Omusolopogasi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2017
- 7,101
- 18,061
Kuna mwalimu alikuwa anatufundisha tebo wakati tuko darasa la 2. Ukikosea unapigwa na kufinywa. Kabla ya kujaribiwa uwezo wako wa tebo, uliitwa mbele ya darasa na kuombwa kuanza kuimba tebo moja moja - ya kwanza hadi ya 12. Kipigo kilipozidi, tukagundua mbinu. Tukaandika tebo ngumu ngumu kwenye sakafu. Tukifika kwenye tebo ngumu, tunapiga chabo kwenye sakafu. Mwalimu hakuwahi kugundua.