OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,819
- 117,362
Kiungo wa kimataifa wa Tanzania Feisali Salum Abdallah “Feitoto” amewasilisha juzi maombi yake kwenye ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF akitaka Kamati ya hadhi na haki za wachezaji na wanachama ipitie upya shauri lake na irekebishe hukumu yake na kumpa haki.
Feisali alivunja mkataba na Yanga SC tarehe 22/12/2022 kwa maandishi akitumia kipengele namba 14.7 cha mkataba baina yake na Yanga ambapo ilimpasa kuilipa klabu pesa ya usajili aliyopokea pamoja na mshahara wa miezi 3 tu.
Yanga SC walipinga jambo hilo na kulalamika TFF ambako lilipelekwa kwenye Kamati husika na shauri kusikilizwa hadi hukumu kutoka ambako Kamati ilimuamuru Feisali kubaki Yanga.
Mchezaji anaona Kamati haikufanya sawasawa na haikujielekeza kwenye hoja (issues) ambazo zililetwa mezani kwa pande zote mbili badala yake ilisema yeye anapaswa kurudi Yanga kitu haukuwa hoja.
Zaidi upande wa mchezaji wanaamini pia kwamba Kamati haikuwa sahihi kusema Feisali ni mchezaji wa Yanga kwa mujibu wa mkataba ambao Fei ameuvunja na Yanga pia wanajua amevunja ila wao kama partners hawakushirikishwa na ndiyo hoja yao ilipo.
Walitegemea kamati ijielekeze kama namna alivyovunja mkataba Fei ilikuwa sahihi au sio sahihi.
Kama sahihi mkataba uvunjike na kama sio sahihi mchezaji aadhibiwe na sio kumlazimisha kurudi sehemu alikoshindwa kufanya kazi kwa sababu ambazo alizisema wazi mbele yao alipohojiwa.
Wanasisitiza mchezaji sio mtumwa wa kulazimishwa kufanyakazi mahala ambapo anaona mazingira yake magumu na sio rafiki tena.
Upande wa mchezaji wanalaumu kamati kushindwa kutoa adhabu kwenye hukumu yake kitu ambacho wanakiona pia sio cha kawaida kwa mtu aliyekosea, badala ya kumpa adhabu unamlazimisha kurudi alikoshindwa kuishi.
Wanahoji au kamati inaamini kumrudisha Yanga ni kumuadhibu pia?
Wana imani Kamati ina watu weledi, wajuzi wa mambo na wabobezi ambao wanazijua sheria, kanuni, taratibu zinazitumika na FIFA Dispute resolution chamber pamoja na CAS
My Take
Hivi huyu Feitoto ameondoka na figo ya Utopolo? Acheni roho ya kimasikini