famicho
JF-Expert Member
- Jul 29, 2015
- 2,191
- 2,857
Well said mkuuRwanda ni marafiki wa mashaka,miaka michache iliyopita waliivamia Congo DR,na pia wanadaiwa kuhusika na mambo yaliyomkuta Baba yake na Joseph Kabila,tunajua Mobutu aliondolewa na majeshi ya waasi kwa kushirikiana na Rwanda na ndio maana baada ya kuondolewa kwa Mobutu,Mkuu wa kwanza wa jeshi la CongoDR alitoka Rwanda,Laurent Kabila alianza kutoelewana na Rwanda,Mkuu huyo wa majeshi alirudi na yaliyomkuta Laurent Kabla kila mtu anayajua.
Pia jeshi la Tanzania juzi juzi liliwafukuza M23 kutoka CongoDR,baada ya kufukuzwa,M23 walielekea Rwanda na Uganda na kupokelewa vizuri,jeshi letu bado liko CongoDR na kuna taarifa kwamba M23 wametoroka makambini na inasemekana wamerudi Congo,je kagame anajichekesha ili Tanzania ipotezee ukali na mafanikio yake iliyopata kuzima uasi na kuituliza Congo? Jeshi letu likiwachapa tena M23 bwana kagame atachukuliaje?na anatuchimba chimba kwa urafiki ili ajue nini? Kuhusu nini? Ni Tanzania tu ndio inaweza kuikemea Rwanda!
Nkurunzinza juzi juzi alinusurika mapinduzi akiwa anahudhuria mkutano hapa Tanzania na lawama anatupiwa Kagame,sasa Burundi hahudhurii mikutano ya jumuiya ya afrika mashariki inayofanyikia Rwanda ......tunaona Rwanda akijaribu kuweka utawala DRC,na juzi Burundi,
Rais kagame alikuwa mkuu wa ujasusi wa jeshi la Uganda kabla hajaandaa jeshi lake na kuivamia Rwanda na kusababisha mauaji,kwa kuwa yeye ni mtusi anasema mauaji hayo ya kimbari eti waliuwawa Watusi tu,wahutu hawakuuwawa,kama kagame aliingia na jeshi la Watusi dhidi ya wahutu,kwa nini upande mmoja wafe upande mwingine isemekane hawakuuwawa?....anyway,kagame alikuwa mkuu wa upelelezi wa jeshi la Uganda......kavamia na kupindua Rwanda....huyooo akachora Ramani kumuondoa Mobutu ili amuweke Laurent kabila,kamuweka,wakagombana,Kabila akauwawa,Mkuu wa jeshi la Mzee kabila alitoka Rwanda......juzi akataka kupachika utawala Burundi Tanzania ikamzuia,sasa kaanza kujifanya Rafiki wa Tanzania.
Wanyamulenge,kimsingi wanyamulenge ni wafugaji wa kitusi ambao walipandikizwa mashariki ya Congo kwa miaka mingi na kwa makusudi,wakajigeuza jeshi wakaanza uasi mashariki ya Congo.
Kuna madai kwamba Kagame anaitaka Congo ya Mashariki ili iwe taifa,yaani Congo imegwe wakae Watusi,kama israel ilivyoimega palestina ikaanzisha taifa lake,na uasi katika ukanda huo ni sehemu ya juhudi hizo.
Binafsi hata majadiliano ya Tanzania na wafadhili yaliyofanywa na Kaberuka,Mnyarwanda kwa niaba ya Tanzania sikufurahia
Miaka isiyizidi mitano wakati JK alipoanza operesheni kuwaondoa wahamiaji haramu,mmoja wa wakuu wa idara ya IT jeshini alikuwa Mnyarwanda na alipotea katika mazingira ya kutatanisha,labda alirudi kwao Rwanda ,bado hatujakaa sawa kaberuka anajadili mambo yetu na wafadhili,kuna madai kwamba watu wanaotumikia nchi zao nje ya mipaka ni majasusi,sasa sisi pengine tunafikiria kaberuka ni mchumi ni na mtaalamu,je kama ni mmoja wa majasusi wa Rwanda? Si anakuwa kajua mambo yetu mengi ya wizara ya fedha?
Juzi tu kagame alilaumiwa kwa kumuua Kalegeya huko afrika kusini akiwa hotelini,
Hivi karibuni tu Mkuu wa zamani wa jeshi la Rwanda jenerali kayumba nyamwasa alikoswakoswa risasi na inasemekana kama si Tanzania kumpa safe passage mpaka afrika kusini basi angeuwawa,
Pia hata makundi ya wafugaji wa kinyarwanda wanaojifanya kutafuta malisho katika mapori ya Mkoa wa geita,kagera na kigoma yaangaliwe vizuri sana,majasusi wanaweza kujifanya wafugaji na wakawa wana track kila kinachoendelea mipakani,juzi kuna mkuu wa pori moja huko kagera,alipotaka kuwaondoa wahamiaji haramu akajikuta yeye ndiye anapoteza kazi,hawa watu wana nguvu kiasi gani? Na kwa nini wanyarwanda waone sehemu ya kufugia ni Tanzania lakini waganda na warundi wasione hivyo?