EMPIRE OF DUST: Hii nafikiri ni filamu nzuri yenye funzo, kuna jambo mchina akielezea kutuhusu sisi waafrika kupitia Congo

Mi mi

JF-Expert Member
Jul 14, 2024
2,128
4,327
Tunaweza sote kuitafuta hii filamu. Kupitia video clip niliyoona imenivutia kutaka kujua kiundani zaidi.

Hapa mchina akitoa somo fupi kwa huyu mkongo na kwa kiasi kikubwa somo hili ni picha yetu sote waafrika tunafanana mambo sio kongo wala sio Tanzania au Uganda na ni picha halisi ya wachina nao wanamfanano wa mawazo kama azungumzayo huyu bwana mchina.

Filamu ya empire of dust kwa taarifa za mtandao imefanyika Congo kwenye maeneo ya ujenzi imetoka 2011

Video fupi ya hiyo filamu hii hapa

Nafikiri matatizo yetu kwa kiasi kikubwa yapo zaidi katika tamaduni zetu nakusudia mtindo mzima wa maisha yetu wenda sipo sahihi naweza kusahihishwa ila mimi nimefikiri hivyo.

Ni kama kuna kitu kina niambia kuwa tulichelewa kufanya civilization ili kukimbizana na dunia wakati huo hivyo tukakutwa tupo nyuma sana na kwa kiasi kikubwa sasa hatuoneshi jitihada za dhati za kukimbia kwa kasi kuifikia mahali dunia ilipo.

Nimevutiwa zaidi kuitazama filamu hii kwa sababu nimewahi kufanya kazi na hawa wachina kwa kiasi kikubwa kuna vitu nitavielewa katika hii filamu kuhusu wao.
 
Maendeleo kwa tafsiri ya ulaya sio mtazamo wetu kwani ni kitu kigeni mtazamo wetu kwa tamaduni zetu maendeleo yalipimwa kwa muonekano wa umiliki wa wingi wa mifugo,wake, watoto,mashamba nk.
Na sio kwa hili la ukuaji wa miji ya kisasa,viwanda, huduma za kijamii nk.
Tukitaka haya ni lazima tubadili tamaduni zetu yaani kupokea civilization ukishasema civilization means kuiga ya wenzetu weupe ambayo kuyafikia hayo ni lazima tuwe na mitazamo kama yao.
Maana pana elements za kiafrika na elements za watu weupe.
Elements ndio uleta tofauti za ki maendeleo na sio wingi wa raslimali.
Thus hata leo tuwe tunaokota dhahabu na almaas kama zamani still hatuwezi endelea.
Achana na propaganda za Pan-Africanist za kulaumu ukoloni kama kikwazo utadhani Africa pekee ndo ilitawaliwa.
 
Anhaa najaribu kukuelewa
 
Anauliza wabeljiki wako wapi
Wamewaachia miundombinu na mmeiharibu yote
Pindi mnapopokea mshahara mnaenda kulewa baada ya hapo kesho yake mnaenda kuomba mkopo

Kweli hizi ndio tamaduni anazotaka jamaa mwenye uzi huko tuzifuate?
 
Hapana hayo yalikuwa malalamiko ya huyo mchina kuhusu wafanyakazi wake wa kikongo.

Ndio maana huyo mkalimani wa kikongo aliamua kukaa kimya
 
Mwafrika aliumbwa kuishi porini, kuvaa magome ya miti na ngozi za wanyama, jamii ni mbili wafugaji na wakulima, tawala zetu zilianzia kwenye koo, walipokuja hao washenzi ndio wakabadilisha mfumo wetu wa maisha ili wapate masoko ya bidhaa zao, tulikua na elimu yetu ya asili ya vitendo kutoka Kwa wazazi wetu, kila kitu walikiua ndio maana kucope na tamaduni zao tunajilazimisha tu
 
Nimeelewa vizuri mkuu na mimi nimeelewa hivyo kuwa wao wakongo wameachiwa kila kitu ila wameharibu
Na wakipokea mshahara tu unaisha wanaenda kumuomba Mchina mkopo tena
Au sio hivyo?
 
Mwafrika aliumbwa kuishi porini, kuvaa magome ya miti na ngozi za wanyama, jamii ni mbili wafugaji na wakulima, tawala zetu zilianzia kwenye koo, walipokuja hao washenzi ndio wakabadilisha mfumo wetu wa maisha ili wapate masoko ya bidhaa zao, tulikua na elimu yetu ya asili ya vitendo kutoka Kwa wazazi wetu, kila kitu walikiua ndio maana kucope na tamaduni zao tunajilazimisha tu
Kila jamii ilipitia maisha ya mtindo huo ila ilibadilika
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom