EXCLUSIVE UPDATES: Uchaguzi Mkuu Kenya Agosti 8, 2017

Kenyan

JF-Expert Member
Jun 7, 2012
414
314
OFFICIAL PRESIDENTIAL RESULTS:

01:20am August 09, 2017 UPDATE:

Tume ya Uchaguzi(IEBC) Imetangaza matokeo ya vituo 29,209 kati ya 40,883. Uhuru Kenyatta kura 6,044,745 (55.27%) na Raila Odinga kura 4,805,159 (43.93%).

09:00am August 09, 2017 UPDATE:

Tume ya Uchaguzi(IEBC) imetangaza matokeo ya vituo 36,912 kati ya 40,883. Uhuru Kenyatta kura 7,511,454 (54.62%) na Raila Odinga kura 6,124,426 (44.53%)

12:00pm August 09, 2017 UPDATE:

Tume ya Uchaguzi(IEBC) imetangaza matokeo ya vituo 38,341 kati ya 40,883. Uhuru Kenyatta kura 7,776,101 (54.4%) na Raila Odinga kura 6,394,921 (44.74%)

3:00pm August 09, 2017 UPDATE:

Tume ya Uchaguzi(IEBC) imetangaza matokeo ya vituo 39091 kati ya 40,883. Uhuru Kenyatta kura 7,915,044 (54.35%) na Raila Odinga kura 6,520,918 (44.78%)

August 10, 2017 - 06:30am UPDATE:

Uhuru - 8,030,150 (54.27%)
Raila - 6,634,331 (44.84%)

Valid votes: 14,795,377
Reporting Stations: 39,755 out of 40,883

August 11, 2017 - 09:30PM UPDATE:

Uhuru - 8,196,313 (54.19%)
Raila - 6,793,919 (44.92%)

Valid votes: 15,124,547
Reporting Stations: 40,711 out of 40,883

LIVE VIDEO FEED:

Augus 11, 2017 IEBC Press Briefing




fe7a316c97d3b4563a4c2cbca91a7a97.jpg


c6e580981b0395e5277b6f9e203969ff.jpg


FACT 1: Kenya spent 49.9billion Kshs to organize this election and it's the most expensive since country's independence

KENYA: Uchaguzi Mkuu unafanyika leo, Wapiga kura milioni 19 watachagua Rais, Wabunge, Maseneta, Magavana, Madiwani na Wawakilishi wa Wanawake.

Raia wa Kenya wataamua nani atakuwa Rais wao na Makamu wa Rais kwa miaka 5 ijayo.

Ushindani mkubwa sana uko kati ya vyama vya Jubilee na NASA na wagombea wake wa Urais, Uhuru Kenyatta na Raila Odinga.

Pamoja na kura ya urais pia watapiga kura ya kuchagua magavana wa Kaunti, wawakilishi wa kata(madiwani) na wawakilishi wa Seneti na Bunge.

Fuatilia hapa kupata updates za uchaguzi huu unaohusisha takribani wapiga kura milioni 20 waliojiandikisha.

Waliojiandikisha: Milioni 19
Vituo vya kupigia kura: 40,000
Idadi ya Wakenya: Milioni 48

WASIFU WA WAGOMBEA KWA UFUPI

Tume Huru ya Uchaguzi Kenya (IEBC) iliwaidhinisha wanasiasa wanane ambao watawania urais katika uchaguzi mkuu huu wa Agosti mwaka huu.
Walioidhinishwa ni pamoja na Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee ambaye atakuwa anawania kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa pili, na kiongozi wa muda mrefu wa upinzani Bw Raila Odinga ambaye anawania urais kwa mara ya nne.

Bw Odinga, aliyehudumu kama waziri mkuu katika serikali ya muungano ya Rais Mwai Kibaki kati ya 2008 na 2013, anawania urais chini ya umoja wa vyama vya upinzani kwa jina National Super Alliance (NASA).

Katika uchaguzi huu wa tarehe 8 Agosti, kutakuwa na wagombea wanne pia ambao ni wagombea huru (hawana vyama).

Abduba Dida

Anawania urais kupitia chama cha Alliance for Real Change (ARK) na muungano wa Tunza Coalition.
Alikuwa mwalimu wa shule ya upili ya Lenana jijini Nairobi.
Hii ni mara yake ya pili kuwania urais baada ya mwaka 2013 ambapo alipata kura 52,848 na kumaliza wa tano.

Cyrus Jirongo

Ni mwanasiasa na mfanyabiashara ambaye ni mara yake ya kwanza kuwania urais. Anawania kupitia chama cha United Democratic Party (UDP).

Alipata umaarufu kisiasa mwaka 1992 alipokuwa katika kundi la vijana wa chama cha KANU, Youth for KANU 1992 waliokuwa wakimfanyia kampeni Rais Daniel arap Moi wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka huo.

Ekuru Aukot

Anawania urais kupitia chama cha Thirdway Alliance Kenya (TAK), na ni mara yake ya kwanza kuwania urais. Alihudumu kama katibu katika Kamati ya Wataalamu waliosaidia kutunga Katiba Mpya ya Kenya ambayo iliidhinishwa na kuanza kutekelezwa mwaka 2010. Asili yake ni Kapedo, Turkana kaskazini magharibi mwa Kenya na amejitangaza kama mtu anayeleta mwamko mpya katika uongozi nchini Kenya. Amekuwa pia akitetea makabila madogo.

Japhet Kaluyu

Ni mgombea huru ambaye amerejea nchini Kenya hivi majuzi kutoka Marekani. Amejieleza kama mwalimu, mshauri na mwandishi ambaye ana uzoefu wa kufanya kazi Wall Street. Anasema amebobea katika utafiti katika sekta ya afya na msomi. Ni mara yake ya kwanza kuwania urais.

Joseph Nyagah

Ni mwanasiasa wa muda mrefu nchini Kenya ambaye alihudumu kama waziri wa vyama vya ushirika chini ya Rais Mwai Kibaki, na baadaye akawa mshauri wa Rais Kenyatta. Babake, Jeremiah Nyagah, alikuwa waziri wakati wa utawala wa mwanzilishi wa taifa la Kenya Jomo Kenyatta.

Bw Nyagah, ambaye alikuwahi kuwakilisha Kenya katika Umoja wa Ulaya, alihudumu kama mbunge wa eneo la Gachoka, Kaunti ya Embu mashariki mwa Kenya kabla ya kuteuliwa waziri. Anasema ndiye pekee anayeweza kutatua matatizo yanayoikumba Kenya, kutokana na uzoefu wake katika uongozi.

Akihojiwa na runinga ya NTV baada ya kuidhinishwa, alidokeza kwamba aliacha kazi yake ya kuwa mshauri wa rais baada ya kugundua kwamba ushauri aliokuwa anaoutoa haukuwa unafuatwa.

Prof Michael Wainaina

Yeye ni mgombea huru ambaye amekuwa mhadhiri wa fasihi katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. Amekuwa mkosoaji mkuu wa mfumo wa sasa wa kisiasa Kenya na pia mchanganuzi wa siasa. Anasema aliamua kuwa mgombea huru kwa sababu vyama haviwapi nafasi vijana na wanawake.

Raila Odinga

Ni kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) ambaye anawania chini ya muungano wa vyama vya upinzani kwa jina National Super Alliance (NASA). Aliwahi kuhudumu kama waziri mkuu wa kwanza wa Kenya, wadhifa ulioundwa kufuatia Mkataba wa Kitaifa ulioafikiwa kumaliza ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007-2008, ambapo aligawana mamlaka na Rais Mwai Kibaki.

Ni mara yake ya nne kuwania urais Kenya. Mwaka 2013, akiwa bado na mgombea wake wa sasa Makamu wa Rais wa zamani Kalonzo Musyoka, alishindwa na Rais Uhuru Kenyatta. Alipinga matokeo hayo mahakamani lakini mahakama ikatupilia mbali kesi hiyo.

Uhuru Kenyatta

Anawania kwa muhula wa pili kupitia chama cha Jubilee Party ambacho asili yake ni muungano wa Jubilee wa vyama vya TNA na URP alioutumia kushinda urais mwaka 2013. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ni mwanawe mwanzilishi wa taifa la Kenya Mzee Jomo Kenyatta. Mgombea wake mwenza ni Bw William Ruto kutoka eneo la Bonde la Ufa la Kenya. Wawili hao wanawaomba wapiga kura kuwachagua tena kuendeleza maendeleo ambayo wanaamini serikali yao imetekeleza katika kipindi cha miaka minne ambayo wamekuwa madarakani.

Bw Kenyatta aliwania urais mara ya kwanza 2002 dhidi ya Mwai Kibaki kupitia chama kilichokuwa kinatawala wakati huo, chama cha KANU cha Rais Moi aliyekuwa anaondoka madarakani baada ya kuongoza kwa miaka 24. Alishindwa na akawa kiongozi wa upinzani na kwa pamoja na Bw Odinga wakafaulu kupinga Katiba Mpya iliyopendekezwa mwaka 2005. Mwaka 2007, alimuunga mkono Rais Kibaki uchaguzini.

========

UPDATES:

d8a791dd363227292d5e7e5d0038f123.jpg

Man on a life support machine casts his vote at Dandora Primary School

LIVE TEXT FEED:

08:50am updates

> Rais Uhuru Kenyatta amewataka wakenya wajitokeze kwa wingi kuchagua viongozi wanaowapenda

> NASA wameamua kufuta kauli yao dhidi ya KDF baada ya kuhakikishiwa kuwa kila kitu kitaenda kwa mujibu wa taratibu na sheria

> Waangalizi wa EU wameridhika na mwenendo unaoonekana hadi sasa

> Wakenya wengi wamekiri kuwepo kwa propaganda kwa njia ya mitandao ya kijamii na hivyo kuwachanganya wengi

09:50am updates

df39ac57afe4eb0c080a6da1047863ce.jpg

> Takribani Wafungwa 167 wameruhusiwa kupiga kura na hata wanahabari wameruhusiwa kuhojiana nao kupata maoni yao juu ya uchaguzi huu (picha inajieleza)

> Tume ya Uchaguzi(IEBC) imekanusha kukwama kwa zoezi la Uchaguzi huko Kisumu. Wamesema kila kituo kuna vifaa vya akiba

> Gavana Wycliffe Oparanya amepiga kura katika Shule ya Msingi ya Mabole, Butere. Amewataka Wakenya kufanya uamuzi wa busara

11:30am updates:

> Waziri wa Kilimo katika Kaunti ya Meru, Genaro Gatangugi na Mbae Kiugo wameshambuliwa na wananchi baada ya kufumaniwa wakinunua vitambulisho eneo la Imenti Kusini

12:00pm updates:

> Mgombea Urais, Raila Odinga(NASA) anaelekea kupiga Kura katika kituo cha shule ya msingi Kibera

> Mgombea Urais kwa tiketi ya Jubilee, Uhuru Kenyatta amepiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Mutomo, Gatundu Kusini

> Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 64, Patrick Wame amezirai na kufariki dunia baada ya kupiga kura ktk kituo cha Lela, Nyando.

> Maafisa wawili wa Tume ya Uchaguzi(IEBC) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujaribu kubadili majina ya makarani wa vituo. Maafisa hao walitaka kuwaweka Makarani wanaowataka wao kinyume na utaratibu. Tukio limetokea Kandara, Murang'a.

> Watu 24 wamejeruhiwa katika kituo cha Shule ya Msingi Moi Avenue baada ya kukanyagana wakati wakisubiri kupiga kura.

======
3: 00 PM UPDATES


> Mwanamke mmoja amejifungua Mtoto wa Kike katika kituo cha kupigia kura kilichopo Pokot Kaskazini. Mtoto huyo amepewa jina la Chepkura kwasababu amezaliwa siku ya uchaguzi.

> Mawakala watatu wa Jubilee wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuendesha zoezi la kuhesabu kura ktk Kituo cha Heshima Shule ya Msingi.

> Gari moja lenye namba za usajiri bandia za KBY 840C likiwa katika msafara unaolindwa limekamatwa na Maafisa wa Jeshi la Polisi na kukutwa na karatasi za kura ziliwe zimewekewa alama kwa Wagombea wa Jubilee. Limekamatwa huko traveling under escort found carrying (KIEMS) Mandera, Banissa.

> Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi(IEBC), Wafula Chebukati atoa taarifa fupi ya namna Uchaguzi unavyoendelea nchini humo.
  • Wafula Chebukati akiongea na Waandishi wa habari asema zoezi la Uchaguzi linaendelea vyema kwa maeneo mengi nchini humo.
  • Zoezi la kupiga kura linaendelea vyema Magerezani, kwa yale maeneo yaliyochelewa kuanza kupiga kura wataongezewa muda.
  • Chebukati: Vituo vitatu vilivyopo Laikipia vilipata changamoto za kiusalama lakini changamoto hizo zimetatuliwa na zoezi la kupiga kura linaendelea.

=====

4: 00 PM UPDATES

> Rais mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki, amekwama kupiga kura baada ya kukosa jina lake kwenye orodha ya majina ya wapiga kura iliyotolewa na Tume

> Katika vituo vipatavyo 40,883 vya kupigia kura, vituo sita vilikuwa na mpiga kura mmoja aliyeandikishwa.

> Raia wa kenya 4,300 walijiandikisha katika nchi za Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na Afrka Kusini. Wamepiga kura katika nchi hizo.


5:34 PM
> Hatimaye Rais Mstaafu, Mwai Kibaki afanikiwa kupiga kura ikiwa ni dakika 34 baada ya muda wa kupiga kura kuisha.

> Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi(IEBC), Wafula Chekibukati amesema vituo 300 vimeongezewa muda wa kupiga kura kutokana na changamoto mbalimbali.

Ametoa mfano wa baadhi ya vituo hivyo na changamoto zilizojitokeza;
  • Huko katika Kaunti ya Turkana vituo 18 havikufunguliwa kwa wakati kutokana na kunyesha kwa mvua kubwa kuanzia usiku wa kuamkia leo.
  • Jimbo la Ndia ambalo linavituo vya kupigia kura vipatavyo 70 ambavyo vilikumbwa na changamoto ya kuishiwa na karatasi za kupigia kura. Pia Vituo vya Nakuru Mashariki(Eneo lenye vituo 185) vilikumbwa na changamoto hiyo.
01:30am UPDATE:

Viongozi wa NASA wayakataa matokeo yote yaliyokwishatangazwa na IEBC kwa madai kuna faulo zinachezwa kwani fomu nambari 34A haijatumika kama sheria inavyoelekeza.



======

9th August, 2017

UPDATES 12:00 PM


> Kiongozi muandamizi wa NASA, Kalonzo Musyoka amewataka Wakenya kuwa watulivu. Wanaendelea kufuatilia malalamiko ya udukuzi.

> Askari Polisi wamewatawanya kwa mabomu ya machozi wafuasi wa Raila Odinga waliokuwa wameanza kuandamana.

c395a95e-cda3-4f58-acd8-8c7b7391833b.jpg
e90c086a-e49d-4653-89aa-87e8e8e1d2ef.jpg

1: 30 PM
> Wanaharakati wameungana na Raila Odinga kuyakataa matokeo ya Uchaguzi. Wameituhumu IEBC kumpendelea Uhuru Kenyatta.
  • Wanaharakati wameungana na Raila Odinga kuyakataa matokeo ya Uchaguzi. Wameituhumu IEBC kumpendelea Uhuru Kenyatta.
  • Chini ya Kempeni ya 'Kura Yangu Sauti Yangu' wamesema matokeo yamekiuka Katiba kwani hayajaambatanishwa na Fomu 34A.
  • Kiongozi wa Wanaharakati hao, amedai Sheria inaitaka Tume ya Uchaguzi kutoa Fomu namba 34A lakini hawajafanya hivyo.
  • Kundi hilo limeenda mbali na kudai Tume ya Uchaguzi(IEBC) imepunguza kura za Raila Odinga na kumuongezea Uhuru Kenyatta.
  • Mfano matokeo ya Uchaguzi ktk vituo vya Dagoretti, Langata, Nandi, Kisumu na Kepchebor yametofautiana na nakala za Fomu.
2:40 PM
> Mtu mmoja amefariki kwa kupigwa risasi na Askari wa Jeshi la Polisi akiwa nje ya kituo cha kujumlishia kura cha Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Nduru kilichopo Kusini mwa Jimbo la Mugirango.
  • Mmmoja wa mashuhuda bwana Evans Okemwa amesema Mwanaume huyo amepigwa risasi mgongoni huku akilalamika kuwa hakukuwa na sababu ya msingi ya Askari huyo kufanya unyama huo.
  • Kamanda wa Polisi wa Kisii, Abdi Hassan amesema kuwa Askari huyo aliyefanya tukio hilo tayari amewekwa rumande kwa hatua zaidi za kisheria.
  • Shuhuda mwingine Bi. Evelyn Nyaboke amesema alimuona marehemu akijaribu kuwaamua wenzie wawili waliokuwa wakipigana lakini chakushangaza ni kwamba Askari huyo ambaye alikuwa mbali na tukio hilo alifyatua bomu la machozi kisha kumpiga risasi kijana huyo.
3:15 PM
> KENYA: Tume ya Uchaguzi(IEBC) imetangaza kuyafuta matokeo ya Uchaguzi ktk kituo cha Enenkeshui Jimbo la Kilgoris.
  • Akitangaza hatua hiyo Afisa wa Tume ya Uchaguzi(IEBC), Elijah Ombogo amesema kuwa wamebaini idadi ya walioandikishwa ni 285 lakini kura zilizopigwa siku ya uchaguzi(Jana) ni 325.
> Mgombea binafsi wa Kiti cha Urais, Japhet Kavinga amekubali kushindwa katika kinyang'anyiro hicho. Amesema si rahisi kutoka kura 10,000 alizonazo hadi kura 9,000,000.
  • Ameahidi kumuunga mkono mgombea yeyote atayeibuka mshindi pia ameahidi kumpatia ushirikiano.
> Viongozi wa Dini wameitisha mkutano na Waandishi wa Habari huko Bomas ili kuongelea mwenendo wa matokeo ya Uchaguzi.

  • Tutafanya mazungumzo na Wanasiasa, pia tutahusishwa katika kujumlisha kura mwisho tutatoa mtazamo wetu.
  • Tunawaomba Wananchi wawe watulivu na sisi tutatoa mtazamo wetu utakao kuwa huru kabisa.
4:00 PM
> MACHAKOS: Mgombea wa nafasi ya Ugavana, Bi. Wavinya Ndeti ameyakataa matokeo ya awali yanayoonesha mpianzani wake bwana Alfred Mutua anaongoza. Amelalamika na kudai ameibiwa kura.

> Makamu Mwenyeiti wa Tume ya Uchaguzi(IEBC), Consolata Nkatha ametangaza kuanza kwa zoezi la kuhesabu kura za Urais kupitia Fomu namba 34A.

> NAIROBI: Watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi baada ya waandamaji kuwashambulia Askari wa Jeshi la Polisi katika mitaa ya Mathare.

======
10th August, 2017 UPDATES
8:00 AM

> KENYA: Mwanafunzi wa Chuo Kikuu, John Mwirigi(24) ashinda Ubunge Jimbo la Igembe Kusini. Hakuchapisha karatasi za kujinadi kutokana na kukosa fedha.
  • Kijana huyo ambaye ni yatima aligombea kama mgombe binafsi na kumshinda mgombea kutoka chama cha Jubilee.
  • Mwirigi amepata jumla ya kura 18,659 ambazo ni sawa na asilimia 39.09 ya kura zote huku mpinzani wake Joseph Miriti Mwereria amepata 15,635 sawa na asilimia 32.76.
  • Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2013 wananchi wa Meru walimchagua bwana Boniface Kinoti Gatobu kuwa Mbunge akiwa na umri wa miaka 26 na kuliwakilisha jimbo la Buuri.
10:15 PM
> Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) wameipongeza Tume ya Uchaguzi nchini Kenya(IEBC) kwa kuendesha uchaguzi huru na haki.
  • Utaratibu wa kupiga kura uliendeshwa kwa haraka kitendo kilichowapa Raia wengi fursa ya kushiriki kupiga kura. Vituo vilifunguliwa kwa wakati.
  • Wananchi wamepiga kura kwa amani na tunawapongeza Maafisa wa Tume ya Uchaguzi(IEBC) kwa kufanya kazi kwa Ueledi.
  • Tumefanya uangalizi katika jumla ya vitu 289 na tumeshuhudia hali ya utulivu.
  • Vyombo vya Habari vya hapa Kenya vimetoa taarifa kwa Ueledi na kufanya kazi kubwa sana.
  • Tunawaomba walioshindwa kuyakubali matokea au kufuata taratibu za kisheria katika kutatua malalamiko na changamoto zilizojitokeza.
> Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Afrika(AU) kupitia Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki wamesema Uchaguzi ulikuwa huru na haki na Uchaguzi umekidhi viwango vya kimataifa.
  • Thambo Mbeki: Sisi ni waangalizi na si Wachunguzi tumekutana na NASA wametupa taarifa ya udukuzi ktk mfumo wa matokeo wa IEBC.
  • Thambo Mbeki: Lakini tunawaomba NASA na Jubilee waipe muda Tume ya Uchaguzi(IEBC) kukamilisha kujumlisha matokeo yote.
> Waangalizi kutoka Jumuiya ya Madola(Common Wealth): Waliojitokeza kupiga kura ni wengi na walikuwa huru. Tume ya Uchaguzi inapaswa kupongezwa.

> Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Jumuiya ya Ulaya wazitaja kasoro kadhaa zilizojitokeza ikiwepo vitisho kwa wagombea Wanawake.
  • Marietje Schaake(EU): Kulikuwa na muda mchache wa kufanya maandalizi ya Uchaguzi kutokana na changamoto za kisheria.
  • Marietje Schaake(EU): Tume imeonesha nia thabiti ya kuendesha uchaguzi kwa uwazi kwa kuweka fomu za matokeo mtandaoni.
  • Marietje Schaake(EU): Wakati wa kampeni matusi na lugha za chuki na zile zenye utata zilitamalaki kwa Wagombea na wafuasi.
  • Marietje Schaake(EU): Tumebaini kuwepo kwa kutokuaminiana na kutoamini Mamlaka za Uchaguzi. Pia tunalaani kifo cha Msando.
  • Marietje Schaake(EU): Tunasisitiza uchunguzi juu ya mateso na kifo chake vifanyike.
  • Marietje Schaake(EU): Kuna matatizo ya Usalama na kutokuwepo kwa kumbukumbu za kutosha za kuwatambua wapiga kura.
  • Marietje Schaake(EU): Baada ya Uchaguzi huu uliokuwa na ushindani Viongozi wanapaswa kuwarudisha Wananchi kuwa kitu kimoja.
  • Marietje Schaake(EU): Demokrasia ni zaidi ya Mtu mmoja kura moja.
2: 30 PM
> LUHAMBI: Jeshi la Polisi linamsaka Msimamizi wa Kituo cha Uchaguzi aliyetokomea bila ya kukabidhi masanduku ya kura.

> Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (IEBC), Wafula Chebukati asema walipendekeza Watu wapakue Fomu 34A kutoka katika tovuti.
  • Wafula Chebukati: Kutoka siku ya jana hadi leo Fomu 34A zipatazo laki tatu(300,000) zimepakuliwa.
  • Wafula Chebukati: Tumepokea Fomu 29,000 za 34A na 117 za 34B kutoka maeneo mbalimbali. Tumezipokea pongezi za Waangalizi.
  • Wafula Chebukati: Kulikuwa na majaribio ya Kudukua mfumo wa matokeo lakini majaribio hayo hayakufanikiwa.
  • Tume ya Uchaguzi(IEBC) imesema kuwa matokeo ya Mshindi wa kiti cha Urais yatatangazwa siku ya kesho(Ijumaa) jioni.
  • Tume itakamilisha zoezi la kuhesabu kura za majimbo yote 290 ifikapo kesho. Mpaka sasa bado vituo 1,032 havijawasilisha matokeo.
4:30 PM
> Mmoja ya Viongozi wa Muungano wa Upinzani(NASA) Musalia Mudavadi: asema wameiandikia barua ya malalamiko Tume ya Uchaguzi.
  • Musalia Mudavidi : Tunaitaka Tume ya Uchaguzi(IEBC) iwatangaze Raila Odinga na Kalonzo Musyoka kuwa washindi katika uchaguzi.
  • Musalia Mudavadi: Tunataka Raila Odinga atangazwe kuwa mshindi na Kalonzo Musyoka kuwa Makamu wa Rais.
  • NASA, tunauhakika kutoka katika chanzo chetu cha uhakika Raila Odinga amepata kura Milioni 8.4 na Uhuru Kenyatta kura Milioni 7.75.

FUATILIA HAPA MATOKEO YA UCHAGUZI

RESULTS
 
UPDATES katika PICHA, VIDEOS na AUDIO:

f49ca0a2803050b6fc88f67719cbcd0f.jpg

Mandera east OCPD Ezekiel Singoe casts his vote at Mandera DEB Primary School

07d718a5deb64b733bbf406c40be7747.jpg

Gatundu South MP, Moses Kuria marked his secret ballot at Wamwangi Primary School at 6am.

1e9400155567a5ba3edf5615d9e31703.jpg

Wapiga kura wakiwa katika kituo cha shule ya msingi Westlands mapema leo

e7b79bcc50cfe3ae9e492bf461f87e18.jpg

Long queues as voters brave the morning chill at Ruthimitu mixed Secondary School to vote.

c4d1f04834d7d7d5448ba3eaad63f520.jpg

Chief Justice(CJ) David Maraga and his wife Eucabeth Moraa leaving Bosose polling centre in West Mugirango constituency after casting their votes

a484823c701e0cc960712e3b4fea480d.jpg

Hali ilivyo huko Turbo, Kaunti ya Uasin Gishu

02fbad3534fd9a99b1c69bad50142dc8.jpg

Mgombea wa Ubunge ktk Jimbo la Starehe, Boniface Mwangi akipiga kura huku akiambatana na familia yake(Mke na Watoto)

9988154377ab6db56ac28dab7be68a2a.jpg

Gavana Wycliffe Oparanya amepiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi ya Mabole, Butere na kuwataka Wakenya kufanya uamuzi wa busara

268fcfa3fba8125a520723daf52d81db.jpg

Waziri wa Kilimo katika Kaunti ya Meru, Genaro Gatangugi na Mbae Kiugo wameshambuliwa na wananchi waliowafumania wakinunua vitambulisho eneo la Imenti Kusini

bb89e5be279adbeb533ab88c241c680e.jpg

DP William Ruto queues to vote at Kosachei Primary polling station, Turbo.

cbeae171b45eb42dbaf852fafd7b1002.jpg

Deputy President William Ruto casts his vote at Kosachei Primary School in Turbo Constituency, Uasin Gishu

60397a9bbf0c089c4b9bf9433ecca1a1.jpg

Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa katika shule ya Rwathe iliyopo Kaunti ya Murang'a katika eneo la Bunge la Kandara.

cc43f794627382c2da81338d6bbf122d.jpg

Mgombea Urais kwa tiketi ya Jubilee, Uhuru Kenyatta amepiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Mutomo, Gatundu Kusini

44df43c5785c8bcf2a7979c75052bbef.jpg

Mgombea Urais, Raila Odinga(NASA) ameweza kupiga Kura katika kituo cha shule ya msingi Kibera

WhatsApp Image 2017-08-08 at 12.55.27 PM.jpeg

Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Juja, Francis Waititu akipiga kura huku akiwa amepiga magoti.

WhatsApp Image 2017-08-08 at 1.01.46 PM.jpeg


Mgombea wa kiti cha Ugavana wa Jiji la Nairobi, Mike Sonko akipiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi ya Bidii.

73a4b0f9-ce34-484d-bd2c-d997483d5663.jpg


=======
4:00 PM Updates

Vikongwe mbalimbali waliojitokeza kushiriki zoezi la kuchagua viongozi mbalimbali katika uchaguzi Mkuu nchini humo mapema leo.

Wengi walikuwa wakisaidiwa na Watoto na Wajukuu wao.

b057ac38-c904-4a42-91b2-c32b7146c850.jpg

2a7a9313-7efc-4ad7-891a-44c98cbbf420.jpg

cbd09d1a-5243-4072-b116-979ced632d2d.jpg

df3b608f-5569-4962-b9da-c6f22345b846.jpg

Katika vituo vipatavyo 40,883 vya kupigia kura, vituo sita vilikuwa na mpiga kura mmoja aliyeandikishwa.

c2854518-8c73-436a-a147-7e7ecbd72714.jpg
 
Dadeki, saa kumi na mbili na dakika thelathini na tatu ndo nimepiga kura yangu! Son of the soil, nimeshatimiza wajibu wangu kwa nchi yangu, shukran zote ni kwa Maulana!

Hongera tume ya uchaguzi na mipaka IEBC mmejipanga vyema sana! Diwani wangu Ustadh Kanchory mwenyewe, tumepatana nikitoka akanisalimia na kupiga bonge la smile, aisee ni kama ameshinda Sportpesa vile! Anajua nishampa zake tano tena!

Jubilee hoyee!
 
Back
Top Bottom