Fahamu kuhusu Private Jets

Mla Bata

JF-Expert Member
Jan 24, 2013
7,417
15,961
Wasalaam,

Ulikuwa unafahamu hili?

Duniani kote inakadiriwa ni ndege 23,241 pekee zimesajiliwa kama ndege binafsi (private jets) ambazo zinatumiwa na kumilikiwa na watu maarufu pamoja na wafanya biashara wakubwa duniani kote, huku taifa kubwa la Marekani likiwa na asilimia 63 ya sajili ya ndege zote binafsi ulimwenguni.

B4548AA4-A583-41EC-8D1B-742471FDBBF9.jpeg


Idadi hiyo inaweza kuwa imekushangaza, ni ndogo of course ukifananisha na namba ya mabillionare matajiri na watu maarufu duniani kote. Kwanini?

0F4DBE6A-AF64-4B9B-A28B-8DDF829A6083.jpeg


Licha ya Umiliki wa ndege binafsi kwa wafanyabiashara na watu maarufu duniani kuwa ni alama ya utajiri, huku ukimpa muhusika uhuru na faragha katika mambo yake, na kwa upande mwingine private jets si tu inakupa uharaka lakini flexibility na urahisi wa kuepukana na usumbufu wa kuconnect ndege na usumbufu mwingine katika ndege za jamii lakini bado ukweli unabaki kuwa kuwa kumiliki private jets na kuzirun is not for everyone 😅

0890D39E-17AF-49C6-9819-1CD583AABA3A.jpeg



Well, leo nimekuletea ABCs kuhusu umiliki, gharama na aina mbalimbali za hizi private jets. Twenzetu,

Umiliki wa ndege binafsi upo wa namna mbili, moja ni ile namna ya kununua na kumiliki ndege kwa asilimia 100 na kuwa mmiliki halali wa ndege hiyo. Lakini upande wa pili unaweza kumiliki ndege kwa asilimia kadhaa ya gharama yake husika na muhusika kupata nafasi ya kuitumia kwa gharama zake kutegemea na vipengele na makubaliano ya pande zote za wamiliki.
Najua una hamu ya kufahamu ni kwa gharama gani unaweza kumiliki ndege binafsi duniani.

Gharama ya ndege binafsi inatokana na

•Aina ya ndege husika

•Ukubwa wa ndege na uwezo/umbali wa kuruka kutoka point moja kwenda nyingine kwa mruko mmoja.

•Kampuni husika, class, model.

•Masaa na idadi ya miruko ya ndege husika tangu kutengenezwa kwake. The more kilometers na miruko mingi ya ndege na ndio gharama inapungua.

Kama ilivyo kwa vyombo vingine vya usafiri kwa ndege pia zipo zile ambazo ni second hand (pre-owned private jets) ambazo zilishamilikiwa na kutumika kabla na kuna zile ambazo ni mpya kabisa, hii inaweza kudetermine gharama ya kununua na kumiliki ndege.

Inakadiriwa, ili kuweza kumiliki private jet, basi ni lazima atleast uwe na kuanzia USD 3 Millions mpaka USD 78 Millions. Ambapo kwa madafu ni karibia sh bilioni saba taslimu na kuendelea.

Surprisingly zipo ndege binafsi za luxury mpaka USD 500,000 takribani shilingi bilioni moja za kitanzania. Mind you gharama hizi za private jet ni gharama za kununua tu ndege hizo husika, hazihusiani na gharama za kuajiri flight crew, gharama za urushaji, na leseni mbalimbali za umiliki wa ndege binafsi.

Ndege hizi binafsi pia zimegawanyika kwa makundi manne kama ifuatavyo.

Very light jets
Hizi ni ndege ndogo sana na zenye uzito mdogo na pia zenye uwezo wa kubeba namba ndogo ya abiria (wastani wa abiria wanne). Ndege hizi mara nyingi zina uwezo wa kuruka takribani masaa mawili kwa mruko mmoja kutoka point A kwenda B huku zikiwa zinaongozwa na idadi ya pilot mmoja tu. Kundi hili linaingia ndege za bei ya chini kuliko zote kwenye makundi ya private jets, huku ikikadiriwa kuwa na idadi ya ndege 2000 zilizosajiliwa kuoperate duniani kote.

Kwenye kundi hili aina ya ndege maarufu za Cessna citation mustang zinaongoza kuwa kwenye category hii huku ikiaminika kati ya ndege 2000 za very light private jets ndege 487 za kampuni hiyo zina operate duniani kote huku nyingi zikiwa zinamilikiwa na kampuni ya Usafirishaji ya GlobeAir.


50DA17FE-B6A5-48D2-8FD0-342A054B6422.jpeg


C635CEAF-7177-463D-8190-ED88EF8D383F.jpeg



Light Jets
Hizi ni ndege zenye uwezo zaidi ukifananisha na very light ones kuanzia namba ya abiria (kuanzia 6-8 abiria) muda unaotumika kuruka kutoka point moja mpaka nyingine kwa mruko mmoja. Na inakadiriwa ndege hizi unaweza kupata kuanzia USD 5 millions kwa pre owned mpaka USD 10 millions kwa zile mpya. (Bilioni 12 mpaka 24 za kitanzania)

Medium Jets

Kama unahitaji private jets zenye nafasi za kutosha na zinazoweza kubeba namba kubwa ya abiria (up to 10 passengers) basi aina hizi za ndege ndio chagua sahihi zaidi huku zikiwa na options za kutua hata kwenye viwanja rough na zinaweza kuruka takribani masaa nane kwa mruko mmoja bila kituo. Mifano ya medium Jets maarufu ni kama Hawker 800XP, learjet 55B, G100 na Falcon 200.

19B80225-E8C4-48C9-B689-BB8A3A54B410.jpeg

Hawker 800XP


Large Jets

Group hili linajumuisha ndege private kubwa zaidi ambazo zinauwezo wa kuruka masafa marefu zaidi na hata kukatisha bahari kubwa kutoka bara moja kwenda jingine huku zikiweza kutumia zaidi ya masaa 12 kwa mruko mmoja kutoka point moja kwenda nyingine.

Kwenye kundi hili unaweza kupata ndege kuanzia USD 8 millions mpaka USD 70 millions kwa kampuni maarufu kama Gulfstream G700 zenye engine za Rolls-Royce Pearl 700 huku ikikadiliwa kumiliki takribani ndege 600 katika kundi hili la ndege kubwa za private.

B07D005E-BD57-419D-9BB1-6A15AFD631CE.jpeg

Gulfstream G550

Mpaka sasa makadilio ya private jets za gharama kabisa duniani ni kama ifuatavyo

•Air force one - USD 660 millions

•Airbus A380- USD 600 millions

•Airbus A340-USD 500 millions

•Boeng 747-8 VIP-USD 367 millions

Hii ni list ya wasanii na baadhi ya watu maarufu barani kwetu afrika wanaomiliki private jets.

Aliko Dangote -Bombardier Global Express XRS $45 Million.

Adedeji Adeleke (Davido’s Father)-
Bombardier Global Express 6000 - $62 million
Davido -Bombardier challenger 605- USD 27 Millions

Wiz kid- price unknown

Tiwa Savage-Price unknown

Don jazzy- Price unknown

Dj Cuppy- Price unknown

Swali, kibongo bongo watu wetu maarufu na wasanii wetu hili la kumiliki na kuoperate ndege binafsi linawezekana???
Imeandaliwa na kuchapishwa na Mla Bata


Sources.

https://compareprivateplanes.com
https://www.avbuyer.com

https://www.youthhekima.com

https://www.globalair.com

Wasalaam.
 
Back
Top Bottom