DSTV mmeniudhi kwa kweli, bora AzamTv

Mimi decoder yangu ya Dstv watoto wamegeuza toy LA kuchezea.. Wapuuzi sana bei za ajabu kisa EPL.. Nimetulia azam nachomis ni EPL tu ambayo naangalizia bar! Chonde chonde Mzee bakhresa tuwekee EPL hata kama utaongeza gharama kidogo
Suppose DStv nao wanashusha being,je utahamia Azam au utabaki DStv. acheni maneno,namba mshaisoma mnabaki kulalamika.
 
Sorry hivi DSTV inacost sh ngapi kununua decoda na mazagazaga yote pamoja na kufungiwa
 
Halafu wana ving'amuzi vya kizamani,ukiwasha ni dakika 20 mpaka kipate moto,pia ukilipia unasubirrrrrrrrrriiiiiiiiiiii,wanapitwa na STAR TIMES,wamelewa sifa hawa wapuuzi.
 
Sijui mnachoringia kwenye ushindani huu wa ving'amuzi! Nimekuwa mteja wenu wa muda mrefu lakini sasa naona mnataka niwakimbie. Toka nibadilishe kwenda kwenye ving'amuzi vya HD huu ni mwezi wa tatu kila ninapolipia hadi niwapigie simu niwabembelezeeeeee ndo mfungue picha. mmenifanya nimelipia kwenye Azam sasa wakati hayakuwa matarajio yangu, Ukilipia Azam hata dakika haiishi wanakuwa wameisha ifungua lakini DStv hadi uwapigie simu. Ukiwapigia wanaanza maswali sijui nini, wapuuzi nyie hamuangalii hata pesa zinazoingia zimetoka wapi....kama wahusika mpo humu angalieni Smartcard yangu [HASHTAG]#10434141577[/HASHTAG].
Ni kweli ni wasumbufu kupita maelezo
 
Tatizo lako unaunga unga na kuruka tuka kama ndege tulia na kifurushi kimoja na usibadili badili km kinyonga kila mwezi ni system zote za vingamuzi ukilipia kile kilichoisha itafunguka ila umelipia kingine lazima uwapigie wakuhamishie kwny hicho ulicholipia kwani ukitaka kushuka kituo cha msaada kwny daladala si lazima umwambie konda asimamishe gari .....acha ufukunyuku
 
Nimetupa Dstv, nipo Azam tv...angalau pesa itabaki ndani na kuajiri wazawa.Azam kweli ni burudani kwa wote.
 
Back
Top Bottom