Fatma Karume amshtaki Polisi aliyemzonga Mahakamani, adai fidia ya bilioni moja

hazole1

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
4,319
3,914
Wakili Fatma Karume amefungua kesi ya madai akidai kulipwa fidia ya shilingi bilioni moja kutoka kwa Inspekta (mpelelezi) wa Polisi, Eugene Mwampondela wa Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es salaam.

Wakili Fatma anataka alipwe na mpelelezi huyo kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni moja kwa makosa matatu ya kumuingilia mwilini mwake, kumbughudhi na kumzuia kufanya kazi yake (assault, battery, and misfeasance in public office).

Fatma amesema kuwa Inspekta Mwampondela alimshika na kumvuta mkono, hatua iliyomsababishia maumivu kwenye mkono wake.

“Ukiandika nalishtaki Jeshi la Polisi na wewe nitakufikisha mahakamani. Mimi nimemshtaki Inspekta Mwampondela kwa kosa la kuniingilia mwilini na kunivuta mkono.

“Aliniambia ameagizwa na wakubwa kutoka juu, hivyo namfikisha mahakamani amueleze Jaji huyo aliyemwagiza ni nani. Na mimi sitaki kushikwashikwa mwili wangu, kwahiyo nataka anilipe shilingi bilioni moja ili liwe fundisho kwa wengine,” alisema Fatma Karume.

Fatma alikutana na kadhia hiyo juzi alipokuwa katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam akiwa ni mmoja wa mawakili wa Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Antipas Lissu.

Chanzo: Mtanzania

Kujua kisa na mkasa, soma=>VIDEO: Polisi wamemzuia Fatma Karume Kuongea na Waandishi wa Habari, Wabishana dakika kadhaa
 
Safi sana Fatma najua umeamua kuchagua upande wa wananchi japo umezaliwa upande wa kifalme ni watu wachahe sana wa upande wa ufalme kuamua kuwa upande wa watu simamia haki zako kisheria hili watu wanaotaka kuwarizisha wafalme wajifunze uko mbeleni wakumbuke kuwa yakiwakuta wanakuwa wako peke yao
 
Hiyo kesi itupiliwe mbali na mahakama maana haina mashiko.

Ingekuwa kanaswa kibao kweli. Ila kuzungukwa na watu au hata kuguswa sio kosa. Yeye kama mda wake wa kazi mahakamani uliisha alitakiwa aondoke ili wengine waweze kutumia mahakama.

Polisi walikuwa na haki ya kumzuia kuigeuza mahakama kuwa political platform na walimwambia apande kwenye gari lake akaongee na waandishi wa habari ofisini kwake.

Tena polisi walimstahi, ilitakiwa FFU wawe wameshamlamba virungu kwa kuleta bugdha mahakamani. Ana bahati sana mtafuta kiki huyu...
 
hii ni kutuma ujumbe kwa polisi wengine kuwa sio kila muda unapaswa kumzongazinga mtu kumshika shika utakavyo kwa kuwa tu umevaa uniform za upolisi.

Siku nyingine watakuwa na staha kidogo Mbona kamanda siro aliookuwa hataki mikusanyiko alikuwa anawasihi watu kwa lugha ya kistaarabu na wanatii?
 
Hiyo kesi itupiliwe mbali na mahakama maana haina mashiko. Ingekuwa kanaswa kibao kweli. Ila kuzungukwa na watu au hata kuguswa sio kosa. Yeye kama mda wake wa kazi mahakamani uliisha alitakiwa aondoke ili wengine waweze kutumia mahakama. Polisi walikuwa na haki ya kumzuia kuigeuza mahakama kuwa political platform na walimwambia apande kwenye gari lake akaongee na waandishi wa habari mahakamani. Tena polisi walimstahi, ilitakiwa FFU wawe wameshamlamba virungu kwa kuleta bugdha mahakamani. Ana bahati sana mtafuta kiki huyu...
Yule ni wakili Hana mteja mmoja anawawakilisha na watu wengine pia yey ni officer of the court, sasa kumfukuza na kumzuia kuzungumza na mteja wake mahakamani hlo ni Tatizo.
 
Hiyo kesi itupiliwe mbali na mahakama maana haina mashiko.

Ingekuwa kanaswa kibao kweli. Ila kuzungukwa na watu au hata kuguswa sio kosa. Yeye kama mda wake wa kazi mahakamani uliisha alitakiwa aondoke ili wengine waweze kutumia mahakama.

Polisi walikuwa na haki ya kumzuia kuigeuza mahakama kuwa political platform na walimwambia apande kwenye gari lake akaongee na waandishi wa habari mahakamani.

Tena polisi walimstahi, ilitakiwa FFU wawe wameshamlamba virungu kwa kuleta bugdha mahakamani. Ana bahati sana mtafuta kiki huyu...
Kawe wakili wa polisi maana mwenzako maji ya shingo yamemfika
 
Back
Top Bottom