Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 302
Sijakuelewa unapodai chaguzi za kibabe zina mwisho kwa hiyo unaposema tuwape muda ina maana tuwasubiri hadi watakaposema sasa leo ndio mwisho wa ubabe, you must be joking.kwa vyovote vile kama marekani akisitisha misaada basi viongozi wetu sio wataoteseka bali ni yule mwananchi wa kijijini. leo mimi na wewe tunaweza kuishi ata kama nchi yetu ikisitishiwa misaada lakini kizazi cha masikini katika taifa letu kitateseka .kwa maslahi ya taifa letu nadhani ni vema tufanye chaguzi huu umepita na tugange yajayo. dr slaa bado ananafasi ya kujijenga kwani yeye ni katibu mkuu wa chama kitachokuwa na wabunge kama 50(+viti vya wakike ,maalum). mimi ni mshabiki wa haki daima lakini sitokuwa tayari kuunga mkono kauli na shinikizo la marekani ata kama kwa lengo zuri. daima naipenda tz na naheshimu tawala zilizopo pia nazikosoa lakini sitokubali kupokea amri ya kuishinikiza serikali yangu toka kwa wakoloni. ni bora nitawaliwe na kiongozi nisiyempenda kuliko kusalimu amri kwa marekani.
daima chaguzi za kibabe zina mwisho lakini uwezi kukwepa mabadiliko. pia tambua kuanguka kwa ccm ghafla kungeweza kuleta magonjwa ya moyo kwa makada wake na ata machafuko. nadhani tupeni kipindi cha kuwaandaa wana CCM kwa miaka 5 ,hapo itakuwa ni wakati ambao ata wao wanajua watashindwa na hakutakuwa na madhara makubwa. CHADEMA tambueni miaka 5 si mingi. msivuruge nchi mtayokuja kuitawala