Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,818
- 5,420
Aliyekuwa mtangazaji nguli wa EATV na East Africa Radio, Dullah Planet, Mjukuu wa Wambua rasmi ametambulishwa na kukaribishwa kwenye Radio ya Ali Kiba, Crown Radio. Ambapo tayari accounts za instagram zimepost kuonesha kumkaribisha nguli huyo wa vipindi vya TV na Radio.
Wiki chache zilizopita Dullah alionekana kuacha kazi katika kituo cha matangazo cha East Africa TV & Radio, hakusema ni wapi anaelekea au ni nini kilichomfanya aache kazi. Lakini badala yake Hapo jana ametambulishwa na Radio ya Ali Kiba.
SWALI: Je, hizi radio mpya haziwezi kuanza na kuibua watangazaji wapya wenye vipaji, yani ni mpaka wachukue watangazaji wakongwe wa-boost? Je, wasomi wa vyuo vya utangazaji hawatosholezi kuanzisha vipindi vya radio au ni mfumo wa Elimu ya utangazaji ni duni? Kwa nini watangazaji wale wale tu ndio wanagombaniwa na hizi media?