Enough is Enough

Dionize N

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,848
3,293
ULE msala wangu na girlfriend wangu ulotokea ijumaa nikawasilisha ili kupata ushauri hatimaye jana uvumilivu ulinishinda maana naona alidhamilia kujidhuru, toka ijumaa jioni hadi jana mchana alikua bado kagoma kula ikabidi niende kwa mjumbe na nikamweleza issue nzima nikaja nae home ili kumaliza

Mjumbe kamuuliza maswali huyu dada hakupata hata cha kujibu na rasmi jana tukaachana na leo saa 12 kapanda gari kurudi kwao Tabora.
Ila sasa kanitumia ka ujumbe anasema haki yake haipotei bure kwa vile nimeamua kumpiga chini siwezi mtumia kwa muda wa miaka miwili halafu aende hivihivi

Kwa kukaa kwetu miaka miwili tayari kulikua na ndoa hivo nimpe fidia kwa aidha mkwanja au tugawane vitu vinginevyo anaenda mahakamani kudai haki yake kwa kigezo kwa Presumption of marriage...mimi nmemjibu nenda huko huko mahakamani tutajua

WANAWAKE WA KIZAZI HIKI CA BONGO FLEVA BANA MNAKUA KAMA MMELOGWA AISEE, TUNAJUA SASA HIVI HALI NI NGUMU ILA ACHENI KUTAFTA UNAFUU KWA NGUVU.
 
Tabora..!
Mkuu..! huyo ni muongo haendi mahakamani,watu wa Tabora huwa hawana uwezo wa kuongea mahakamani na hilo wanalijua, kesi zao nyingi huwa wanashindwa.
Kimbilio lao kubwa katika kudai haki zao ni kwa Mzee Sangoma, hapo ndio hawajawahi kushindwa.
Nasikitika kwa kukupoteza JF mkuu..!
 
Mkuu mimi namwamini Mungu sangoma hawezi shindana na Mungu, namimi nahisi anatishia tuu kwenda mahakamani lakini vyovyote iwavyo make hamna namna. Lakini kwanini umesema unasikitika kunipoteza JF?
 
Mwanamme wewe usishindane na mwanamke,hata kama humtaki mueleweshe na malizaneni kwa ustarabu kama mlivyo tafutana,zogo kelele inahusu nini mpaka mfike kote huko?
 
Mkuu..! huyo ni muongo haendi mahakamani,watu wa Tabora huwa hawana uwezo wa kuongea mahakamani na hilo wanalijua, kesi zao nyingi huwa wanashindwa.
Kimbilio lao kubwa katika kudai haki zao ni kwa Mzee Sangoma, hapo ndio hawajawahi kushindwa.

!!!!!!!
 
Umemuelewa jamaa alivyojieleza? Mtu hataki kuongea sasa afanye nn
Hashindwi kumfanya akaongea si mtu wake? ambembeleze ataongea jamani mwanamke ni mtu wa kudekezwa pole pole atasema lakini ukimfanya kama unaongea na mwanamme mwenzio atasemajeee?
 
Mkuu mimi namwamini Mungu sangoma hawezi shindana na Mungu, namimi nahisi anatishia tuu kwenda mahakamani lakini vyovyote iwavyo make hamna namna. Lakini kwanini umesema unasikitika kunipoteza JF?

Uamwani Mugu wakati umezini na dada yangu mlipe chake sisis watu wa Tabora sio wa sport sport, moto gwa nsanzu ...........
 
Mwanamme wewe usishindane na mwanamke,hata kama humtaki mueleweshe na malizaneni kwa ustarabu kama mlivyo tafutana,zogo kelele inahusu nini mpaka mfike kote huko?
Nimejitahidi sana kutafta suluhisho lakin ananiangalia tuu kama picha na nashangaa kwann kabadilika ghafla sina namna nyingine aisee
 
Umemtia mwenzako hofu hofu na mashaka tele... hajui kwanini huyu demu ana roho....
 
Nimejitahidi sana kutafta suluhisho lakin ananiangalia tuu kama picha na nashangaa kwann kabadilika ghafla sina namna nyingine aisee
Sio kweli mkuu kua huna namna ukisema umemchoka i can understand,lakini namna huna sio kweli umeweza kumsomesha mpaka akakutolea nguo unashindwaje na hili jamani...
 
Sio kweli mkuu kua huna namna ukisema umemchoka i can understand,lakini namna huna sio kweli umeweza kumsomesha mpaka akakutolea nguo unashindwaje na hili jamani...
sijamchoka ila alikua anajaribu kunichosha kwa kitendo chake alichokifanya kwa huo muda mfupi. nmeongea nae karibia kila aina ya maneno ila wapi
 
Mmh huyo alikua anatafuta tu sababu,wanawake kuna muda tunapenda mteremko sasa mambo ya kugawana vitu ya nini!! Jitahidi tu umpe kiasi cha fedha anazotaka kuepusha ugomvi
 
Mpo katika sehemu ya pili ya mapenzi yaani nyakati za Shubiri ......pole sana ila umekosea kumuacha aende peke yake imagine asipofika kwao huku ndugu zake wakijua yupo kwako na akajapatwa na madhara (kufikwa na umati ) utasemaje? Muda mwingine wanaume mtumie akili kwanza unaakaje na mtoto wa watu miaka 2 bila ya ndoa !?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…