their right to do so.Kama huwezi kumudu there's always the second best or third best option. Sasa angalia matokeo ya UPE na MMEM watoto wanaenda shule lakini they come out semiliterate. Baadhi yetu labda tulifaidi matunda ya UPE but it could last only a few years kabla ya system kulemewa na quality kudeteriorate.

Enzi za kulelewa na serikali is over and for the best, kwani serikali ikianza kukuingilia maisha itataka kukuingilia all the way, then forget privacy, freedom of expression, freedom of movement etc. Au umesahau enzi hizo za ujamaa tulivyonyimwa haki zetu?
 
atleast the hoja at hand shows the contrast iliyokuwepo kati ya waliosema hayo maneno na JKN in real life....... wewe kama huujui wasifu wa JKN just google....na usiwe mvivu kusoma

jenga hoja iliyo na nguvu na sio kuita majina hoja za wenzio......call it whatever........to me it simply suggest the shallowness of ones mind...........
 
Sorry Ogah, hivi umenijibu mimi au? BTW I do not need to google JKN, I grew up on JKN and his works! There was no choice but to read all his books and essays na kuandika sifa zake. Na kama ulikuwa unajibu hoja ya mtu mwingine, si vibaya ukatafakari kwamba perception ya kila mtu ni tofauti. Sidhani kwamba tatizo ni watu kutojua kazi za Nyerere, ni jinsi wanavyopokea maneno yake na walivyoexperience maisha under Nyerere.
 
Pamoja na mengi mazuri ya Mwalimu lazima nikubaliane na Field Marshall Es alipoandika haya:-
Yes yanayotukuta sasa, mengi ni uzembe wetu wenyewe kibin-adam, as a nation, lakini kisiasa ni lazima kuwe na someone to point a fingure at..

Hapa mkuu nipo nawe mia kwa mia..samahani kwa kuwarudisha nyuma.

Nyerere Kisiasa alitumaliza kabisaaaaaaaaa na ndio maana tumeshindwa kufanya mageuzi ya Kiuchumi kwani hadi leo siasa zetu ndizo zinaongoza hali ya uchumi...
Pamoja na mazuri yote ya Azimio la Arusha chini ya chama kimoja hapakuwepo na haja ya kutokea tena Azimio la Zanzibar wala kuendelea kulienzi Azimio hilo ambalo limejengwa na baadhi ya watu wachache toka chama kimoja...

Mkandara:

Tanzania ni nchi kubwa. Vipenzi wa Nyerere ningependa mfanye kitu vifuatavyo:

Kaanzisheni makazi yetu. Na huko kwenye makazi yenu ishini kijamaa. Mfanye kazi za kujitolea. Mtoe matibabu bure na mfanye utopia wa aina yoyote mnayoweza.

Mkifanikiwa mtatuonyesha juhudi zenu kwa vitendo na mtapata wafuasi.

Haya mambo ya kutuhimiza kutukuza fikra ambazo nyinyi wenyewe hamjawahi kuzifuata ni PURE CRAP.

Na kama unatoa mifano ya dini basi kitu kimoja ni hiki, sijaona asiyeamini Mungu anahimiza wenzake kuwa wakristo au waIslam. Ni mwislamu atakayehimiza watu waingie kwenye dini hiyo. Na ni mkristo atayehimiza watu kufuata dini ya Kristo.

Haya mambo ya kuwa Nyerere alifanya makosa ya kibinadamu ni uzushi, mzee mzima alichemsha.
 
Susu,

Nakubaliana nawe ktk contradiction katika baadhi ya fikra za Mwl JKN na utekelezaje wake. Na ndio maana katika hoja yangu ya mwanzo nimesema......inabidi kuuelimisha umma na ideas zikubalike ndio utapata mafanikio ktk utekelezaji.

Matajiri mbona walikuwepo, wala sikatai hilo, walikuwepo kuanzia Uchagani kwa akina Mangi mpaka usukumani kwa akina Rupia......na nilipinga sana suala la kutaifisha miradi mikubwa ya hawa jamaa.....lile likuwa kosa na hata matokeo yake tumeyaona hatukufika navyo mbali.

Kuhus elimu ndugu yangu Susu, sisemi kusiwepo na private schools.....hizo shule ziwepo......japokuwa zinatakiwa ziwe under Control na hasa kwenye quality.......shule nyingi zimefunguliwa kama uyoga bongo........ukichunguza kwa makini quality yake ni duni.................kwani hata mimi niliingia ktk mkumbo wa kupeleka mwanangu ktk hizo "Academy".......i learnt a lesson...na sirudii tena
 
Sorry Ogah, hivi umenijibu mimi au? BTW I do not need to google JKN, I grew up on JKN and his works! There was no choice but to read all his books and essays na kuandika sifa zake. Na kama ulikuwa unajibu hoja ya mtu mwingine, si vibaya ukatafakari kwamba perception ya kila mtu ni tofauti. Sidhani kwamba tatizo ni watu kutojua kazi za Nyerere, ni jinsi wanavyopokea maneno yake na walivyoexperience maisha under Nyerere.

oopps sorry Susu.......sikuwa nakujibu wewe.....................nashukuru kwa ushauri pia
 
Ogah: unataka kuniambia kwamba state controlled economy is the solution?
UFISADI: Naomba kukubishia: ufisadi na ubepari are not correlated, kwani unataka kuniambia Jittu Patel alijenga lini nyumba yake Masaki? Unafikiri enzi za Nyerere, Mkono hakuwa tajiri? You know the difference, they didn't flaunt their wealth! Unafikiri huko North Korea (the last stance of communism) hakuna mafisadi? WAPO! Mimi nadhani ufisadi ni matunda ya culture of ujamaa na unafiki tuliyorithi from enzi za Nyerere. CCM has ruled for more than 40 years without much challenge, wamejisahau. Pia wanaCCM wenyewe kwa wenyewe wanaogopana na hawaelezani ukweli. Na wananchi pia tunaonea haya viongozi wetu tunawaona kama miungu mtu kama Nyerere.

ELIMU: mfumo wa elimu wa Tanzania ni lazima uwe wa kujitegemea. Mimi sijaona kama Kenya kuna so much government subsidy in education au in some Asian countries like Phillippines, Thailand etc lakini utakuta family inasacrfice ili watoto waende shule. Na kuhusu ada za shule binafsi in Bongo, it is demand and supply. Kama wazazi wako tayari kulipa ada kubwa sana it is their right to do so.Kama huwezi kumudu there's always the second best or third best option. Sasa angalia matokeo ya UPE na MMEM watoto wanaenda shule lakini they come out semiliterate. Baadhi yetu labda tulifaidi matunda ya UPE but it could last only a few years kabla ya system kulemewa na quality kudeteriorate.

Enzi za kulelewa na serikali is over and for the best, kwani serikali ikianza kukuingilia maisha itataka kukuingilia all the way, then forget privacy, freedom of expression, freedom of movement etc. Au umesahau enzi hizo za ujamaa tulivyonyimwa haki zetu?

Unajua wakati ujamaa unapamba moto intellectualls wengi wa political science au development studies walikuwa ni watu wa mkondo wa kushoto. Hata vyuo vikuu vya Marekani vilijazana watu wanaohubiri Ujamaa.

Uki-google na kuangalia nani aliyeandika au kumsifu Nyerere, utaona walewale watu wa mkondo wa kushoto na wenye maneno mengi lakini hakuna walichofanya. Na wengine hapa wanaona sifa kwa sababu alikuwa anasifiwa na wazungu.

Watanzania tuliona ukiritimba kwa macho na hatuna sababu ya ku-google. Hakuna mzungu au mtu wa nje atakayeeleza vizuri zaidi sisi.
 
ELIMU: mfumo wa elimu wa Tanzania ni lazima uwe wa kujitegemea. Mimi sijaona kama Kenya kuna so much government subsidy in education au in some Asian countries like Phillippines, Thailand etc lakini utakuta family inasacrfice ili watoto waende shule. Na kuhusu ada za shule binafsi in Bongo, it is demand and supply. Kama wazazi wako tayari kulipa ada kubwa sana it is their right to do so.Kama huwezi kumudu there's always the second best or third best option. Sasa angalia matokeo ya UPE na MMEM watoto wanaenda shule lakini they come out semiliterate. Baadhi yetu labda tulifaidi matunda ya UPE but it could last only a few years kabla ya system kulemewa na quality kudeteriorate.

Enzi za kulelewa na serikali is over and for the best, kwani serikali ikianza kukuingilia maisha itataka kukuingilia all the way, then forget privacy, freedom of expression, freedom of movement etc. Au umesahau enzi hizo za ujamaa tulivyonyimwa haki zetu?

Kamanda kapate facts zako straight uone kuwa Kenya sasa hivi wanatoa elimu bure ya primary na secondary kwa subsidy kibao.

Ubepari umewashinda na wanarudi kwenye ujamaa wa Nyerere. Kitu hiki ni the same kwa Marekani ambayo inatoa elimu ya msingi na ya upili bure (msingi wa ujamaa) na kuwa na program nyingi tu za UPE

Pata facts kabla ya kuchangia!
 
Mkandara:

Tanzania ni nchi kubwa. Vipenzi wa Nyerere ningependa mfanye kitu vifuatavyo:

Kaanzisheni makazi yetu. Na huko kwenye makazi yenu ishini kijamaa. Mfanye kazi za kujitolea. Mtoe matibabu bure na mfanye utopia wa aina yoyote mnayoweza.

Mkifanikiwa mtatuonyesha juhudi zenu kwa vitendo na mtapata wafuasi.

Baadhi yetu tayari tunaishi kwenye nchi ambazo tayari zinafanya haya yote:

Afya bure kwa masikini - Scandinavia na Canada
Elimu bure kwa wote - Marekani na ulaya
Huduma za afya kwa wazee na wastaafu bure - Marekani

Huduma kubwa sana ya kusaidia wastaafu (social security program) kwa nchi zote zilizoendelea.

Haya mambo ya kutuhimiza kutukuza fikra ambazo nyinyi wenyewe hamjawahi kuzifuata ni PURE CRAP.

Na kama unatoa mifano ya dini basi kitu kimoja ni hiki, sijaona asiyeamini Mungu anahimiza wenzake kuwa wakristo au waIslam. Ni mwislamu atakayehimiza watu waingie kwenye dini hiyo. Na ni mkristo atayehimiza watu kufuata dini ya Kristo.

Haya mambo ya kuwa Nyerere alifanya makosa ya kibinadamu ni uzushi, mzee mzima alichemsha.

Kama umesahau, ujamaa umeshinda na mabepari karibu wote wanakopa zile program za kijamaa kwa maigizo na majina makubwa ya kibepari.

Ujamaa ==== Socialism ==== social services including social security administration!

Just to begin with!
 
Wakati hii thread inaendelea,

Naomba wanaopondea ujamaa na kusifia ubepari wanitajia nchi hata moja ambayo ni ya kibepari hapa duniani Kisha mimi nitataja nchi zaidi ya mia moja ambazo ni za kijamaa au zinaongozwa kwa sera za kijamaa (wanaziita za mrengo wa kushoto) ikiwemo majimbo 20 au zaidi ya marekani.
 
mwafrika nashukuru kwa hili lakini ndugu zetu hapa tutajarribu kwenda nao pole pole na natumaini wakifungua macho watashangaa ni jinsi gani dunia ni ya kijamaa zaidi kuliko ya kibepari. Lakini kwa wakati huu naendelea kwenye fikra za Mwalimu.

Kwa anayetaka kuchangia kuhusu legacy ya Mwl na kadhalika kuna zile mada nyingine na kuna mada ya Ibara ya 15 nadhani tuendelee kule kuzungumzia lolote lakini hapa naomba niwe Dikteta mkarimu, tuangalia hoja baada ya hoja juu ya fikra za Mwalimu; tufanye hivyo kwa kuangalia substance ya mawazo na fikra hizo na si kingine.
 
Kwanza, niwashukuru wachangiaji wote kwa mjadala wa kiungwana na kidugu kuliko nilivyotarajia. Lakini naomba nitoe maombi yafuatayo kwani sioni sababu ya kupoteza mwelekeo hivyo nalazimika kudirect tulikoanzia kwa sababu najua kuna jaribu la kutoka nje ya mjadala au kwende mbele ya mjadala. Naomba twende kwa hatua ili tusipotezane njiani.

a. Ninapozungumzia "fikra" sizungumzii mawazo (random thoughts) au vitendo (actions) vya Mwalimu na sizungumzii maamuzi ya chama au utendaji wa serikali. Nazungumzia "ideas" yaani mfumo wa mawazo yenye muelekeo uliopangwa na wenye kuongozwa na kanuni zilizowazi.

b. Kama nilivyosema awali, najaribu kuconcentrate kwa jambo moja baada ya jingine na ningependa kufanya hivyo thematically, yaani kwa kuangalia eneo moja jinsi mwalimu alivyoliona na kuliarticulate. Sasa mniwe radhi kama nitakuwa nawarudisha katika kile alichosema Mwalimu na kuangalia substance yake na siyo kuinfer au kujaribu kuongeza maana ya zaidili kilichosemwa.

c. Najua watu wana passion na myriad of thoughts on Mwalimu. Naomba nieleweke mada inasema "Fikra za Mwalimu; hizi hapa mzikubali au mzipinge". Siyo kusudio langu kumpima Nyerere na kiongozi mwingine, siyo kusudio langu kuangalia utawala wa Nyerere ulikuwaje, au alifanikiwa vipi kwenye hili au lile. Kusudio langu is very simple look at the ideas of Mwalimu as articulated in so many places and then and only then decide on the validity and the plausibility of their substance. Period.

Nina maana ya hivi Mwalimu akisema "kila mwanadamu ana haki ya kutammbuliwa na kuthaminiwa utu wake" tunachoangalia ni je alikuwa sawa kutoa kauli ya namna hiyo na hivyo kuwasilisha msimamo wake kifikra juu ya haki za wanadamu. Kama hatukubaliani basi hatukubaliani substantially.

Hilo ndilo ninajaribu kufanya. Ni sawa nikimuomba mtu aangalie maandishi ya Plato on Socrates au ya Aristotle. Itakuwa ni ajabu kuanza kupima jinsi gani Socrates alifeli kwa kunywa sumu au jinsi gani Plato hakuweza kuwa mfalme licha ya mawazo yake mazuri. Na itakuwa makosa kusema Plato alifeli kwa sababu mwanafunzi wake Alexander Mkuu alikufa akiwa kijana na ufalme wake kutawanyika! No, tunaangalia kama ni "the Republic", "Laws" or "Statesman". Tuangalie substance ya alichosema Mwalimu na tuamue if it is valid, agreeable or total rubbish.

So naomba nianze kutoa majibu ya waheshimiwa wajumbe ambao nitaweza kuwajibu usiku huu, wengine nitajaribu kesho.

Yes, mawazo ya Mwalimu yana nafasi kubwa sana, lakini a change of what na under what conditions au under who's expense?

Ahsante Mkuu.

Kabla ya kwenda kwenye detail ya jambo lolote one has to articulate clearly the basis of that undertaking. Ndio maana, kabla ya Wamarekani hawajapigania uhuru wao waliweka azimio la wao kutaka kuwa huru na kabla jamhuri haijaanza waliandika Katiba yao (as imperfect as it was).

Sasa kabla hatujaenda jinsi gani viongozi wangefanya, la kwanza tuangalie kanuni ambazo zingewaongoza. Hivyo, Tunachokiona hapo siyo details za jinsi gani Mwalimu angeamua kuongoza Tanzani lakini principle ya change which was threefold in nature.

a. Africa must change
b. The change has to be positive
c. Africans have to initiate and steer that change.

Hizo ni kanuni ambazo zinaongoza mabadiliko hayo. Details zake ndiyo kama tutakavyokuja kuziona mbele katika fikra nyingine za Mwalimu.

Hivyo, nilichouliza hapo mwanzo si kingine bali kwanza tuangalie ubaya wa principle hiyo as articulated by Mwalimu ni nini?

Mkuu Kada,

Heshima mbele,

1. Heshima kwa Mwalimu hilo halina ubishi, I have a great respect kwake na all the good things he did kwa taifa letu, ninaaamini kuwa amefanya mengi sana mazuri kwa taifa letu, lakini pia kuna mapungufu, ambayo ndio hasa chanzo cha kudumaa kwetu kisiasa, kiuchumi, na hasa cha muhimu kuliko yote kisheria.

si kweli, alichokabidhiwa Mwalimu ile Disemba tisa kilikuwa ni jamii ya watu wenye nia mbalimbali, maslahi mbalimbali, makabila mbalimbali n.k Na kutoka kwa hawa ilitakiwa ajenge Taifa. Katika kufanya hivyo kuna maamuzi ambayo ilimpasa kuchukua kuna maamuzi ambayo ilimpasa kufanya.

Ukiangalia katika hii hoja yake ya msingi ameuliza maswali muhimu, anasema katika kubadilika huko tutafanya nini kama kuna kanuni zinazogongana? mahitaji ya mtu binafsi na ya jamii yakigongana tuchaguaje?
2. Change is always a good thing, lakini tatizo ni what change?

Mzee soma tena alichosema Nyerere kuhusu change, hakuwa anazungumzia hewani. Amezungumzia change kama kitu ambacho ni cha lazima kwa bara la Afrika na ni lazima iwe positive change. Hakuzungumzia change kutoka hewani.
Mkapa alipotoa hotuba yake ya kwanza baada ya kuapishwa kuwa rais, hivi unajua maneno aliyoyasema mkuu kuhusu change? Unakumbuka maneno ya Muungwana baada ya kuapishwa kuhusu change? Change iko wapi? Ni bin-adama gani unayemjua anayeweza kukubali change bila bakora nyuma?

mzee sitakwenda huko, nabakia kwenye aliyoyasema Nyerere.

3. Kinachoniudhi ni idea ya NEC Butiama, ya kusema kuwa sasa wamegundua kuwa wanahitaji kurudi kwenye maaandishi ya Mwalimu, na kwamba sasa watayachapisha na kuyasambaza, eti this way itasaidia something I do not even know ni nini, man! ninasema hivi Mwalimu, had his time, ametawala miaka 23, na hata akiwa nje ya urais bado ameeendelea kutawala, tizama tulipo, we had a chance kufanya mabadiliko, lakini tizama tunavyozidi kuzama, fisadi aliyethibitishwa na kamati ya kisheria ya bunge, eti ajiuzulu tu, that is it? hiyo ndio change?

Again, I won't go there.
I am a CCM, member lakini kwenye hili siko down kabisaa, maneno yanatakiwa yafanywe na vitendo, Mwalimu did what he could, sasa viongozi tulio nao sasa wanaposema kuwa turudi kwenye maneno ya Mwalimu, ina maana wameshindwa hawana mapya, basi watoke na kuwaachia wengine, lakini tusiendelee kudanganyana, tufike mahali tuambiane ukweli enough is enough!

very valid argument but haihusiani kabisa na alichosema Nyerere on substance.

Hapa tunajaribu kuelimishana kwa kutumia hoja, binafsi I am learning a lot, na ninategmea kujifunza more kuhusu maandishi ya Mwalimu, mimi nimeishi part of utawala wa Mwalimu, sasa ninasubiri kuona mazuri ambayo sikuyaona kwenye utawala wake, lakini yapo kwenye maneno yake na maandishi yake!

siyo jaribio langu kuonesha mazuri ya utawala wa Mwalimu. Substance ya fikra zake as articulated in various works.

Uzuri wa fikra za kiongozi unaonekana kwenye matendo yanayotokana na fikra hizo. Fikra za kiuongozi haziwezi kuwa nzuri "in abstract".

si kweli. fikra nzuri ziko huru na vitendo vya mtu au watu wengine. Mtu akisema "ukijumlisha mbili na mbili unapata nne" siyo tu anatoa wazo lakini ana articulate ukweli fulani. Lakini mtu huyo huyo akiamua kwenda pembeni na kumdanganya mtu kuwa mbili na mbili ni sita, kitendo chake hicho ni kiovu lakini ukweli alioutoa unasimama wenyewe.

Hivyo basi, fikra (ideas) hazitegemei kama anayesema amefanya nini au vipi kwani ukweli ni ukweli hata ukisemwa na kichaa. Hivyo ninachojaribu kuangalia ni substance ya fikra za Mwalimu siangalii kitu kingine chochote.

Anayetaka kuzungumzia Udikteta wa Mwalimu ipo thread, anayetaka kuzungumzia jinsi mwalimu alivyofeli kiuongozi nadhani ipo thread n.k siyo kusudio langu kufanya haya mengine.

So, valid ideas are true not only in abstract but very so abstractly. Hazitemei kitu kingine chochote kama vile nani alisema, lini ilisemwa au katika mazingira gani ilisemwa.

Mwalimu aliongea kwa falsafa kubwa sana bila kuigeuza kuwa vitendo.

mzee mwenzangu nadhani uko karibu sana na ninakoelekea. Kuna fikra ambazo inachukua muda kupata mtekelezaji na kuna fikra ambazo hata mtu mwenyewe aliyezitoa anashindwa kuzitekeleza. Lakini huu ni ukweli wa wanafalsafa wengi siyo wafalme. Aristotle , Plato, Thomas Aquinas na wengine wametoa mchango mkubwa sana katika uelewa wetu wa maadili, utawala na uchumi, lakini mawazo yao yalibakia vitabuni hadi pale walipopatikana watu walioamua kuyafanyia kazi kweli.

So, hilo la Mwalimu kushindwa kutimiza kila aina ya fikra zake kwa vitendo lawezekana kuwa ni mapungufu ya kibinadamu lakini haiondoi ukweli wa fikra zake.

Kuhusu mawazo yake kuhusu need of change in Afrika Mwl. alikuwa sawa? Kama kuna makosa katika alichosema ni yapi?

[COLOR="Blue
[SIZE="3"]Tafadhali Mwalimu! Wakati Nyerere anahubiri ujamaa na kujitegemea mchana, usiku alikuwa anaenda kuomba misaada Ulaya na China. Kwa hiyo, siyo tu fikra zake zilikuwa njozi, pia maneno yake hayakuendana na matendo. Mtu huyo mnamwitaje? Nikimwita anavyotakiwa nitachomwa moto kwa kumtukana Baba wa Taifa[/SIZE].

Again, naangalia fikra katika substance yake. Mawazo hutangulia vitendo, lakini fikra hutangulia vitendo vikuu. Sasa, tuangalie hizo fikra tuone ubaya wake kwamba tuzitupe. Sasa kama Nyerere alikosea au mtu hampendi kwa sababu hakufanya hivi au vile je kunafuta ukweli wa fikra zake? Jibu la kwangu ni no.. kwa sababu fikra ni independe of time, person n.k

Je alichokisema kuhusu need ya Afrika kubadilika na katika mabadiliko ya namna gani kilikuwa na makosa gani?

Mkuu mimi sina dataz zozote, lakini I have lived Mwalimu's policies, nimezisoma primary, secondary, JKT, sasa tatizo likawa what is next? Hakuna! U-China, nimefika na nimekaa sana Shangai, karibu miezi mitatu baada ya meli yangu kuharibika pale...

Sitaenda huko kwa mambo ya china, tuangalie susbstance ya fikra za Mwalimu kuhusu change. Kwa hiyo wewe umekataa kuwa si sahihi.

nimekusikia mzee ila sitaenda huko. Kuna wakati tutafika na kuangalia fikra zake kuhusu mambo ya Azimio la Arusha na tutaona makosa yalikuwa wapi. Lakini kuhusu haja ya Afrika kubadilika kama nilivyoiweka Uk. 3 unakubaliana na substance yake au na wewe unapinga? na kwanini?

Mwanakijiji kabla sijachangia nauliza jee mambo yaliyofanyika wakati wa uongozi wake na kuyabariki tuyaingize katika fikra na mawazo yake?

Hapana, nazungumzia articulations ya principle na mawazo yake na ninaangalia substance ya kile alichokisema. Nje ya hapo tutashindwa kufocus kama ilivyoendelea hadi sasa.

Tafadhali Mwalimu!

yawezekana una sababu ya kusema hayo yote na ningeweza kujibu moja baada ya nyingine, lakini itanitoa kwenye mada at hand. So, unafikiri vipi kuhusu suala la change katika Afrika, maana hii ndiyo theme ya kwanza tunayoiangalia kwa sasa. Je maneno ya Mwalimu yakiwakilisha fikra zake yana makosa gani na substance yake ina makosa gani?

Hongera Mzee Mwkjj kwa kuleta hoja nzuri hapa!

Jamani hebu angalieni contradiction in this essay,

Finally tunaangalia substance ya hoja yenyewe.

hivi Nyerere hakujua ya kuwa forceful dislocation of people will lead to dicontentment?

Samahani Susuviri nadhani umemiss alichomaanisha Nyerere hakuwa anazungumzia sera ya Ujamaa vijijini (hiyo ilikuja miaka ya sabini) lakini alikuwa anazungumzia in generality kuhusu mabadiliko yoyote yale kama ya kujenga Taifa yangeweza kusababisha watu kuhama au kubadili mambo fulani ambayo yangewaletea usumbufu, he was not talking about ujamaa vijijini.

. No, the change that Nyerere speaks about has no place or role in current Tanzania. Hatuwezi kurudi kwenye Azimio la Arusha.

Tutafika na kuangalia hoja za Mwalimu kuhusu Azimio la Arusha na tutaona kama substance yake ilikuwa mbaya. Lakini kwenye substance nzima ya hoja yake ya change usichokubaliana nacho ni hicho cha "dislocation" kama nilivyoielezea au hukubaliani na wazo zima la the necessity of positive change in Africa as articulated in that piece?

Haya mambo ya kuwa Nyerere alifanya makosa ya kibinadamu ni uzushi, mzee mzima alichemsha.

well, endelea basi na mambo mengine. Hilo la kuchemsha limeshaoneshwa na wengine. Sasa angalia alichosema na uamue maneno yake yenyewe yana ukweli kiasi gani au kwa vile yamesemwa na Mwalimu basi hata kuyaangalia unaogopa?

Chuki ni kitu kibaya kwani kina tabia ya kupofusha watu kiasi kwamba ukimchukia mtu hata uzuri wake huwezi kuona na hata kumsikia hutaki hata kama anakuambia ukweli.
 
Baadhi yetu tayari tunaishi kwenye nchi ambazo tayari zinafanya haya yote:

Afya bure kwa masikini - Scandinavia na Canada
Elimu bure kwa wote - Marekani na ulaya
Huduma za afya kwa wazee na wastaafu bure - Marekani

Huduma kubwa sana ya kusaidia wastaafu (social security program) kwa nchi zote zilizoendelea.

Kama umesahau, ujamaa umeshinda na mabepari karibu wote wanakopa zile program za kijamaa kwa maigizo na majina makubwa ya kibepari.

Ujamaa ==== Socialism ==== social services including social security administration!

Just to begin with!

Duh wewe ndugu uanaishi marekani gani inayotoa elimu bure ?Hakuna kitu cha namna hiyo labda kwa wateule vinginevyo elimu na huduma ya afya marekani ni gharama kubwa ,afya mpaka uwe na insurance ndipo unasikilizia unafuu napo deductable inapanda kila siku.Elimu wanachofanaya cha maana ni mikopo ila gharama ni kubwa ,kama New York Un. inafika $45,000 per yr.Na hiyo ngoma lazima urudishe haina janja.
Afya kwa wastaafu wanatumia sehemu ya pesa zao walizokuwa wanalipa kodi kwenye social ambazo zimewekwa kwenye mfuko wa Madicare kwa wazee above 65 and disiabled.

Ila Tukirudi kwenye maada inayo muhusu mwl. inasikitisha mtu anamlaumu kwa kumuimba Kambona kwenye nyimbo za mchakamchaka na mambo kama hayo please jamani kama unaongelea ubaya wa mtu kuhusu nchi sema in such a way that mtu ikisikia kweli aone kweli hili ilikuwa na madhara kwa nchi.Don't make it personal.
Mimi kwa maoni yangu majumuisho ya wasifu wa kiongozi ni kupima mabaya na mazuri aliyoyatenda yatakayo zidi mengine ndio sifa ya kiongozi huyo.
Na naweza kusema hakika Mwl. alikuwa kiongozi bora.Ukiniuliza accomplishment zake nitakutajia.
 
Nakuunga mkono kabisa Mwalimu JK alikuwa Kiongozi Bora, na kwa kuongezea alikuwa Shupavu na Mwenye Malengo / Maono ya muda mrefu. Zaidi ya asilimia 50 % ya Civil service na viongozi wa kisiasa, jeshi nk walioko maofisini hapa nchini wamesoma na kugharamiwa kupitia sera za Elimu Bure zilizoanzishwa na Mwalimu JK. Namalizia kwa kusema, Mwalimu nyerere ni moja ya viongozi bora katika Afrika, yuko kundi la akina Mandella, Lumumba, Nasser nk. Twakusubiri Mwanakijiji na wengineo munaotaka kutuwekea maandiko ya Mwlimu JK humu ndani ya uwanja wa majadiliano (JF), tafadhali mutuwekee, nami nikipata nitaweka. Siku njema
 
Mwafrika, do not confuse between social welfare programs and socialism. Socialism does not allow private ownership of means of production. Under Mwalimu, we kept singing that "the commanding heights of the economy" should be publicly owned. As it turned out, the "commanding heights" of our economy included things like schools, hospitals and small hotels. Mwalimu nationalized these.

Mwalimu alikataza hata mabasi ya watu binafsi. Ilifika wakati ikawa shida kweli kweli kusafiri toka mji hadi mji. Nikiwa mwanafunzi UDSM nilibidika kutegemea KAMATA peke yake ili kwenda Moshi. Ilikuwa wakati mwingine inalala njiani.

Mwalimu alisema "hageuki kuwa jiwe". He could persevere for he really never had to shoulder the pain. Alianzisha "duka la viongozi", akawa anaponea huko yeye na "wezake".
 
Back
Top Bottom