Drama za Utotoni: Kisa cha Leah na Ghetto la Mchongo

Mturutumbi255

JF-Expert Member
Jun 7, 2024
200
419
Eee bwana eeh, stori za mtaa ni noma sana! Basi ebwana, ulikua utotoni kwetu mtoto wa kike mrembo alikua mmoja tu, Leah yule kapisi keupe, si unajua tena sisi wanaume tulivyokuwa tunamuwania. Sasa Leah huyu alikuwa ndo kidume, yeye ndiye anachagua leo rafiki yake awe nani. Na ikifika zamu yako, aaah bro, utaenjoy kinoma!

Siku moja zamu yangu ikafika, wakuu wa mtaa wakatuandalia ghetto la mchongo, tukaingia pale ndani kama bwana na bibi harusi. Kumbe wale majamaa walikuwa washaniuzia teja, wakaenda kunimwaga kwa mama yake Leah. Duuu, vile nilichezea kichapo, mpaka leo hii nikiwa nakumbuka, nasikia maumivu ya belt!

Na kama wewe ni mtoto wa 2000, huwezi elewa hizi movie za mtaa. Hebu wadau, nani anakumbuka matukio kama haya utotoni kwake? Mlijikwaa na kasheshe gani na mademu wa mtaa? Toeni story hapa tucheke pamoja!
 
Back
Top Bottom