Fahamu kama namba yako ya NIDA ilitumika kusajili laini za simu usizozifahamu kwa mawakala wajanja wa kusajili laini

Wasalaam.

Ili kujua unabonyeza *106# kisha usajili wa NIDA (Utaingiza NIDA ID yako), baada ya hapo zitakuja namba zote zilizosajiliwa kwa ID yako ya NIDA. Kama namba haijui siyo yako maana yake wakala (agent) alifanya ujanja kutumia ID yako kusajili line nyingine.

Ukishaona kwenye list namba haijui basi unaenda kwenye shop iliyokaribu nawe una claim, then customer care anakuambia uweke finger print kisha hiyo namba inafutwa.

Kutokana na watu wengi kutokuwa na NIDA, mawakala wengi walitumia ujanjaujanja wa kusajili line kwa kutumia ID ya mtu mwingine na kuuza hizo line kati ya elfu 5 hadi elfu 20, inategemea watakavyokuona na uhitaji wako.

Mawakala wanafanyaje ujanja? Ukienda kusajili line yako atakwambia weka dole gumba lako baada ya dakika atakwambia network inasumbua hebu ingiza tena, ukifanya hivyo basi hapo jua umeumia, ile ya kwanza amesajili line ya mtu mwingine na ya pili anasajili line yako, kama haujui hiyo mbinu hauwezi kumstukia maana wapo very smart.

Kwahiyo, wote mlionunua line kwa mawakala zilizosajiliwa kwa NIDA maarufu kama Take Away, mjiandae kisaikolojia.

Utabonyeza mbili halafu utaweka namba yako ya NIDA, mwisho utatumiwa SMS ya namba zako zote ulizozisajili kama kuna namba haujaisajili utaenda kwenye shop yoyote ya kampuni ya simu ambayo wewe ni mteja wao halafu utapewa fomu ya ku-remove namba ambazo huzitambui.



Jumanne NJEMA.
Nimesajili laini 2 kwa kitambulisho changu, lakin nikicheck kwa hiyo namba naona namba moja tu,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usipinge kabla hujafanya tafiti , utaribu huu upo mitandao yote ya TZ. Km hujui better uulize ukaeleweshwa.
Nataka kama nacheki kwa kutumia mtandao wa airtel, inipe list yote ya namba za mitandao yote niliyojisajili kwa kutumia hii NIDA yangu.
 
Nashukuru nimeshaangalia, its easy, fast, and free.., mmefanya la maana sana. Ila hili jambo lifanywe kwa mujibu wa sheria, kila mtu alazimike kukagua kama namba yake imesajili namba asizozijua, na iwekwe dead line ya siku 30 kila mtu awe amekagua, baada ya hapo ukifanyika uhalifu basi ahusike.
 
Ww acha kujidanganya kisheria ni kosa kutumia laini yenye jina la mtu mwingine maana yake ile laini siyake niya mwenye jina na hata akifanya tukio lolote la kuvunja sheria za nchi atakaekamatwa au kutafutwa sio anaetumia ni alieisajili ambaye jina lake linasomeka hata kana hujui wala hujahusika hayo yote mpaka yajjlikane ionwkane huna hatia ulisha sota sna gerezani mkuu ww unajua sheria au hujui!!?? Huyo anaetumia hiyo laini akiuamua kumshitaki anaweza kabisaa na sheria inambana sana ndii maana kila mtu inatakiwa awe na kitambulisho chake mwenyewe nasi kutumia cha mwingine mkuu
kwani yeye ndiyo aliyefanya huo ujanja au wakala?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ww acha kujidanganya kisheria ni kosa kutumia laini yenye jina la mtu mwingine maana yake ile laini siyake niya mwenye jina na hata akifanya tukio lolote la kuvunja sheria za nchi atakaekamatwa au kutafutwa sio anaetumia ni alieisajili ambaye jina lake linasomeka hata kana hujui wala hujahusika hayo yote mpaka yajjlikane ionwkane huna hatia ulisha sota sna gerezani mkuu ww unajua sheria au hujui!!?? Huyo anaetumia hiyo laini akiuamua kumshitaki anaweza kabisaa na sheria inambana sana ndii maana kila mtu inatakiwa awe na kitambulisho chake mwenyewe nasi kutumia cha mwingine mkuu
Unapotumia line yenye Jina la mtu mwingine, Kosa linakuwa la wakala anayekusajili au wewe mwenyewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Afisa Uchaguzi,
It is useless maana unakupa tuu laini uliyoko kwenye simu unatumia kuhakiki usajili. Uhakiki ungekuwa na maana kama ungekulotea namba za mitandao yote
Inakuletea namba zote za mitandao yote zilizosajiliwa kupitia namba husika ya NIDA, unazozijua na hata usizozijua, legeza ubongo.
 
Kama unatumia laini isiyo yako yaani ambayo imesajiliwa kwa jina la mtu mwingine ambae humjui maana yake umenunua kwa wakala ambao nao wanazopata pale unaposajili laini yako kwa kutumia kitambulisho chako cha taifa NIDA yy anajiongeza kwa kusajili laini zingine zake kwa kutumia kitambulisho chako ili akaziuze apate hera wakat hui ww hujui maana anakuambia tu oohh rudia kuweka kidole gumba mara imeferi network mbovu kumbe hapo kasha maliza kusajili laini yako tayari na sasa anasajili zake kwa ID yako...


Ili kujua kama kitambulisho chako cha taifa NIDA kimesajili namba zipi na ngapi tazama hii video

Ukikuta kuna laini hujui maana yake kuna wakala kakufanyia ushenzi tayar ww unaweza kuifunga na isitumike na ikaacha kusomeka kwa jina lako, kufahamu yote hata tazama hii video hapa chini

Pia una uwezo wa kumshitaki wakala na mtu anaetumia laini yako hata kama yy hajui kwann atumie laini isiyo yake na hamjui mwenye aliisajili!?? Kwa hiyo kutokujua hakukupi uharari wa kutumia laini isiyo yako kisheria una kosa hapa la kujibu.. Kwa iyo hauko salama sana cha mhimu we fuatilia upate kitambulisho chako. Maana unapo tumia laini yenye jina langu au la mwingine ukifanya kosa natafutwa mimi ndio maana ni kosa kisheria.. Mimi nipate kesi ya ujambazi au ubakaji au wizi kwa ajili yako tu.


Kufahamu yote haya angalia hii video ina majibu ya maswali yote


PAMOJA NA MAELEZO MAZURI NDAN KUNA MABWEGE WANAPINGA HAIWEZEKAN AISEE [/B][/QUOTE]
 
Back
Top Bottom