Famous Quotes by Julius Nyerere

Siwezi kuwaachia mbwa nchi watawale.

Umeshiba jasho la watu maskini wewe,hujawahi kupata ajira lakini ukwasi wako unatisha,heri kuwa na mbwa anayefugwa na kutoa ulinzi nyumbani kuliko kuwa nyoka (ccm) anayeuma na kuua watu na ana sumu ya kutisha.
 
Hii nukuu zinalingana na muktadha(context) aliiongelea wapi katika mazingira yepi? Ukijua unainukuu katika mazingira hayo hayo kukazia hoja sio unaandika andika tu eboo

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Tunazikumbuka hizo busara za Mzee wetu hasa kipindi hiki kilichojaa taflan na chengachenga nyingi kwa kila jambo.
 

Hizi ni baadhi tu ya nukuu hizo:​


    1. Hakuna taifa lenye haki ya kufanya maamuzi kwa ajili ya taifa jingine ; hakuna watu kwa ajili ya watu wengine. ( Kutoka 'Ujumbe wa amani wa mwaka mpya ,Tanzania, Januari 1968).
    2. Watu wanapaswa kuhusishwa, ili kufikia maendeleo ya kweli. (Julius Kambarage Nyerere (1974).
    3. Elimu sio njia ya kuepuka umaskini , ni njia ya kupigana nao.
    4. "Umoja hautatufanya kuwa tajiri, lakini unaweza kuwezesha kuiepusha Afrika na watu wa Afrika kutoheshimiwa na kudhalilishwa ". Kutoka katika hotuba aliyoitoa Accra, Ghana, Machi 6, 1997.
    5. Katika Tanganyika tunaamini kuwa ni waovu , watu wasiomuamini Mungu wanaoweza kuifanya rangi ya mwili ya binadamu kuwa kigezo cha kumpa haki zake za kiraia ". Akizungumza na Gavana wa Uingereza , General Richard Gordon Turnbull, kabla ya kuchukua kiti cha uwaziri mkuu mnamo mwaka 1960.
    6. "Demokrasi sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza kuiagiza. Demokrasi inapaswa kuendelezwa kulingana na nchi yenyewe ". Juni 1991 mjini Rio De Janeiro, Brazil.
    7. Hatuwezi kuwa na matumaini ya kutatua matatizo yetu kwa kujifanya kuwa hayapo.
    8. Itakuwa yote ni makosa , na si jambo la muhimu , kuhisi kuwa lazima tusubiri hadi viongozi wafe ndio tuanze kuwakosoa " JK Nyerere.
    9. "Demokrasi sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza kuiagiza. Demokrasi inapaswa kuendelezwa kulingana na nchi yenyewe ". alisema Juni 1991 mjini Rio De Janeiro, Brazil
    1602658359454.png
 
*Nukuu za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K.Nyerere katika Mikutano yake tofaut baada ya Uhuru*

1.Tumekubaliana kwamba tunataka kujenga Taifa lenye uhuru wa kweli,Siyo uhuru wa bendera tu,tumekubaliana kwamba tutaamua mambo yetu wenyewe kwa utashi wetu wenyewe na kwa manufaa yetu wenyewe
1971

2.Chama chochote kinapenda umoja kwa hivyo kinapenda Mshikamano wa Viongozi wake wakuu katika masuala yote muhimu.Na kama viongozi wanao msimamo huo kuwapinga tu kwa ajili ya kupinga ni jambo la Kipumbavu:

(Uongozi wetu na hatima ya Tanzania :63)

3.Daima hatutakubali kuwa vivuli,Vibaraka au Vijibwa vya Watu wengine au Taifa jingine.Hivyo tumeelewana sisi wenyewe na ndivyo dunia inavyotuelewa:
(Mwaka 1989)

4.Ujamaa Maana yake si kugawana Umaskini kwa usawa:Maana yake ni maendeleo ya watu wote na kugawa mali inayopatikana kwa haki kati ya wote walioizalisha ,Isipokuwa wale wenye haki ya kula bila kufanya kazi
(Mkutano Mkuu Maalum wa CCM 1985)

5."Zanzibar ikijitenga kutokana na Ulevi tu Sisi Wanzibara ina Wao Watanganyika wakumbuke kwamba Muungano ndiyo Unaofanya wanasema 'Sisi Wanzibar' Wao Watanganyika
(Nyufa: 10)

6.Viongozi wakigawanyika katika Makundi Chama pia huwa kimo katika hatari ya kugawanyika katika Makundi na kukosa shabaha yake"
(Tujisahihishe:11)

7.Viongozi wa Chama, Waliopo na waliong'atuka ,Wanapaswa kusaidiana na wananchi kuanzisha na kuendesha shughuli za Ushirika wa Uzalishaji mali
(Mkutano Mkuu wa CCM 1987:14)

8.Kazi ya Chama ni kuwa macho wakati wote kuangalia yanayotokea nchini,Kuielekeza Serikali.Chama kinahitaji kusikiliza maelezo yanayotolewa na serikali juu ya vitendo vyake na sababu zake
(Mkutano Mkuu Maalum wa CCM 1985)
 
Back
Top Bottom