Fashion za nguo ambazo sizipendi nikaona bora zinipite

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,122
22,449
Mimi ni mtu ninayependa kuvaa vizuri na kula vizuri. Kumbukumbu zangu zinaonyesha mara ya mwisho kununua mtumba ni miaka mingi ishapita hata zaidi ya 10. Nilijiambia bora niwe na nguo chache ila za ubora wa hali ya juu ambazo hata nikivaa najiongezea thamani yangu. Na ninapenda fashion nzuri. Nikiwa na pesa mingi nitaajiri fashion designer.

Pamoja na yote ila kuna fashion ambazo nilisema potelea mbali acha zinipite. Sikuzipenda kabisa. Zile kaptula fupi zinazovaliwa na vijana siku hizi ninazichukia kama waislamu wanavyochukia kitimoto. Ninatupia picha muelewe.

f986a2d231f220f1af47ce5fead82819.jpg

GettyImages-906655_dajyx3.jpg

71S0IJB5JrL._AC_UF894,1000_QL80_.jpg

images.jpeg

 
Ukiona mtu anavaa ivo vibucta vifup jua ana dalili ya ushoga au bange sana, ukiona mtu anavaa design ya ayo ya kijani jua ni mfupi kwaiyo aina nying za nguo hazimpendezi anajifichia kwenye ayo
na ss tunaovaa suruali za kacha je...?
 
Mie siwezi kuvaa vinjunga(vibukta hivyo), siwezi kuvaa modo yaani kasuruwali kamebanaaa, na wala siwezi kuvaa bwanga, msuruali huo kama enzi za fubu, pia nguo kama alizovaa huyo mase sivai, vitu ambavyo vipo kwenye trend huwa si mvaaji kwa kweli, jinzi ina rangi ya pink, sijui rangi za hovyo hovyo siwezi, kuvaa miwani kwangu changamoto, kipindi fulani vilitoka viatu vya yebo yebo kila bishoo anatinga, yebo yebo kali, mjinzi wa fubu na mjezi wa basketball, micheni inatiririka shingoni 😂, sijawahi fikiria kuvaa cheni.
 
Back
Top Bottom