Faida za choroko na mapishi yake

malisak

JF-Expert Member
Mar 16, 2006
694
773
Choroko ni moja kati ya nafaka zenye kiwango kikubwa cha protini, madini ya phosphorus na calcium. Ukiachilia mbali faida nyingine, virutubisho hivi ni muhimu sana kwa ustawi wa afya ya ubongo.
Wataalam mbalimbali wamenukuliwa na mtandao wa kesehatan.123.com wakielezea umuhimu wa ulaji wa choroko ili kuongeza uwezo wa kufikiri.

Faida nyingine za choroko ni pamoja na kuimarisha mifupa. Hii inatokana na kiwango kikubwa cha madini ya phosphorus na calcium.

Choroko pia ni nzuri kwa afya ya moyo, mafuta yaliyopo kwenye mboga hii ni salama na yana faida katika kuusaidiana moyo kutenda kazi zake vizuri na kwa upande mwingine kusaidia kurahisisha ufyonzwaji wa chakula mwilini hivyo kuepuka hatari ya kupata saratani.

Uwepo wa vitamin B1 na B2 ndani yake husaidia kuimarisha mfumo wa fahamu nasi vizuri kutumiwa na wajawazito kwa sababu zina kiwango kikubwa cha folic acid ambayo ni muhimu kw aukuaji wa mtoto.

Mahitaji
Choroko kikombe 1 na nusu
Nazi kopo 1
Kitunguu kikubwa 1
Nyanya 1/2 kopo
Swaum 1 kijiko cha chai
Curry powder 1 kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Olive oil
Pilipili nzima Ila sio lazima
1691737961072.png


Matayarisho
Loweka choroko usiku mzima kisha zichemshe mpaka ziive na ziweke pembeni. Baada ya hapo saga pamoja nyanya, kitunguu, na swaum kisha vipike mpaka maji yote, baada ya hapo tia mafuta na curry powder, pika mpaka nyanya zitoe mafuta kisha tia choroko,tui la nazi, maji nusu kikombe,pilipili na chumvi, kisha koroga vizuri na uache ichemke. Pika mpaka tui la nazi litakapoiva na rojo ibakie kidogo sana, kisha ipua na mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa.

Mimi huwa napenda kuila na wali ila hata na ugali au chapati inaenda pia. Pia unaweza kupika ukachanganya na mchele ukasonga unakuwa mseto mzuri sana unaweza kula na mboga yeyote uipendayo. Tujitahidi kula vya asili kupunguza uwezekano wa kupata maradhi mbalimbali kwa tunavyokula vyakula vya kileo.

1691738029290.png


KWa wale wapenzi wa vyakula vya majimaji unaweza kutengeneza supu ya choroko ni tamu sana na itakuburisha na kupata faida tajwa hapo juu. Supu hii hupikwa kwa kitumia choroko pamoja na viungo vya aina mbali mbali kama vile; binzari ya manjano, binzari nyembamba na tangawizi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya choroko tamu sana na utapenda ladha yake.

MAHITAJI:
¼ kijiko cha chai cha binzari ya manjano
½ kikombe cha choroko
½ kikombe cha majani ya giligilani yaliyo katwa katwa
½ kijiko cha chai cha mbegu za haradali
½ kijiko cha chai cha binzari nyembamba ya unga
½ kijiko cha chai cha pilipili manga ya unga
½ kijiko cha chai cha chumvi
2 vijiko vya chakula vya limao lililo kamuliwa
2 vijiko vya chai vya mafuta ya kupikia
2 vijiko vya chai vya tangawizi iliyo twangwa
6 vikombe vya maji
6 majani ya mvuje

NAMNA YA KUANDAA:

Chukua bakuli ndogo. Weka kikombe 1 cha maji, kisha roweka choroko ndani ya hilo bakuli lenye maji, kwa muda wa dakika 30.

Baada ya dakika 30, mimina choroko hizo zilizo rowekwa kwenye sufuria kubwa. Weka pia kwenye hilo sufuria, binzari ya manjano, chumvi, pamoja na vikombe 2 vya maji, kisha weka sufuria hilo kwenye jiko lenye moto mkubwa, halafu acha ichemke.

Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu acha iendelee kuchemka huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 20 mpaka 30, au hadi utakapo ona choroko zimeiva, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka mchanganyiko wa choroko ulio chemsha kwenye hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

Mimina mchanganyiko wa choroko ulio usaga kwenye lile sufuria kubwa ulilotumia kuchemsha mchanganyiko huo wa choroko. Weka tangawizi pamoja na vikombe 4 vya maji, kisha funika sufuria na acha ichemke katika moto mkubwa. Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria halafu acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5.

Chukua sufuria nyingine ndogo lenye mafuta ya kupikia na uweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka mbegu za haradali, binzari nyembamba, pilipili manga pamoja na majani ya mvuje, halafu kaanga kwa muda wa sekunde 30, kisha epua mchanganyiko huo na umimine kwenye sufuria lenye supu.

Weka limao pamoja na majani ya giligilani, halafu koroga vizuri. Acha supu ichemke kwa muda mfupi, kisha epua na upakue kwenye bakuli tayari kwa kunywa. Unaweza kunywa na mkate ama kitafunwa chochote ukipenda ila si lazima maana hata yenyewe ukinywa unashiba vizuri. Enjoy!




1691738315136.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom