Espionage; How agents transmit findings

Ila hao maspy wote cha mtoto kwa mapunda wa kitanzania.wee mtu anasafirisha kete kadhaa za sembe toka bongo hadi uchina kwa njia ya haja kubwa na bado anawasili salama bila kushukiwa.
Hao ni rahisi tu kushikwa, sema tu mamlaka husika zimeendekeza rushwa. Mtu aliyehifadhi madawa tumboni mwake akifanya full body screening mbona yanaonekana tu
 
Habari wakuu, natumai wote ni wazima. Napenda kuwaletea thread kuhusu Espionage au Intelligence. Espionage ni nini? Espionage ni kitendo cha kukusanya taarifa au nyalaka muhimu za nchi/taifa au taasisi kubwa. Taarifa izo zaweza kua za biashara, siasa au nguvu ya jeshi la taifa jingine nk na kuzi hamisha au peleka sehemu zinapotakiwa kwenda. Kumbuka kua, taarifa izi hupatikana kupitia njia za kwa siri kwaiyo lazima zifichwe ili yule anayechunguzwa asiweze gundua kile kinachoendelea na vile vile ni kwaajili ya kulinda usalama wa taarifa zenyewe, yaani taarifa zifike zikiwa katika ubora unao hitajika.

Thread hii inalenga kuzitaja njia zitumikazo kuhamisha { transmit or communicate } taarifa za kijasusi. Taarifa zikishapatikana zinahitaji kufanyiwa kazi au kuchunguzwa, sasa taarifa haiwezi chunguzwa kama haijafika pale panapo staili

· Kwa kutumia geresha ya sigara au kiko

Hii njia hupendwa kwasababu si rahisi, katika hari ya kawaida mtu kufikiri kua, ndani ya sigara anayovuta spy kuna weza kua na ujumbe wa kiintelejinsia. Pia ni njia rahisi kwa usalama wa spy huyo maana kama akigundulika au akishukiwa, basi huweza poteza ushahidi kwa kuuchoma kama vile anavuta sigara.

· Kwa kutumia soli za viatu

Kwenye soli ya kiatu kuna kua na nafasi ndogo ambayo imetengenezwa ( chamber ) ili kuweza kuhifadhi taarifa ndogo ndogo. Mfano memory cards zinaweza fichwa hapo. Njia hii ilipendwa sana na warusi maana ilikuwa, japokuwa inaonekana ndogo lakini ina uwezo mkubwa. Memory card iliyofichwa kwenye soli inaweza kua na mafile ya picha hadi 500 – 10000. Au mafaili ya audio records 1000 kutegemea na ukubwa wa device.

· Kwa kutumia michoro ( tattoo ) kwenye visogo, kisha kuotesha nywele kwenye maeneo hayo ya kisogo upya

Njia hii inatumika kwasababu ya usiri wake. Si rahisi mtu kumshuku spy kama anaweza kua ameficha taarifa kwenye kisogo chake kwa kutumia michoro. Kwaiyo ujumbe au taarifa zinaweza kuonekana pale tu baada ya spu huyo kunyolewa nywele na kupaka kimiminika ( chemical ) sahihi kisogoni kwake.

· Kwa kutumia macho feki

Hii njia inatumika kwa kuchukua kipande cha kioo ( lenzi ) na kuweka kwenye macho, ila nyuma ya lenzi iyo kuna kua na nafasi ndogo ya kuweza kuhifadhi devices ndogo kama micro chips ambazo zinakua zime hifadhi taarifa muhimu.

· Kwa kutumia sarafu au shillingi

Hii shillingi huonekana kua ni ndogo kwa mtazamo, ila zinkua na katundu kadogo kadogo ambacho hakaonekani kirahisi, ambacho ukichukua pini na kuipenyeza kwenye ako katundu basi shillingi iyo, inajifungua kati kati au nusu kwa nusu. Katikati unaweza tunza micro chips au memory cards ambayo inaweza kua na taarifa yenye ata kurasa 50 au zaidi.

· Kwa kutumia karatasi maalumu

Hii ni karatasi ambayo, kwa mtazamo inakua tupu yaani haina maandishi kwaiyo sio rahisi kwa mtu kuishuku. Ila ukweli ni kua, karatasi hii inakua imebeba ujumbe ndani yake. Ujumbe huu huweza kuonekana kwa kuchemsha iyo karatasi kwenye vimimini vya kemikali sahihi, au maji nk

· Kwa kutumia dead drop

Hapa taarifa hufichwa kwenye eneo ambalo linajulikana kabla au mapema, na baada ya muda mfupi, mtu mwingine anaenda kuzichukua. Njia hii ni maarafu sana na inatumika sana, ni kama zile the most celebrated kamasutra positions hahaha. Faida yake ni kua, inazuia nafasi za yule anayeficha taarifa na mpokeaji kukutana uso kwa uso au kua wote pamoja kwa wakati mmoja katika eneo husika. Ivyo basi, ata ikitokea muhusika anafuatilia ( kama ni double agent ) anaweza akajitetea, na hasa kama eneo lenyewe ni kama kwenye garden, anaweza sema kua ameenda kupunga upepo nk. Taarifa inaweza wekwa kwenye mfuko wa takataka, kinyesi cha ng’ombe au sehemu yeyote ile ambayo itamfanya mpita njia akiona asiweze kuoata kishawishi cha kutaka kuchukua au kudadisi izo taarifa.

· Kwa kutumia mizoga ya wanyama

Mnyama ( panya, paka, sungura nk ) mwenye umbo dogo, ambae yupo hai, anauawa, kisha taarifa za siri zinawekwa ndani yake, anashonwa kwa operation. Baada ya hapo hatua inayofutia ndo muhimu zaidi na ndiyo inayoleta tofauti ( usiri ). Mnyama huyo hunyunyuziwa vimiminika vya kemikali ambavyo hufanya aoze na kutoa harufu mbaya ambayo ni kero kwa watu na ata wanyama ambao katika hari ya kawaida hua wanakula jamii iyo ya wanyama ( mzoga ) kuchukizwa na iyo harufu na kupuuzia huo mzoga, kisha hutupwa kwenye eneo husika au lililokusudiwa ili muhuika wa upande mwingine aweze kuona na kuchukua taarifa izo.

Kama unafahamu njia zingine, pls share
kuna mada iliyokuwa na kichwa TISS wanatumia vyombo Gani vya mawasiliano? ilianzaishwa siku kama tatu zilizopita ila naona ilikwisha fungiwa. kwa sasa naona umeamua kuja kwa style nyingine tofauti kabisa. rai yangu kubwa kwetu sote ni kwamba naomba tusipende kuwachimba sana hawa ndugu zetu wa TISS kwa kuwa wanayoyafanya ni kwa maslahi ya taifa zima la Tanzania pasipo kujalia itikadi zetu. kuelimishana kuhusu taaluma hii kongwe ya ujajusi si vibaya sana lakini naomba tujiwekee mipaka ya vitu vya kuuliza.
Long live Tanzania.
"Das Billige ist immer das Teuerste"
 
Tiss haijatajwa hapa, acha kuleta uchochezi, rejea kichwa cha habari.
 
kuna mada iliyokuwa na kichwa TISS wanatumia vyombo Gani vya mawasiliano? ilianzaishwa siku kama tatu zilizopita ila naona ilikwisha fungiwa. kwa sasa naona umeamua kuja kwa style nyingine tofauti kabisa. rai yangu kubwa kwetu sote ni kwamba naomba tusipende kuwachimba sana hawa ndugu zetu wa TISS kwa kuwa wanayoyafanya ni kwa maslahi ya taifa zima la Tanzania pasipo kujalia itikadi zetu. kuelimishana kuhusu taaluma hii kongwe ya ujajusi si vibaya sana lakini naomba tujiwekee mipaka ya vitu vya kuuliza.
Long live Tanzania.
"Das Billige ist immer das Teuerste"
Sawa mkuu. Ndiyo maana nimesema machache tu
 
mkuu,kuna taarifa kuwa sio mapunda wanaofanikiwa kupitia ktk viwanja vya ndege bila kushukiwa wametoa rushwa.

inasemekana wengine hutumia sayansi ya kiafrika.
Kuzidiana akili na uwezo iyo ni kawaida
 
Animals,
1. Birds.
2. Rodents (squirrels are the best)
3. Dolphins.
4. Cats and dogs. (Thou the feline family is too unstable)

Broadcasting,
1. Radio broadcasting. ( Notoriously used in Kossovo)
2. Television broadcasting.

Theatre and Arts,
1. Paintings.
2. Movies. ( The CIA and MOSSAD use this, thanks to Joseph Goebbels and Abhwer for developing this)
3. Music. ( Used in Yugoslavia, Afghanistan and Chechnya)
4. Books. (Developed by the British secret service)
 
Noted sir
 
Back
Top Bottom