mackj
Member
- Jul 25, 2023
- 84
- 97
Tanzania ni Miongoni mwa nchi ambazo zinavyuo na taasisi zilizo na wataalamu wazuri wa utayarishaji mifumo mbalimbali kwa njia ya tehama mfano tume ya sayansi na teknolojia COSTECH, vyuo km DIT, na mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA, vyote hivi kwa pamoja na wadau wa sayansi na teknolojia waliopo nchini siamini kama wameshindwa kuishauri serikali kuja na mabadiliko ya kutoka kwenye giza la kifikra linalotengenezwa kwa makusudi ili kuendelea kuwa na uatawala wa aina moja ambao umekuwa ukizua tafrani kila ifikapo nyakati za uchaguzi kutokana na wizi wa kura zinazopigwa kwa njia ya makaratasi (ballot papers)
Ambapo yamekuwepo maalalmiko ya wizi wa kura na kupelekea kupata viongozi ambao siyo chaguo la wananchi jambo ambalo wananchi wanaona nikama kuwafanya wajinga na wakati mwingine, wengine huenda mbali na kususia kupiga kura maana wanaona ni kama kupoteza muda ikiwa wanajua mshindi ni nani! hali hii huua demokrasia na kuminya haki ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa.
"Nini kifanyike?"
Kama nchi ni muda Muafaka tuseme “ballot papers basi" utengenezwe mfumo wa upigaji kura kwa njia ya kielektronik ambao utaondoa kura bandia, na wizi wa kura, mchezo ambao umekuwa ukilitafuna taifa na kuondoa umoja wa kitaifa kitu ambacho kinaweza siku moja kuliingiza taifa kwenye machafuko.
Mfumo huu unafanyikaje?
Picha (chanzo) india today
Mfumo huu ni rahisi kutengenezwa maana hata wenzetu Kenya wameweza kuutumia na ni mfumo unaoleta uwazi ikiwa mpiga kura atapiga kura, mfumo utatambua amepiga kura na hakuna haja ya kuchovya kidole katika wino maana atatumia kitambulisho chake alichokipata kwa njia ya bayometriki kwa kuscan QR CODE kwenye mashine maalum kisha mfumo kumtambua, na kisha kupiga kura.
Na iwapo atapiga kura tayari grafu itapanda katika mfumo wa asilimia kuonesha idadi ya waliokwisha piga kura kuongezeka, na upande ambao hawajapiga kura grafu ikishuka.
Hii mifumo itafungwa katika vituo vya kujumuishia matokeo ambapo mwananchi anakuwa na haki ya kwenda kuona mchakato unavyokwenda na kisha kuondoka, lakini katika vituo vya kupigia kura kunakuwa na mashine maalumu zinazokuwa na APP/system ya tume ya taifa ya uchaguzi ambazo zitakuwa zikitumika kupigia kura, na zitakuwa na majina ya vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi, picha na majina ya wagombea na nafasi wanazogombea ili kumrahisishia mpiga kura kujua na kutambua mgombea anaempenda.
"Kuhusu udhibiti wa mfumo kutoruhusu wizi ukoje?"
Kutakuwa na saver zitakazo kuwa zinaratibiwa na tume huru ya uchaguzi ambayo hii kwa mfumo wa nchi yetu ulivyo, ambapo Rais anamchagua mkurugenzi wa tume unaweza kuwa na ukakasi hivyo saver zitatofautishwa na base data ambapo base data zitakuwa na uratibu wa mawakala wa kitehama kutoka vyama vyote vya siasa ili kuondoa udukuzi wa majumuisho ya kura katika mchakato wote wa uchaguzi, kama ilivyo sasa mawakala wa vyama wanakuwa katika chumba cha kupigia kura kuratibu zoezi la upigaji kura na kutokuwepo michezo ya upigaji kura kwa kujirudia, ndivyo itakavyokuwa pia katika mfumo huu wa upigaji kura kitehama yaani Electronic Voting Mashine (EVM)
Picha (chanzo) india today
mpiga kura utatumika mfumo wa (OTP) kuratibu udanganyifu kwa hiyo akijaribu kutaka kufanya udanganyifu mashine zitamuumbua na kukamatwa kwani itabainika amekwishapiga kura
Ikumbukwe kuwa base data, au data base ndio inayotunza kumbukumbu za taarifa ya upigaji kura na haifunguliwi mpk pale mfumo wa uhesabuji kura utakapomalizika
Pia kutakuwa na screen maalumu zinazoonesha matokeo ambazo zinatatumia interface moja, kisha kama kuna malalamiko basi mawakala wale watakokuwa kwenye vituo na kwenye chumba cha base data za majimbo na taifa watalazimika kujiridhisha kupitia base data hizo ili kuona uwiano wa kura zilizotunzwa kwenye data base na zilizopigwa kwenye mfumo.
"Kwanini mfumo huu wa kisasa wa upigaji kura kwa njia ya kielektronik (EVM) unacheleweshwa?"
Huchelewa au unawekewa vizingiti kwakusingizia gharama zake za kuinstall ni kubwa, swali ni moja mbona mara nyingi tumeshuhudia serikali ikikopa mabilion ya fedha za kugharamia uchaguzi kwanini tusikope kununua vifaa hivi ambavyo vitatumika miaka yote kuliko kila siku kuomba pesa ya mzungu na kisha kufanya mabadilishano ya rasilimali zetu na fedha zake kwa vitisho, kwa kuwa mara nyingi fedha zile ndizo zinawaweka watawala madarakani!
Lakini, Ikiwa nguvu ya wanasiasa ikielekezwa kwenye kudai mfumo wa upigaji kura uwe kwa njia ya EVM, na kuilazimisha serikali kutengeneza mfumo huu malalamiko ya kila chaguzi yatokanayo na wizi na udanganyifu wa chaguzi yataisha tanzania, na matarajio ya watanzania ya kuwapata viongozi wanaowataka yatatimia na idadi ya ushiriki katika zoezi la upigaji kura itaongezeka mara dufu tofauti na miaka ya nyuma
"Je? project hii inachukua muda gani? na je upatikanaji wa vifaa vyake na hizo softwea zipo?"
Picha (chanzo) india today
Project hii inaweza kufanyika kwa muda wa miaka 3-mpaka 5 kwakuwa vifaa vipo vinauzwa na mifumo ipo ilikwisha tengenezwa softwhere developers, ni kuiboresha kutokana na mahitaji ya Tume, kisha kuifunga utajiuliza, ninani aliamini tungeanza kujiandikisha kwa mfumo wa bayometriki? Mbona iliwezekana? Ninani alijua tutalipa kodi kwa EFD? nani alijua mita za maji zitakuja za luku?
Mifumo ipo, teknolojia ipo, ila urasimu na ufisadi umekuwa ndio kikwazo cha mabadiliko kuendana na teknolojia na pia kwakuogopa kutoka madarakani, hali ambayo wanachi hukoswa imani na serikali yao mwishowe kuingia katika machafuko yatokanayo na uchaguzi
Aidha Tanzania tuitakayo dhamana yake iko mikononi mwa wanasiasa, hawa ndio wanaamua tanzania tuitakayo kwa kupigania kuwa na mfumo huu bora wa upigaji kura kwa kutumia teknolojia, siyo kulilia mabadiliko ya sheria za uchaguzi tu!kwani sheria zenyewe nazo zinapindishwa na walio na mamlaka ya kutafsiri sheria zenyewe maana wwenye nafasi za juu huteuliwa na Rais.
Unaweza kujiuliza je? Mifumo hii kule kijini ambako umeme haujafika watapataje haki ya kupiga kura?
Kwa jiografia ya tanzani na jinsi ambavyo serikali ya awamu ya tano ilipambana kusamabaza umeme vijijini utakuwa shahidi kuwa ni asilimia chache sana zimebaki kukamilisha mradi wa umeme katika vijiji vyote nchini tanzania na pia mashine hizi zinatumia solar na umeme, ni (multifunctional) hivyo hakuna changamoto itakayozuia uwepo wa haki ya kupiga kura kwa mfumo wa kielektronik (EVM)
Mtanzania mwenzangu lazima utambue kuwa hatima ya tanzania tuitakayo msingi wake ni siasa huwezi kuipata tanzani uitakayo kwa kuikwepa siasa maana huku ndiko kila kitu katika nyanja zote za maendeleo ya Taifa hili kinapoanzia
Asante