Excel kupanga matokeo, divisions na points

Screenshot_2017-01-02-22-21-44.png
Samahani, kuna mahali nimeona nimeongeza mabano hapo.
Hivi =SUM(SMALL(E28:M28,{1,2,3,4,5,6,7})) ingetosha. Haya mabano ya mwisho yanafunga yote yaliyokua yamefunguliwa mwanzoni.
Nimesikia kuwa kwenye version nyingine za excell, pengine chini ya office 2007 "{ } haikubali, sijajaribu maana sina 2003 na chini yake.
Lakini kwa urahisi kabisa inaweza pia kuandikwa kama hivi. =SMALL(E28:M28,1)+SMALL(E28:M28,2)+SMALL(E28:M28,3)+SMALL(E28:M28,4)+SMALL(E28:M28,5)+SMALL(E28:M28,6)+SMALL(E28:M28,7) inakuja pia

View attachment 453378

Manake ni namba ndogo kabisa iliyo kati ya E28 na M28, jumlisha namba ya pili kwa udogo katika mstari huo huo wa E28:M28, jumlisha namba ya tatu kwa udogo etc hadi 7
View attachment 453381
Hii formula nyingine ni ya kufupisha tu lakini kama inazingua afadhali kupitia parefu.
Mkuu nashukuru sna nimefanya nimefanikiwa nikitumia Point,Ila nikibadiri kuwa Grades mfano A,B,C.. inakuja hivi tatizo ni nini hapa mkuu?
Screenshot_2017-01-02-23-01-59.png
 
Kupanga division huwa yanachukuliwa masomo 7 ambayo mwanafunzi anakua amefualul vizuri zaidi. Somo ambalo mwanafunzi amefaulu zaidi linapoints chache zaidi, kuliko lile alilofeli. Hapa tunatumia Table C. Tunacho hitaji ni masomo 7 yenye points chache zaidi. Hivyo katika masomo 9 tutatafuta 7 yenye points chache zaidi kuliko mengine.
Njia ya kufikia hiyo ni kwa kutumia function ya "Sum" pamoja na function ya "Small"

SUM (kutafuta jumla)
Mara nyingi tumezoea kuandika function ya sum ikiwa na range (mipaka) ya cells (viboksi) tunavyotaka. Kwa mfano "=SUM(E28:M28)" ambavyo cells zilizo kati ya E28 na M28. Lakini vipengele vya sum pia vinaweza kuandikwa kimoja kimoja vikitenganishwa kwa mikato. Kwa mfano "=SUM(E28,F28,G28,H28,I28,K28,J28,L28,M28,)"

View attachment 452874
Nimefanya hivi ili tuelewe kwamba vipengele vya sum vinavyotenganishwa kwa mikato, vinaweza kuwa function nyingine. Na hii function nyingine kwa case yetu ni "SMALL"

SMALL (Ndogo)
Function hii ina vipengele viwili, ambavyo vinatenganishwa kwa mkato vikiwa ndani ya mabano. Vipengele hivi ni Array (Mipaka), ni katika eneo gani unatafuta ndogo. Kipengele cha pili ni " Ndogo ya ngapi" Ndogo ya kwanza (1), ni ndogo kuliko zote, Ndogo ya pili (2) ni kubwa kuliko ndogo ya kwanza nk. Kwahiyo kwa mfano function "=SMALL(E28:M28,3)" itanipa jibu 3. Kwamba ni thamani iliyo ndogo ya tatu kwenye table yetu.

View attachment 452872

SUM na SMALL
Function ya "Small" inaweza kubebwa ndani ya function ya "Sum"
Angalia kwa makini

View attachment 452864

Ni ndefu sana. Lakini inaweza kuandikwa kwa kufupisha kama namna hii
=SUM(SMALL(E28:M28,({1,2,3,4,5,6,7}))).

View attachment 452871
Utapata kitu kile kile. Ni mambo mengine ya Excel. Kwamba kwa namna flan ({1,2,3,4,5,6,7}) kipande hicho kinachezesha function zote mbili.
Drag chini kupata nyingine zote.

View attachment 452876

Utakua umepata jumla ya points.
Tengeneza table ya refferences za division (Tuiite table D) na utumie utaratibu wa "Vlookup" tulivyojifunza awali, kutengeneza divisions.

View attachment 452868
Kumbuka kwamba jumla ya points ndio inakua kipengele cha kwanza cha function ya vlookup, na range hapo ni ya table yetu mpya table D.

View attachment 452883

Kwa bahati mbaya inaonekana wanafunzi wangu watakua wanalingana sana.

Kuna changamoto kwamba table inapokua na points ndio unaweza kukokotoa jumla ya points (kwa sum&small) na dividions (kwa vlookup), lakini mwishoni unataka uwe na Alama, kama vile A, B nk badala ya points kwenye table yako.

View attachment 452888

Tumia utaratibu wa ku-copy columns za Points na divisions na kuzi-paste-values palepale ili kuondoa formulas ili columns hizo zibaki bila kubadilika. Kisha pale ilipokua 3 na kuifanya kuwa 2 kwenye function ya vlookup kama nilivyoonyesha juu. Badili cell ya kwanza juu kushoto kisha drag kulia na chini kusudi sasa ziwe alama A, B nk.
Wadau naomba kama mna chochote cha kurekebisha, kurahisisha, tusaidiane tutajirishane.

Hiki kipengere kimenivuruga mkuu cha ku copy columns za points na divison nazi copy alafu nazi paste wapi maana hpa ni kweli nikibadiri huu mfumo wa point kuja katika Alama katika columnsv za Points na divison zinajivuga na kuja maneno ya ajabu
 
Saaafi sana. Kwa kweli umekwenda vizuri sana. Kimsingi umesha maliza.
Ndio, hii ya mwisho ni changamoto, kwamba Points (1,2,3, etc) ndio zinazo kokotolewa na kuleta jumla ya points (18) na division (II). Sehemu zote hizo zinakua zimeunganika kimahesabu, hivyo unapobadili sehemu moja, kwa mfano ukiweka sasa alama (A,B,C etc), inaleta jambo hilo la ([HASHTAG]#NUM[/HASHTAG]!).
Kinachofanyika hapo, ni kuachanisha column hizo za Points na division kutoka katika utaratibu mzima. Hiyo inakupa sasa uhuru wa Kubadili sehemu ya nyuma kutoka katika utaratibu wa (1,2,3 nk) kwenda katika utaratibu wa (A,B,C nk)
Ukiclick cell ya division au ya points utaona inaonekana ina function badala ya namba.
upload_2017-1-3_10-22-21.png

Hii inatakiwa iondoke.

Inafanyikaje.
1. Select column zote mbili za Points na Division.
select kutoka juu, ili kama una wanafunzi 500 uwe ume-select wote
upload_2017-1-3_10-23-48.png

2. Right click selection kisha Copy
4. Ikiwa hivyo hivyo right-click tena
paste special
upload_2017-1-3_10-30-19.png

paste values

upload_2017-1-3_10-32-49.png

Sasa uki-click tena cell utaona values sio formula. Manake umezi-disconnect.

upload_2017-1-3_10-34-40.png

Sasa endelea, badili za ndani kuwa (A,B,C etc) bila kuathiri points na division.

Hii ni njia ya kwanza na ni ya kienyeji kidogo. Ubaya wake ni kwamba, labda unahitaji kubadilisha marks ya mwanafunzi, haitaleta mabadiliko kwenye points na divisions maana umesha ziachanisha. Ipo njia nyingine ambayo, unaweza kuzifanya bado ziwe zimeunganika zote. Na njia hiyo ni kwa kuvitenganisha vipengele na kuviunga kwa njia ambayo ukibadili marks za mwanafunzi zinabadili pia points na division. Ngoja nitayarishe maelezo yake nita-attach pia na excel.
 
Njia ya pili na ambayo itabadilisha points na division ukibadili marks za mwanafunzi.
Sasa kwanza download excel yangu hapo inayoitwa "Mfano Marks" halafu tuelekezane. (Kwa bahati mbaya office yangu ni 2007, pengine tunaweza kupishana kama una version ya mbele).
Utaona ina tabs tatu (Original, Points na Final) Kwenye excel tabs zinaweza kuongezwa na kupewa majina.
upload_2017-1-3_11-57-25.png

1. Kwenye Tab ya kwanza, utaona nimeweka table original zenye marks za wanafunzi, pamoja na vi-refference table viwili. Kimoja cha points na kingine cha divisions.
(By the way :- Unaweza pia kuweka kila kitu kwenye tab moja ila kazi itakua pana sana, kama unajua mbinu za kuhide cells inakua vizuri pia)
2. Kwenye tab ya Pili nimetengeneza Table ya vlookup.
Nimefanyaje.
Kwanza nikiwa hapo kwenye "tab" ya "points", nimeclick cell ya kwanza kabisa ambayo ni A1. Nikaweka alama ya swasawa "=". Nikaenda kwenye tab ya Original, nikaclick cell ya A1 ambayo ni "Student name" kisha nika bonyeza enter, Student name ikaja kwenye A1 ya tab ya Points. Nika click cell hiyo na kuivuta kwa kikona kwenda pembeni hadi mwisho. kama 0 zikitokea umepitiliza, zifute.
upload_2017-1-3_11-59-52.png

Kisha nika-select Student name na Sex hapohapo, nikazivuta kwenda chini kwa mtindo huo huo.
upload_2017-1-3_12-1-16.png

Nikaenda kiboksi cha kwanza juu kushoto C2 kenye tab hiyo hiyo ya Points, nika-click na nikaanza kuandika formula yangu ya vlookup.
Nikaandika hivi
=vlookup( kisha nikaclick tab ya original, halafu nikaclick C2 pale original, nikabonyeza mkato (coma). Baada ya hapo natakiwa niweke table array, nikaselect table B yote isipokua heading yake, kisha nikaboyeza F4 kuweka alama ya Dollar, nikabonyeza mkato tena, halafu nikaandika 3 kwamba ninachotakiwa kupata hapo ni points column ya tatu, mkato tena, halafu nikaandika true Nikafunga mabano. nikapress enter. Kwenye kiboksi C2 kwenye tab ya points ikaja point. Nikaiselect kisha nikaidrag kushoto kisha chini kama kawaida kujaza viboksi vya points vilivyo baki.
Kisha hapo hapo kwenye tab ya points nikaongeza column za columns za Points na divisions
3.Kwenye divisions nikatumia utaratibu wa Sum na small kama maelekezo awali.

4. Kwenye division nikaandika vlookup namna hii
Kwanza nikaclick kiboksi cha kwanza ambacho ni M2, kisha nikaandika =vlookup( kisha nikaclick kiboksi cha nyuma yake ni L2, nikabonyeza mkato, kisha nikaclick tab ya original, nikaselect table C yote isipokua heading, kisha nikabonyeza F4 kuweka alama za dola, kisha nikaweka mkato tena, nikaandika 2 kisha mkato, nikaandika true kisha, nikafunga mabano, kisha nikabonyeza enter. Division ikaja kwenye kiboksi cha M2 kwenye tab ya points. Nikaishika kwa kona nikaidrag chini kama kawaida kujaza viboksi vyote.

5. Kwenye tab ya final cell A1, nikaweka alama ya "=" Kisha nika-click tab ya points, na pale nikaclick cell ya kwanza yaani A1, nikabonyeza enter, Student name ikaja kwenye cell ya A1 kwenye tab ya final. Nikadrag kushoto, kujaza, kisha nika select student name na Sex, nikadrag chini kama nilivyo fanya awali kwenye tab ya points.
Nikaenda kwenye tab ya points tena. nikaclick cell ya somo ya kwanza juu kushoto, yaani C2. Nika-right click kisha nika-copy. Nikaenda kwenye tab ya final kwenye C2 nika-paste. Ikaja function ya vlookup niliyotumia kwenye tab ya points. Nikaenda kwenye kipengele cha 3 cha function hiyo ya vlookup, nikabadili 3 kuwa 2, kisha nikabonyeza enter. Kwenye kiboksi cha C2 kwenye tab ya final ikaja "A" ambayo ni mark ya mwanafunzi Chungwa Tamu katika somo la Biology.
upload_2017-1-3_12-9-8.png

Nika drag kushoto kisha chini kama kawaida kujaza viboksi vyote

6. Kwenye kiboksi cha L2 kwenye tab ya final, ambacho ni points za mwanafunzi Chungwa, nikaweka alama ya sawasawa "=" , kisha nika-click tab ya points nikaclick pale kiboksi L2, kisha enter. Points za mwanafunzi chungwa zikatokea pia kwenye kiboksi cha L2 kwenye tab ya final. Nikadrag kushoto hadi usawa wa division, kisha nikadrag zote chini hadi mwisho kujaza points na division kwenye tab ya final. Kitu kikawa kimetokea na mabadiliko yoyote ya marks yatakayo fanyika kwenye tab ya original tatatokea kila mahali.
upload_2017-1-3_12-11-28.png

Ndefu sana, lakini jaribu kuielewa. Usisahau kudownload excel yenyewe
 
Mkuu nmepiga kazi nimekwama kwenye division yan sijakupata hapo kwenye vlookup ya mwisho ili nipate división, nmejaribu inaniletea wanafunzi wote wamepata zero
 
Mkuu nmepiga kazi nimekwama kwenye division yan sijakupata hapo kwenye vlookup ya mwisho ili nipate división, nmejaribu inaniletea wanafunzi wote wamepata zero

Vlookup imegawanyika katika sehemu nne, kama unavyoona hapo
sehemu zimegawanywa kwa mikato
upload_2017-1-4_9-0-19.png

Vlookup kwenye upande wa division inakwenda namna hii:-
Kwenye namba moja ya function ni cell ile yenye jumla ya points ulizopata baada ya kukokotoa sum na small jumla points za mwanafunzi.
Kwenye namba mbili, weka cells range ya kale katable kanakoonyesha utaratibu wa divisions, kwamba division one inaanzia kwenye ngapi, division two inaanzia kwenye ngapi nk.
Kwenye namba tatu, weka 2, pengine hapa ndipo unapokosea labda unaweka 3. Weka 2 kwasababu katable kale ka utaratibu wa divisions kana columns 2 tu. Ukiweka 3 columna ya 3 haina kitu ndio maana pengine inakuletea zero.
Kwenye namba nne weka true, kwasababu ni relative, inayo karibiana.
Pia usisahau kudownload excel yangu na kuangalia nilivyo fanya. Click hapa kudownload excel ni ya mwaka 2007
 
Vlookup imegawanyika katika sehemu nne, kama unavyoona hapo
sehemu zimegawanywa kwa mikato
View attachment 454093

Vlookup kwenye upande wa division inakwenda namna hii:-
Kwenye namba moja ya function ni cell ile yenye jumla ya points ulizopata baada ya kukokotoa sum na small jumla points za mwanafunzi.
Kwenye namba mbili, weka cells range ya kale katable kanakoonyesha utaratibu wa divisions, kwamba division one inaanzia kwenye ngapi, division two inaanzia kwenye ngapi nk.
Kwenye namba tatu, weka 2, pengine hapa ndipo unapokosea labda unaweka 3. Weka 2 kwasababu katable kale ka utaratibu wa divisions kana columns 2 tu. Ukiweka 3 columna ya 3 haina kitu ndio maana pengine inakuletea zero.
Kwenye namba nne weka true, kwasababu ni relative, inayo karibiana.
Pia usisahau kudownload excel yangu na kuangalia nilivyo fanya. Click hapa kudownload excel ni ya mwaka 2007
Mkuu mungu akubarik kazi nimekamilisha vizuri na sio ngumu kama nilivyokua nazani
 
Sijaelewa kwa kweli (Kiswahili kigumu!!) yaani hapo labda ungetumia lugha ya Malikia Elizabeth ndio ningelikuelewa!
 
Mimi nafanya sales,nina routes 5 na product 10 of different size (liter) nahitaji kuwa na template ambayo nikiingiza mauzo ya siku ya kila route na kila product na ujazo wake inipatie volume ya siku,wiki na mwezi kwa route,product,volume.
Naomba kueleweshwa tafadhali mkuu.
 
Watu wengi wamekua wakiuliza swali hili, hasa wale wanaofanya kazi kama waalimu, ambao wanatakiwa kuwa-grade wanafunzi kulingana na matokeo ya mitihani kwa kutumia Microsoft excel.
Nimeona watu wengi wametoa maelekezo kwa kutumia function ya "If" na ndiyo niliyokua naijaribu katika kutatua tatizo hilo lakini baadae nimeona ni ndefu sana, na mahali fulani unaweza kujivuruga wakati wa kupanga mambo. Kwa mfano nilikua naangalia maelekezo ya Kyatsvapi akiwa anajibu swali hilo. Ni njia nzuri na ndiyo niliyokua natumia kwa muda mrefu.

Lakini nilikua nafikiria Kutumia function ya "Vlookup" kupanga points na baadae kutumia function ya "sum" pamoja na ya "small" Kupata divisions.
SASA TWENDE HATUA KWA HATUA.
Kwanza, nina wanafunzi wangu
View attachment 452183
Na hizo ndo marks zao.
Pili
Mahali fulani kwenye excel yangu natengeneza refference table yangu
View attachment 452185
Column ya kwanza ni Marks ya pili kama unavoona ni kwamba mark inaangukia kwenye A au B,C nk ya tatu ni points husika.
Tatu
Naenda kwenye cell ambayo nitacopy table ya matokeo na badala ya marks table itaniletea sasa Points kwa kila somo lililo kwenye table ya matokeo.
Namna rahisi ni kwa kutumia alama "=" Naiweka mahali ninapo taka table yangu itokekee,
kisha naclick cell ya juu kushoto ya table yangu
View attachment 452193

kisha enter
cell niliyochagua itajirudia kwenye point niliyo chagua
Kisha na-drag kwenda kulia kwa kushika dot ya chini ya cell
View attachment 452195
Mpaka row yote itokee namna hii
View attachment 452197
halafu naselect tena cell mbili za kushoto kabisa, maana column ya sex itajirudia
Nashika dot kwenye kona ya cells hizo na kudrag chini
View attachment 452200
Hadi cell za kwenda chini zitokee
View attachment 452201
Table yangu ipo tayari kwa kujaza points
View attachment 452203
Hapa ndio tunaanza kuweka mambo ya "Vlookup" na tunaanza na cell yenye marks za Biology za mwanafunzi Chungwa Tamu. pale andika alama ya sawasawa, kisha vlookup kisha fungua mabano =vlookup(

View attachment 452206

Kisha click Marks za biology za Chungwa Tamu kwenye ile table yenye marks
View attachment 452208

bonyeza mkato , Kisha select ile table ya refference yote
View attachment 452211
Bonyeza F4 ili alama za dolar zitokee kwenye hiyo refference, au table array

View attachment 452212
Bonyeza mkato tena tayari kwa kuweka return value ya table ya refference, ambayo ni column ya value unayotaka irudi. Ka case yetu ni column ya tatu

View attachment 452220

Kwa hiyo baada ya mkato tunaweka 3
Mkato tena, sasa hapo kuna true na false. True kama ni approximate match, au False kama ni exact match. Lakini kwasababu kenye refference table yetu kutoka 0 hadi 30 kuna namba katikati na zinatakiwa zikadiriwe kuwa ni poit 5 au 4 kwahiyo jibu letu ni True approximate.
Sasa kitu chetu kitaonekana hivi
View attachment 452222

Hapo gonga enter. Na utaona 1 inatokea ikimaanisha 89 ambayo ni marks ya Chungwa tamu katika Biology, ikipimwa na table yetu inakua ni point 1.
Sasa shika tena kona ya cell hiyo na uivute hadi mwisho
View attachment 452224

Kisha ushike tena kona hiyo uivute hadi chini
View attachment 452225

Na kila kitu kitakua kimejaa kwa mwendo wa point.

Wamenikataza nisiongeze picha. Naomba niishie hapa kwanza. Halafu nitaendeleza kwa mwendo sasa wa division na kumalizia kila kitu. Kimsingi maelezo ni mengi sana, lakini unapokuja kwenye uhalisia na kuelewa itakua ni kitu cha dakika chache tu. Pia kuna mambo ya kurahisisha, kwa mfano baada ya kudrag kwa kukatisha, unapotaka kujaza kwa kwenda chini select viboksi vitupu vya chini kisha bonyeza control na D.
Nitaendelea. Baadae nitaleta sample na utaona ni rahisi sana.
Hiyo iko poa! Ila bado ni manual work mimi nina mfumo (full automatic) kwa ajili ya management ya shule nzima kuanzia udahili kuchakata matokeo (mzazi au mlezi anaweza kuona matokea hayo) , tarifa za walimu (hr na finance ) makusanyo ya ada na n.k kwa maelezo zaidi anayetaka anione pm
 
Kupanga division huwa yanachukuliwa masomo 7 ambayo mwanafunzi anakua amefualul vizuri zaidi. Somo ambalo mwanafunzi amefaulu zaidi linapoints chache zaidi, kuliko lile alilofeli. Hapa tunatumia Table C. Tunacho hitaji ni masomo 7 yenye points chache zaidi. Hivyo katika masomo 9 tutatafuta 7 yenye points chache zaidi kuliko mengine.
Njia ya kufikia hiyo ni kwa kutumia function ya "Sum" pamoja na function ya "Small"

SUM (kutafuta jumla)
Mara nyingi tumezoea kuandika function ya sum ikiwa na range (mipaka) ya cells (viboksi) tunavyotaka. Kwa mfano "=SUM(E28:M28)" ambavyo cells zilizo kati ya E28 na M28. Lakini vipengele vya sum pia vinaweza kuandikwa kimoja kimoja vikitenganishwa kwa mikato. Kwa mfano "=SUM(E28,F28,G28,H28,I28,K28,J28,L28,M28,)"

View attachment 452874
Nimefanya hivi ili tuelewe kwamba vipengele vya sum vinavyotenganishwa kwa mikato, vinaweza kuwa function nyingine. Na hii function nyingine kwa case yetu ni "SMALL"

SMALL (Ndogo)
Function hii ina vipengele viwili, ambavyo vinatenganishwa kwa mkato vikiwa ndani ya mabano. Vipengele hivi ni Array (Mipaka), ni katika eneo gani unatafuta ndogo. Kipengele cha pili ni " Ndogo ya ngapi" Ndogo ya kwanza (1), ni ndogo kuliko zote, Ndogo ya pili (2) ni kubwa kuliko ndogo ya kwanza nk. Kwahiyo kwa mfano function "=SMALL(E28:M28,3)" itanipa jibu 3. Kwamba ni thamani iliyo ndogo ya tatu kwenye table yetu.

View attachment 452872

SUM na SMALL
Function ya "Small" inaweza kubebwa ndani ya function ya "Sum"
Angalia kwa makini

View attachment 452864

Ni ndefu sana. Lakini inaweza kuandikwa kwa kufupisha kama namna hii
=SUM(SMALL(E28:M28,({1,2,3,4,5,6,7}))).

View attachment 452871
Utapata kitu kile kile. Ni mambo mengine ya Excel. Kwamba kwa namna flan ({1,2,3,4,5,6,7}) kipande hicho kinachezesha function zote mbili.
Drag chini kupata nyingine zote.

View attachment 452876

Utakua umepata jumla ya points.
Tengeneza table ya refferences za division (Tuiite table D) na utumie utaratibu wa "Vlookup" tulivyojifunza awali, kutengeneza divisions.

View attachment 452868
Kumbuka kwamba jumla ya points ndio inakua kipengele cha kwanza cha function ya vlookup, na range hapo ni ya table yetu mpya table D.

View attachment 452883

Kwa bahati mbaya inaonekana wanafunzi wangu watakua wanalingana sana.

Kuna changamoto kwamba table inapokua na points ndio unaweza kukokotoa jumla ya points (kwa sum&small) na dividions (kwa vlookup), lakini mwishoni unataka uwe na Alama, kama vile A, B nk badala ya points kwenye table yako.

View attachment 452888

Tumia utaratibu wa ku-copy columns za Points na divisions na kuzi-paste-values palepale ili kuondoa formulas ili columns hizo zibaki bila kubadilika. Kisha pale ilipokua 3 na kuifanya kuwa 2 kwenye function ya vlookup kama nilivyoonyesha juu. Badili cell ya kwanza juu kushoto kisha drag kulia na chini kusudi sasa ziwe alama A, B nk.
Wadau naomba kama mna chochote cha kurekebisha, kurahisisha, tusaidiane tutajirishane.
Hayo mabano kama ya kwenye set katika formula ya sum(small(1,2,3,4,5,6,7)). Nayapata wapi mkuu.
 
Nashukuru kwa darasa ulilotoa. Binafsi nilikuwa natumia zaidi IF function kwenye kazi za hivyo ila nitajaribu hiyo function ya vlook
 
Back
Top Bottom