Fedha za Rambirambi Lucky Vincent kutumika kukarabati hospitali ya Mount Meru

Sitaki kuamini kama hii habari ni kweli na kama ni kweli, basi hii serikali itakuwa na laana!!!

Ikiwa waliweza kutumia michango ya tetemeko la Kagera kufanyia kile ambacho hakikusudiwa!!

Halafu tena watumie rambirambi kufanyia jambo tofauti na matumizi ya rambirambi!!

Hivi tutalaumiwa tukisema hii serikali hivi sasa itakuwa inaombea wananchi wapate majanga ili hatimae michango ikipatikana watumie michango hiyo kufanyia kazi ambayo ni serikali ndio wenye wajibu nayo?!
 
Hivi kweli Serikali ya Awamu hii tumepewa kama Adhabu kwetu?
Yaani misiba na majanga ya kitaifa imekuwa kama Chanzo cha Mapato!!!
Mkiwa majukwaani, utasikia;mtuombee kwa Mungu, Hivi mnajua kama Mungu anawaona mnayotenda????

Siku zote ombeni Mungu asimame kama BABA katika maisha yenu, lakini atakaposimama kama Mungu maishani mwenu na haya matendo yenu, ghadhabu yake mtaisoma.
 
Niliwahi kwenda kijiji kimoja nikakuta wakazi wanaomba kwa dhati eti utokee msiba kwa tajiri na hasa anayeishi mikoani. Maana wakifiwa hao ndipo wakazi wanakunya walau bia, nyama za uhakika (anachinjwa ng'ombe) na kula pilau. Niliyaona kama masihara lakini sasa naanza kuamini kuwa hata watu wa mijini kama wapambaji, wauza majeneza, wakodisha macoster nk wanaombea 'mabaya' kutokea ili nao wanufaike.
Japo sikutegemea kabisa kuwa na taasisi nazo zimo kwenye kikapu hicho!!!
 
Iwapo kura yangu ingeenda ccm ningejilaumu maisha yangu yote. Hii serikali imeshidwa kuongoza nchi,imeshindwa kubuni vyanzo vya kueleweka vya mapato zaidi ya kamata kamata ya traffic na pesa za majanga ndo wanazisubiria. Hali imekua mbaya sana hadi pesa za maafa wanazipiga hii ni zaidi ya richmond na escrow aisee. Sasa tukiwaita wao ndo wapiga dili tutatua tunakosea kweli?.
 
Hongera Gambo kwa kutuonyesha sura halisi ya chama chako na Bosi wako.Hongera sana.Nadhani mnaomba majanga yaendelee kutokea ili muweze kutekeleza ilani yenu ya CCM,kupitia pesa ya rambi rambi.Kagera na sasa Arusha.Nendeni na Zanzibar nako kuna pesa imechangwa fanyeni haraka kabla hazijafika kwa walengwa.
 
Popote duniani pesa ya rambi rambi ni kwaajili ya wafiwa tu, swala la kusema kuwa kiasi cha fedha cha rambi rambi kinapelekwa kwa ajili ya majeruhi si sahihi, marafiki walio marekani walisema kuwa wamejitolea gharama zote na kuwahifadhi wasindikizaji na kuwahudumia wakati wote wakiwa huko marekani.

Serikali ingeonyesha mchango wake katika swala la kuwahudumia wazizi waliosindikiza watoto kwenda kwenye matibabu na hao madaktari wangetakiwa wapewe posho kutoka serikalini kutokana na utaratibu wa posho wa kiserekali.
 
JINAMIZI la matumizi ya fedha za rambirambi kwenda kwa familia za wanafunzi limegeuka kaa la moto kwa kuamuliwa sehemu ya fedha hizo zipelekwe kukarabati Hospitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru.

Fedha hizo ni zinazotakiwa kuwasilishwa kwa familia za wanafunzi 33, walimu na dereva wa basi la Shule ya Lucky Vincent, waliofariki katika ajali iliyotokea wiki chache zilizopita.

Habari zinasema, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo anadaiwa kuwaita wazazi wafiwa akiwataka wakubali Sh milioni 56 walizotakiwa kupewa, zielekezwe kufanya mambo mengine tofauti.

Gumba anadaiwa kutaka fedha hizo zielekezwe katika mambo matatu ambayo ni kuboresha wodi ya wagonjwa mahututi (ICU), kujenga kitengo cha magonjwa ya akili au kuboresha chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru.

Akizungumza mjini hapa jana baada ya Ibada maalumu ya kuombea majeruhi walioko Marekani na wazazi waliopoteza watoto wao kwenye ajali hiyo, mmoja wa wazazi ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema wameamua kujitoa kwenye kamati ya kupanga matumizi ya Sh milioni 56 zilizobaki ili kuipa serikali fursa ya kupanga yenyewe matumizi ya fedha hizo.


Mzazi huyo aliyeomba kutotajwa gazetini kwa sababu za usalama wake, alisema wameamua kujitoa kwenye kamati hiyo baada ya kutoona sababu na umuhimu wa kuwapo kwao.

“Mambo mengi sana yalishafanywa na kukamilika, sisi tuliitwa Mei 16, mwaka huu kwa mkuu wa mkoa na kusomewa taarifa ya fedha zilizotumika.

“Baada ya kikao hicho ikaundwa kamati ya kusimamia Sh milioni 56 zilizokuwa zitumike kwa ajili ya kumbukumbu ya watu 35 waliokufa.

"Nilichaguliwa kuwa mmoja wa wanakamati tukiwa wanaume wawili na wanawake Wawili, tuungane na kamati iliyopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa….wenzangu walikwenda kwenye kikao mimi sikwenda sikuwa na taarifa.

“Sh milioni 56 zilizobakia tuliambiwa tuangalie zifanye nini huku tayari mapendekezo yakiwa ni Hospitali ya Mount Meru kwamba zifanye maboresho chumba cha kuhifadhi maiti, chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) au kuweka kitengo cha magonjwa ya akili badala ya wagonjwa kupelekwa Hospitali ya Mawenzi au Mirembe Dodoma,” alisema mzazi huyo.

Mzazi huyo alidai kwamba Ijumaa iliyopita walikwenda Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa na kueleza nia yao ya kutoendelea kwenye kamati hiyo kama sehemu ya wazazi waliofiwa.

“Tumeona ni vema serikali iendelee na utaratibu wote kwa sababu kitendo pia cha wazazi wafiwa kuwekwa chini ya ulinzi na polisi kule shuleni Lucky Vincent kilitusukuma kuona hatuna sababu ya kuwa sehemu ya kamati,” alisema mzazi huyo na kuongeza:

“Tuliitwa baada ya mambo yote kukamilika, kwa ujumla hatukuridhishwa na fedha za rambirambi kubadilishiwa matumizi.

“Kubwa linalotusikitisha ni kuambiwa kwamba fedha hizo za rambirambi zimetokana na nguvu ya uchangishaji ya mkuu wa mkoa kwa hiyo wana haki ya kuzifanyia utaratibu wao wenyewe,” alisema.

Taarifa inayodaiwa kutolewa na Gambo iliyosambaa katika mitandao mbalimbali ya jamii jana, ilimnukuu mkuu huyo wa mkoa akisema ameona ni vema nguvu kubwa ikapelekwa kuwahudumia majeruhi watatu wanaopatiwa matibabu Marekani.

Kupitia taarifa hiyo, Gambo alisema hadi Mei 20 mwaka huu kutokana na wadau kuendelea kuchangia rambirambi, zimepatikana zaidi ya Sh milioni 67.9, hivyo fedha hizo zitatumika kuwahudumia majeruhi hao.

“Kutokana na wadau kuendelea kuchangia tumebakiwa na Sh milioni 67,993,885, kwa mantiki hiyo busara imeelekeza kuwa nguvu kubwa sasa ipelekwe kwenye kuwahudumia majeruhi maana hata tufanyeje wale ambao Mungu kwa mapenzi yake amewachukua hatuna namna tena ya kuwarudisha,” alisema na kuongeza.

"Jumatatu Mei 22 mwaka huu tutazitumia familia za majeruhi na madaktari wetu waliojitoa kuwasindikiza majeruhi Dola za Marekani 20,000 (Sh 44,720,000), kila familia itapata Dola 5,000, daktari Dola 2500 na muuguzi Dola 2500, kama sehemu ya kuendelea kuwafariji na kuwapunguzia changamoto huko ugenini".

Gambo alisema baada ya matumizi hayo zitabaki zaidi ya Sh milioni 22.2 huku hali za majeruhi zikiendelewa kuangaliwa na fedha zilizobaki zitaendelea kuwekewa utaratibu kupitia timu ya wafiwa wane walioteuliwa na wafiwa wenzao kushirikiana na serikali kuhakikisha mapato na matumizi ya suala hilo yanaeleweka kwa umma.

Alisema pia kuwa ofisi yake imehitimisha rasmi hatua ya kupokea rambirambi ili ipate muda zaidi wa kufuatilia mustakabali wa majeruhi walioko Marekani kwa

matibabu.

Akijibu hoja za fedha kuchepushwa na kupelekwa katika ujenzi wa hospitali, Gambo aliwashangaa watu wanaojadili hewa kwani hakuna fedha iliyopelekwa katika ujenzi.



“Mnajadili hewa badala ya taarifa sahihi. Hakuna hela iliyokwenda Mount Meru Hospitali. Mtu ukiwa mnafiki ukiwa kijana ukizeeka unakuwa mchawi,” alijibu Gambo katika moja la magropu ya mtandao wa kijamii wa WhatApp

MEYA
Katika ibada ya jana, mbali na wazazi na walezi waliopoteza watoto wao katika ajali hiyo, wengine weliokuwapo ni Meya. Calist Lazaro madiwani wa Halmashauri ya Jiji hilo na wengine kutoka Halmashauri ya Meru.

Akizungumzia hatua ya kamati hiyo kujitoa kabla ya kufanya shughuli iliyokusudiwa, Lazaro alisema kwa vile suala hilo lina ukakasi, wananchi wa Arusha na viongozi wengine ambao hawakushirikishwa katika mchakato huo, hawatashiriki jambo lolote kuhusu fedha za rambirambi zilizobaki kwa Gambo.

"Nashukuru Mungu amesaidia leo tumehitimisha ibada maalum ya kuwaombea watoto wetu wanaotibiwa Marekani ila kwa uamuzi huo wa wazazi wetu ambao wamechukizwa na vitendo ambavyo Mkuu wa Mkoa anaendelea kuvifanya, wa kuamua kujitoa kwenye kamati, tunawaunga mkono na hatutaingilia jambo hili ambalo lilikwisha kuharibiwa,” alisema.

CHANZO: Mtanzania
Very good ni moja wapo ya chanzo kizuri cha mapato ya serikali ya awamu hii. Heko RC Gambo!!!!!!
 
Ukisoma na kufuatilia mambo toka tukio hili lilipotokea, maswali ni mengi zaidi ya majibu.
ukipitia ile ripoti ya matumizi ya rambirambi iliyotolewa na mkuu wa mkoa unakata tamaa.
Akili yangu inanituma kuamini watanzania tuna amini miungu tofauti,
Binafsi naamini kupitia Mungu wa Eliya na Yakobo, Mungu wangu hadhihakiwi na akiamua kushusha adhabu hakika ni kiama.
Nahisi baadhi ya watanzania Mungu wao labda ni tofauti na Mungu wangu, kwa hii drama ya Arusha, tumuache Mungu aendelee kuitwa Mungu.
Naamini katika Biblia takatifu
Kumbukumbu la Torati 11:28
" na laana ni hapo msiposikiza maagizo ya Bwana,Mungu wenu, mkikengeuka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua".

Dumni katika Mungu alie hai.
 
Sasa likitokea janga kama inachangisha serikali badala ya wadau husika hatutoi.... Washatufunya sisi wajinga
 
Ndio muache kutoa rambi rambi kwenye majanga ambayo serikali inahusika. Pelekeni rambi rambi moja kwa moja kwa muhusika.
.
.
Sitachangia harambee yoyote ile inayoendeshwa na serikali.
 
MPAKA HAPA HILI JAMBO LILIPOFIKIA, CCM NA SERIKALI YAKE WAMEJIPAKA KINYESI NA KUJIPALILIA LAANA NA CHUKI ISIYO KIFANI. YA KAGERA NA ARUSHA NI KIELELEZO AINA YA RAIS, CHAMA NA VIONGOZI WETU AWAMU YA TANO WALIVYO. NI JANGA LA TAIFA NA AIBU YA KIMATAIFA. KUNA HAJA GANI MKUU MZIMA WA MKOA KUFUKUZANA NA VIPESA VYA RAMBIRAMBI KANA KWAMBA HAKUNA KAZI NYINGINE YA KUFANYA MKOA MZIMA.
 
Kusaidia majeruhi hii yote ni zuga zuga ya Gambo ili apige pesa hakuna kingine, huyo muuguzi na daktari awanaotaka kuwatumia dola 5000 si ni watumishi wa umma? Kwani utaratibu wa serikali unasemaje pale mtumishi wa umma anapokua nje ya kituo chake cha kazi, je huwa analipwa na nani? Je ni pesa za michango ya wananchi (rambi rambi na pole) au ni pesa za umma? Huyu kijana asituchezee akili hana haja ya kutoa taarifa yeye azile tu kimya kimya na chama chake lakini si kwa uongo huu,wazazi waliopelekwa ulaya hawahitaji pesa maana hata matembezi hawana wao wanachohitaji ni Afya za watoto wao tu ndio maana hakuna sehemu mzazi ameonekana aki spend time nje ya jengo la hospital
 
Back
Top Bottom