Dr Tulizo: Kwa mwaka 2023 asilimia 42 ya wagonjwa waliohudumiwa JKCI waligundulika kuwa na shinikizo la juu la damu

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
138
229
Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya Shinikizo la juu la damu ambayo uadhimishwa kila Mei 17, kila mwaka, Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka hospitali ya JKCI,Dr Tulizo Shemu amesema kuwa katika wastani wa watu wazima 10 kati yao watatu hadi watano wanakuwa na shinikizo la damu.
images - 2024-05-16T084730.488.jpeg

Amesema kuwa kati ya watu hao asilimia 30 ndio wanatambua kama wana changamoto hiyo na ndio wamefanya vipimo na kuwa kati yao asilimia 9 ndio wamekuwa wakipatiwa aina mbalimbali za matibabu ambao kati yao asilimia 4 tayari wameanza kuthibiti msukumo wao wa damu mwilini (Blood pressure)

Aidha imeelezwa kuwa Takwimu za Wizara ya Afya kupitia MTUHA( DHIS-2) kumekuwepo na ongezeko asilimia 9.4 kwa wagonjwa wa moyo na shinikizo la damu pekee kutoka wagonjwa milioni 2.5 mwaka 2017 hadi wagonjwa milioni 3.4 mwaka 2002

Aidha Daktari huyo amesema "Kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ni hospitali pekee ya moyo hapa nchini kati ya wagonjwa 125, 927 waliotibiwa mwaka 2023 asilimia 42 sawa na watu 52,900 walikuwa na tatizo la shinikizo la juu la damu. "

Amesema hiyo ina maana kwamba kila wagonjwa 10 waliowapokea hospitalini hapo wanne walikuwa na tatizo la shinikizo la juu la damu au madhara ya ugonjwa huo.

Amesema kuwa ugonjwa huo kwa sababu sio rahisi kuona dalili zake, lakini amedai kuwa inaonesha kwamba nchini kuna Watu wengi wanasumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la juu la damu lakini hawatambui kama wana ugonjwa huo kwa kuwa hawajapima.

Amesema kuwa katika kuadhimisha siku hiyo wataalamu kutoka JKCI kwa kushirikiana na wadau wengine wanatoa huduma ya vipimo bure kwa siku mbili kuanzia Mei 16 (leo) hadi kesho Mei 17, 2024 ambapo itakuwa siku ya maadhimisho, zoezi hilo litafanyikia Hospitali ya Dar group iliyopo pembezoni na daraja Mfugale Jijini Dar es Salaam.
images - 2024-05-16T085430.072.jpeg

Amesema kuwa licha ya vipimo huduma hiyo inaambatana na ushauri mbalimbali kwa Watu wenye changamoto hiyo na hatua mbalimbali ambazo wanaweza kuzichukua kuepuka madhara zaidi. Ameongeza kuwa huduma hiyo itakuwa kwa ajili ya watu wote bila kujalisha vijana, ambapo amedai kuwa kuwa hata vijana kwa sasa wanaonekana kukumbwa na tatizo hilo, hivyo ametoa rai watu kujitokeza kufahamu hali ya afya zao.

Awali amedokeza kwamba shinikizo la juu la damu linaweza kuepukika kwa watu kufanya mazoezi kuzingatia lishe bora kwa kula matunda na mboga mboga, vyakula vyenye madini ya potassium, vilevile kupunguza ulaji wa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha mafuta na chumvi kuepuka uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kupita uliokithiri, kutambua kiwango cha sukari katika mwili, kutambua msukumo wa damu na kiwango cha mafuta mwilini.

Amesema kuwa madhara mbalimbali yamekuwa yakitokea ikiwemo kutokana na tatizo hilo, ikiwemo mwili kupooza, shambulio la moyo, moyo kushindwa kufanya kazi, kutanuka kwa ukuta wa mishipa ya moyo, ugonjwa wa figo, kupunguza nguvu za kiume na kupunguza muda wa kuishi.
 
Huu ndio ukweli
Ukweli mwingine ni kuwa hao watu wengi ni wafanyakazi either serikalini au kwenye taasisi binafsi na mashirika ambapo huko ni mwendo wa kunafikiana Kila kukicha na kupeana tabasam za uongo huku Kila siku vitisho na mikwamo vikiongezeka
 
Back
Top Bottom