Edward Lowassa ni mwanamikakati au mwanasanaa?

Kwenye maandiko matakatifu yanaonyesha kuwa Sauli aliendelea kumtesa Daudi kwa mrefu na hata kutaka kumua kwa mkuki wana wa israeli waliteswa miaka 400 saa ya Mungu ilipofika Daudi kawa mfalme na wana wa israeli wakatoka misri kwa kishindo hivyo saa ya Mungu ikifika watanzania watatoka misri kwa kishindo kwenda nchi ya ahadi kishindo
 
Mwanamikakati ni mtu ambaye ana uwezo mkubwa wa kupanga mikakati ambayo huzaa matokeo chanya.

Mwanasanaa ni mtu mwenye uwezo wa kutengeneza mazingira yanayovutia lakini ambayo hayana ukweli au uhalisia.

Mwaka 2010 alipewa kazi kuhakikisha Mkoa wa Arusha unabaki kuwa ngome ya CCM kwenye uchaguzi wa Madiwani na Ubunge lakini akapata ‘’kipigo cha mbwa’’ kutoka kwa Godbless Lema.

Mwaka 2012, CCM walimpa tena jukumu la mikakati na kusimamia Uchaguzi wa Arumeru Mashariki lakini akagaragazwa na kijana Joshua Nassari wa tiketi ya CHADEMA.

Mwaka 2015 akajitosa katika kinyang’anyiro cha kuteuliwa kuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM huku akitumia mbinu ya ''mafuriko ya wanachama'' kama nguzo yake lakini jina lake halikukatiza hata kwenye Kamati Kuu ya CCM.

Baada ya miezi michache, CHADEMA walimpa jukumu la kuwapeleka Ikulu lakini akaishia kulalamika kuwa ameibiwa kura wakati alisema wamwachie kazi ya kulinda kura.

Mwaka huu, CHADEMA wamempa kazi ya kuwanadi wagombea udiwani wa CHADEMA katika uchaguzi mdogo, matokeo yanaonyesha amefanikiwa kushinda mgombea mmoja kati ya 20 waliogombea.

Huyu ni Mwanamikakati au Msanii?

Huyu katika siasa ni assset au Liability?
Ni "msanii"
 
Sio lazima kila mtu awe rais Wa nchi hii tufike mahali tuwe wakweli Lowassa ilikuwa ni kete ya hatari sana kumpa nchi......

Mtu ambaye alishinda Makanisani na misikitini akitoa Rushwa na marafiki zake wakina Rostam Aziz ungetegemea nini kipya kutoka kwake?.............

Ni bora mabadiliko yachelewe lakini si kumpa mtu asiyeaminika kwa jamii.......

Wacha tusubiri mabadiliko ya kweli hata kama watayaona wajukuu zetu..........
Dah, umenikumbusha Rostam. Taarifa za Forbes zinasema aliuza baadhi ya hisa zake 17.4% mwaka 2014. Sijui yalikuwa maandalizi?
 
Hata mziki wa Lowasa ulimfanya mtu kupiga push up na Mzee wa miaka mingi kuhamia kanda ya ziwa kuhakikisha hadi kuwapiga watu vibao wale waliogoma kusaini matokeo kuwa wameshindwa ili hali wameshinda.
Ila juzi kati Jirani zetu wamemuumbua
Kwa hiyo Lowassa anafanya mikakati ya watu kupiga pushup? This is fun to say the least!

Ok, Lowassa ni mwanamikakati!

Mikakati mingine ya Lowassa hii hapa ambapo vijana walideki barabara ili wakati anapita asipate vumbi;

CRBXbVCWwAALRZS.jpg
 
Saw a tufanye Lowassa ni mwepesi na upinzani ni mwepesi sana na haukubaliki kwa wananchi.
Sasa kwa nini kwenye uchaguzi kuna wizi wa kura, ulaghai, wasimamizi ambao ni makada kupindisha matokeo, matumizi ya nguvu za dola, kupigisha kura mpaka marehemu na figisu za kutosha kama tulizo ziona juzi uchaguzi wa madiwani na kule Dimani?
Mbona maeneo ambayo huwa ccm inayhakika wa kushinda kama Dodoma na Tabora hali huwa shwari?
Watu wazima kufanya ubazazi halafu kujiaminisha kuwa ni washindi huku mkijua kuwa bila mbinu chafu na tume yenu hakuna kitu ni zaidi ya upunguani.
Jee huu upunguani ndani ya ccm ni wa ku act kama bongo movie au ni upunguani halisia?
Wizi wa kura hutolewa maamuzi Mahakamani. Au hata mahakama huziamini?

Kinachofurahisha zaidi, hizi kelele za wizi wa kura husikika tu pale wanaposhindwa lakini huwezi kuzisikia wanaposhinda.

Kama wanafahamu kuna wizi wa kura, kwa nini wanaingia kwenye uchaguzi?
 
Dah... Halafu Mbowe anakuja kudai eti Lowassa kaongeza kura za upinzani uchaguzi ulipita.....wakati ndiyo alizipunguza.... Kura nyingi zilikuwepo kabla ya ujio wake ndani ya UKAWA... zilitengenezwa na viongozi... akiwamo Dr Slaa na Prof Lipumba..... alichokuja nacho Lowassa ndani ya UKAWA ni fedha... ndicho alichokipenda Mbowe
Ninakubaliana na angalizo/mtazamo wako.
 
Wizi wa kura hutolewa maamuzi Mahakamani. Au hata mahakama huziamini?

Kinachofurahisha zaidi, hizi kelele za wizi wa kura husikika tu pale wanaposhindwa lakini huwezi kuzisikia wanaposhinda.

Kama wanafahamu kuna wizi wa kura, kwa nini wanaingia kwenye uchaguzi?
Mkuu kuwa mkweli kama jina unalotumia, umeona jinsi maeneo ambayo upinzani unashinda jinsi juhudi za ziada zinazofanywa ili haki ipatikane.
Hakuna mahali mpinzani katangazwa mshindi huku yeye na wafuasi wake wako mahali wanakunywa kahawa, lazima kwa mbinde. Na kuhusu mahakama sio kila kitu kinapelekwa mahakamani kama huridhiki nacho, kwanza hata kufungua tuu shauri ni mamilioni yanahitajika. Hayo anayaweza Wassira mwenye fedha nyingi na muda wa bure
 
Bandiko langu limeonyesha hata wakati Lowassa akiwa CCM, aliwahi kugaragazwa kwenye chaguzi. Kama CCM inaiba kura kwa nini hakuiba hizo kura?

Kama wapinzani wanafahamu CCM wanaiba kura kwa nini hawapeleki malalamiko mahakamani na kama mahakama hawaziamini, kwa nini wanaingia kwenye chaguzi ambazo wanafahamu wataibiwa kura?

Sehemu wasiyoiba ni ile sehemu ya watu wanaojitambua haswa. Mahakama hazina tabia ya kutoa haki kwa wapinzani kwani hao mahakimu ni wajisiriatumbo. Wapinzani wanashiriki kwani ni haki yao kwakuwa hata wao ni walipa kodi hivyo wanahaki ya kutumia kodi zao wakati wowote.
 
Ni dhahiri watuu wa arusha hawaipendi ccm tokea kipindi Lowasa ndio mwenyekit wa ccm mkoa. so sishangai Lowassa kugaragazwa ktk hizo previous ellection.
 
Mi naamini kuendelea tu kuamini kwamba kura huibwa ni kujiweka mahali pabovu zaidi. Kulisemwa hapa, wakuu wa mikakati ya wizi wa kura ndani ya ccm ni Lowasa na Kingunge, leo wapo upinzani na Lowasa ni bilionea, bado tu tuendelee kuyaamini haya?

Kuendeleza imani hizi zinawanyima wapinzani kuujua udhaifu wao wa kweli ktk chaguzi. Hata wizi ukiwepo, upinzani una madhaifu mengi sana kuweza kushinda ktk baadhi ya maeneo.

Nilishawahi kusema humu, kuna yahusishwayo na hivi vyama vya upinzani, mfano : udini, ukanda, ukabila, ubinafsi, uhitaji wa mali na vyeo, ufamilia nk.

Hata kama itakuwa ni propaganda za wapinzani wao, kushindwa kujinasua nazo ni udhaifu na ushahidi wa ukweli haya mambo. Kwanini wasijitengenezee kamkakati wa kujinasua? Yanasemwa na yanaendelea tu kuendelea, nini maana yake hapa?

Ushauri kwa cdm, kama chama kikuu cha upinzani nchini, watanzania hawahitaji demokrasia wala kelele hizo, wanataka ustawi wao tu. Tengenezeni sera nzuri, jengeni utaifa, ziuzeni na wananchi waone kweli neema itafika. Cdm hawatangazi sera siku hizi hata hakieleweki.

Watz waliamishwa ufisadi na mafisadi ndo kikwazo ktk ustawi wao, mkawabeza kuwa hakukuwa na ufisadi wala mafisadi nchini. Sasa mdandia hata mabaa yanayotokea kiasili tu, njaa na matetemeko, yakisha sijui mtasafiria yapi tena.

Mrejesheni Dr. Slaa, mumuombe radhi, fukuza Mbowe na mamluki wake wote, ondoeni ukanda, simamieni sera zenu. Mtashinda, kinyume na hapo, mtazidi kushuka hadi kife kabisa. Mtazamo.
 
Kwa hiyo Lowassa anafanya mikakati ya watu kupiga pushup? This is fun to say the least!

Ok, Lowassa ni mwanamikakati!

Mikakati mingine ya Lowassa hii hapa ambapo vijana walideki barabara ili wakati anapita asipate vumbi;

CRBXbVCWwAALRZS.jpg
Kudeki barabara ulikuwa ujinga wa kiwango cha phd kwa wana ukwawa
 
Back
Top Bottom