Shing Yui
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 16,229
- 41,857
Mwanaume, unaponunua ngo'mbe kamwe usinunue kwenye eneo au kijiji ulichopo.
Kwanini?! Kwa sababu kuna siku ng'ombe ataenda mtoni kwa lengo la kunywa maji.
Kisia nani atakuwa eneo hilo?! Ni mmiliki wake wa mwanzoni. Unajua atakachokifanya huyo mmiliki wake wa zamani?!
Atakachofanya ni kumpigia mluzi, na ng'ombe atatambua mluzi wa mmiliki wake wa zamani, atamfuata, ng'ombe atakapomfuata mmiliki wake wa zamani, kitakachofuata ni zoezi la kukamuliwa maziwa yote mazuri.
Baada ya hapo mmiliki wa zamani atampapasa papasa ng'ombe juu ya mgongo na kumuacha aondoke kana kwamba hakuna lolote lililotokea.
Kisha wewe mmiliki mpya ukimuona ng'ombe karudi nyumbani. Utajawa furaha na kuchukua ndoo ndogo ukitaka umkamue maziwa fresh.
Lakini ng'ombe atakuwa mkali, atakupa Kung Fu kick moja takatifu. Huku akitoa mlio wa hasira. Sababu ng'ombe huwa hapendi utaratibu wa kukamuliwa maziwa yake mara kwa mara tena kwa siku nzima.
Mwanaume usinunue ngo'mbe eneo ulilopo. Huenda ngo'mbe akawa bado na mahusiano ya kihisia na mmiliki wake wa zamani wewe ukajikuta hunywi maziwa