Ex wangu kaniepusha na ajali ya kuangukiwa na ghorofa Kariakoo

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
May 3, 2022
6,156
10,950
Nilitakiwa kuweka bandiko hili siku ya tukio. Ni vile tu nilipatwa na kihoma cha mfadhaiko na mshangao wa hali ya juu kilichopelekea kumtafakari zaidi Israel na kujisahau kuingia JF kwa Baba yetu mpendwa, Mh. Maxence Melo

Wiki moja kabla ya tukio niliachana na Deborah, hii ni baada ya kichapo kikali tulichotembezeana katika mabishano ya kuondoa password kwenye simu yangu, hii ilikuwa baada ya kupatiwa taarifa na rafiki yake kuwa ninatoka na mdogo wake, na eti kuna video iko kwa simu yangu ambayo tulijirekodi. Baada ya Deborah kuipasua simu yangu ukutani nilifula sana, japokuwa mtanange ule ulikuwa ni wa 1:1 nilijikuta nimejaa hasira sana, nikamkwida kabali moja takatifu na kummalizia kichwa cha pua kilichompelekea kutokwa na mafua mekundu ya lasha lasha, na mahusiano yetu yakafia hapo

Siku moja kabla ya tukio, mida ya saa 4 usiku, niliingiza kibinti cha 2000 magetoni nikiwa nimetoka nacho maeneo ya Argentina Manzese. Kile kibinti kikanipikia na kunipatia mzigo. Kama mjuavyo binadamu hawana jema, habari zikawa zimemfikia Deborah. Siku ya tukio asubuhi nikiwa ndani ya mjengo Kariakoo, floor ya kwanza nikiwa namngoja jamaa mmoja hivi muuza nguo za kike afungue ili nichukue magauni fulani hivi ya watoto kwa bei ya jumla ili nikayaweke kwenye fremu yangu na mdogo wangu pale Ilala Boma (Saa 2 Kasoro), simu ikaita. Ile kucheki ni Deborah, akaniambia njoo hapa kwako, nimekuja kuchukua vyombo vyangu na kisimbuzi cha Azam nilichonunua. Sijakaa sawa jirani anatuma sms kwamba huku watu wanatoana damu, eti yule binti uliyekuja naye jana kararuriwa ile mbaya. Muda huo huo nikaamua kutoka nje ya mjengo ule, kuna mdada alikuwa anafagia koridoni nilimpamia, alinitukana sana kumbe yalikuwa ni matukano yake ya mwisho maskini! Nikakimbilia kituo cha mwendokasi Msimbazi, ile niko njiani nikaskia watu wanazungumza ghorofa kudondoka, sikutia maanani maake nilijua ni uko Gaza

Kufupisha habari, asubuhi ya leo nimetoka kula kiboga cha Deborah!
Kaniokoa dhidi ya kifo!
downloadfile.jpg
 
Kaniokoa dhidi ya kifo!View attachment 3156178
Mkuu kwenda ilala boma ulitumia mwendo kasi
 
Back
Top Bottom