Egypt imepinga vikali makubaliano ya usimamizi wa Mto Nile

Maagano (treaty) ya mwaka 1929 kuhusu matumizi ya mto Nile, kura ya turufu (veto) wanayo Egypt pekee siyo mataifa mengine ya ukanda wa Afrika Mashariki


View: https://m.youtube.com/watch?v=qlW6k3XGWXw

Kihistoria Misri imepitisha mtazamo mkali wa matumizi ya mtiririko wa Mto Nile. Cairo inauchukulia Mto Nile kama suala la usalama wa kitaifa na taarifa zinaendelea kujumuisha vitisho vya hatua za kijeshi dhidi ya Ethiopia iwapo itaingilia mtiririko kama ilivyoainishwa katika mikataba iliyotiwa saini mwaka 1929 na mwingine wa mwaka 1959 .

Makubaliano ya kwanza yalifanywa kati ya Uingereza, kama nguvu ya kikoloni katika Afrika Mashariki, na Misri. Cairo ilipendelewa zaidi ya nchi zingine za pwani kama mali muhimu ya kilimo. Kwa kuongezea, Mfereji wa Suez unaoendeshwa na Misri ulikuwa muhimu kwa matarajio ya kifalme ya Uingereza.

Makoloni wa Uingereza ya - Sudan, Uganda, Kenya na Tanganyika (sasa Tanzania) - pamoja na Ethiopia hawakuwa na sauti.

Chini ya masharti hayo, Misri ingepokea mita za ujazo bilioni 48 kila mwaka na Sudan mita za ujazo bilioni 4. Misri haitahitaji ridhaa ya mataifa ya juu kufanya miradi ya maji katika maeneo yake lakini inaweza kupinga miradi yoyote ya mito ya Mto Nile katika nchi zenye chanzo cha mto Nile, ikiwa ni pamoja na kilomita za mraba 43,130 Ziwa Victoria. Ziwa la pili kwa ukubwa duniani la maji safi hulishwa na mvua ya moja kwa moja na maelfu ya vijito kutoka Tanzania, Burundi, Uganda na Kenya, zote ziko mashariki ya kati mwa Afrika
 
Misri iende ikawadai waingereza maji, ndiyo iliyowapa hizo haki za kutumia maji kwa ujazo huo.
Sisi kama Taifa huru hatujawahi kuingia mkataba na misri wowote kuhusiana na haki za kutumia maji.

Kama Misri ilijitutumua na kutwaa mfereji wa Suezi kinguvu dhidi ya muingereza, kwa nini itegemee sisi kuheshimu mkataba wa kikoloni wa muingereza?
 
Profesa James Ker-Lindsay anachambua mkwamo na tishio la vita kutokana na maji ya mto Nile
Views 79K

View: https://m.youtube.com/watch?v=7esq0T0J2nE


Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, mvutano umekuwa ukiongezeka kati ya Misri na Ethiopia, pande mbili kubwa na zenye ushawishi mkubwa barani Afrika.

Mara baada ya kufanya kazi kikamilifu, Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance litakuwa jenereta kubwa zaidi ya kuzalisha umeme kwa maji katika bara - na moja ya miradi mikubwa zaidi duniani.

Hata hivyo, Misri inahofia kuwa itatishia pia kutatiza maji yanayotiririka kando ya Mto Nile. Kulingana na mto huo kwa zaidi ya 97% ya maji yake ya kunywa, pamoja na kilimo, Misri imezitaka nchi hizo mbili kufikia suluhu kuhusu suala hilo.

Hata hivyo, licha ya juhudi za muda mrefu za upatanishi zinazofanywa na Umoja wa Afrika, wameshindwa kufikia muafaka. Wakati huo huo, pia kuna mvutano unaoongezeka na nchi jirani ya Sudan kuhusu suala hilo.

Kwa hiyo, kwa nini hasa tatizo limejitokeza? Je, suluhisho linaweza kupatikana? Na je, kuna uwezekano kweli kwamba inaweza kusababisha migogoro ya kupelekea matumizi ya silaha?

Msikilize kwa umakini uchambuzi wa kina wa Profesa James Ker-Lindsay mchambuzi bobevu wa migongano ya kimaslahi inayoweza kupelekea nchi na nchi kuingia katika mtifuano mkubwa na sababu zake hapo juu ktk video.

Source : James Ker-Lindsay
 
October 2024
Profesa James Ker-Lindsay - Tuangazie ubavu wa taifa la Ethiopia na kama linaweza kuhimili changamoto za ndani na zile kutoka nje.
Views: 211,878

View: https://m.youtube.com/watch?v=mOR1PsR7siU
Video hii inachunguza mzozo unaoongezeka wa Amhara nchini Ethiopia na uwezekano wake wa kuzua vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vinatishia kuwepo kwa nchi hiyo.

Mzozo huo ulianza Aprili 2023 wakati serikali ya Ethiopia ilipoanzisha operesheni ya kuwapokonya silaha wanamgambo katika eneo la Amhara, wakiwemo wanamgambo wenye nguvu wa Fano.

Walakini, kile kilichoanza kama hatua ya kawaida ya kijeshi iliongezeka haraka na kuwa uasi mkubwa, huku vikosi vya Amhara vikipinga kile walichokiona kama unyanyasaji wa serikali na usaliti kufuatia jukumu lao katika Vita vya Tigray.

Amhara, ambayo kwa kawaida ni kitovu cha siasa na utambulisho wa Ethiopia, sasa inakabiliana na kuongezeka kwa mivutano ya kikabila.

Mzozo huo, unaotokana na malalamiko ya kihistoria, unachochewa na mizozo ya kieneo na Tigray na Oromia, pamoja na tuhuma za serikali ya shirikisho inayoongozwa na jamii ya waOromo chini ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed Ali.

Kufikia 2024, vurugu kati ya Amhara na vikosi vya serikali na mapigano na mikoa jirani imeongezeka. Licha ya juhudi za kujadili amani, ukosefu wa uongozi wa umoja ndani ya Fano na ushindani mkubwa wa kikabila kote Ethiopia una maazimio magumu.

Huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu uvunjaji sheria na makundi yenye silaha yanayotumia machafuko hayo, Ethiopia inakabiliwa na mustakabali mbaya huku mzozo huo ukiibua hofu ya kusambaratika kwa taifa.
Source: Prof. James Ker-Lindsay
 
Kwahiyo unafhani kanuni za survival ni kuoneana huruma? Ili uwe giant lazima kuna mtu mahali aumie. Unadhani marekani amekuwa superpower kwa kuonea huruma vinchi vyenye resources?
Siyo lazima mtu aumie,huo ni mtazamo wa kibepari/kibibafsi
 
Mradi wetu wa Julius Nyerere HydroPower Project JNHPP Rufiji unaojengwa na Egypt utamalizika salama kwa kuwanyima maji wanayotaka Egypt kupitia ziwa Victoria na mto Kagera ?

Mradi wa JNHPP Rufiji unajengwa na kampuni ya kidola ya Egypt na hadi sasa ni vinu 3 katika ya tisa ndiyo vinazalisha umeme. Vinu turbines hivyo ni namba 9, namba 8 na namba 7.

Kila kinu kinauwezo wa kuzalisha 235MW. Uzalishaji ukifanywa kwa vinu vyote 9 kwa pamoja nchi itapata jumla ya 2115 MW za ziada kuingiza katika gridi ya taifa.


View attachment 3123870
Hii hoja yako ina uhusiano upi na Maji ya Mto Nile mkuu??

Maana kama ni swala la ukandarasi ni hawajengi bure.Wameshinda tenda na wakimaliza wanapewa chao
 
Hii hoja yako ina uhusiano upi na Maji ya Mto Nile mkuu??

Maana kama ni swala la ukandarasi ni hawajengi bure.Wameshinda tenda na wakimaliza wanapewa chao

Soft power nguvu isiyo umiza nchi kivita inayotetea maslahi yake (Egypt) inaweza kutumika kuweka rehani Tanzania mradi wake.

Mataifa mengi huona mbali inapojiingiza katika miradi ya kimkakati bandari, reli, mabwawa ya umem, usambazaji umeme ktk gridi ya taifa n.k .

Na nchi ya Egypt ina mikakati mingi ya fujo isiyoumiza bila kutumia vita au silaha lakini ikatumia kandarasi kuhujumu au kulazimisha kupata wakitakacho kwa njia nyingi ficho.

Unaposikia China, Russia, USA n.k kadhalika wanawekea vikwazo kampuni za nje ni mbinu mojawapo ya kujilinda, kuhujumu au kudhoofisha nafasi ya hasimu wake bila kuingia vitani kwa kutumia fujo isiyoumiza.

HUAWEI YA CHINA , MASHIRIKA YA MAREKANI YA USALAMA NSA, CIA , FBI.. WASEMA NI HATARI KWA USALAMA WA TAIFA

View: https://m.youtube.com/watch?v=iojQ153cai8
 
Egypt kama hawalijui JWTZ waende kwa Wafuasi wa zamani wa IDDI AMIN DADA...

Maji ya Ziwa Nyanza yanaweza saidia nchi nzima kuwa na kilimo cha umwagiliaji tukalisha Dunia nzima chakula we are blessed sema Misri wanatuzuia
 
Egypt kama hawalijui JWTZ waende kwa Wafuasi wa zamani wa IDDI AMIN DADA...

Maji ya Ziwa Nyanza yanaweza saidia nchi nzima kuwa na kilimo cha umwagiliaji tukalisha Dunia nzima chakula we are blessed sema Misri wanatuzuia
Labda Enzi za jiwe tungeweza kuwaonyesha. Tungechimba mabwawa kuelekea Mtwara
 
Waziri wa Maji wa Egypt amesema nchi yake haitakubali kupoteza hata mita ya ujazo ya maji ya Mto Nile. Amesema makubaliano yo yote lazima yahusishe nchi zote.
Wapumbavu
Waje watunze mazingira huku
Kuishi na mwarabu ni mateso tu
 
Back
Top Bottom