Dr. Kitine: Ni Ndoto Maalim Seif Kuwa Rais wa Zanzibar

Nashauri kusiwe na uchaguzi tena Zanzibar na badala yake ingojewe siku ambayo yatafanyika mapinduzi mengine hata kama ni miaka 2000 ijayo.

Hela za uchaguzi zitumike kuboresha huduma muhimu za jamii.
 
Sasa kama wanajua hivyo kwanini chama cha majipu kinaitisha uchaguzi, halafu huyo ni msomi wa phd anaongea uharo huo bado tuna safari ndefu.
 
Dk. Kitine, pamoja na makandokando yake lakini walau kama kachero mbobevu na DG wa TISS mstaafu hakupepesa macho wala kumung'una maneno. Huo ndio ukweli wa mkwamo wa kisiasa Zanziberi.
Sasa kama huu ndio ukweli kwa watawala kuna haja gani ya kuwa na uchaguzi wa vyama vingi Zanzibar? Kwanini serikali inaendelea kupoteza pesa ya uchaguzi huku ikijua kama akishinda fulani hapewi nchi? Swali kwa Dr. Kitine, yeye kama mtu mwenye kujua siri nyingi na muhimu za taifa letu anashauri nini kuhusu chaguzi za Zanzibar? Na suruhisho la milele la tatizo hili ni nini? Je, yawezekana kurejea mfumo wa chama kimoja Zanzibar maana bila kufanya hivyo unazuiaje watu wasichague upande mwingine kama si kutaka kuleta vurugu na mifarakano kwa watu wetu mara kwa mara? Tatizo kubwa la nchi hii ni kutosa uwazi na kutosema ukweli kuhusu mambo muhimu kwa taifa letu hasa kwa baadhi ya viongozi na wasomi ya nchi hii. Taifa limekuwa "politicalized" in all sectors of life.
 
kuna wakati historia hufutwa,kuandikwa upya na hata kusahaulika, kuna nchi zilipata uhuru kwa mapinduzi lakini baadae demokrasia ikatawala, Zanzibar inaweza kutawalika na yeyote mradi tu achaguliwe kihalali pia Tanzania inaweza kutawaliwa na chama chochote mradi kuwa na uhuru wa uchaguzi!!! 1964 -2016 ni mbali na mengi yamepita....
 
  • Thanks
Reactions: BAK
CCM inataka kupoteza fedha mara mbili kwa ajili ya uchaguzi wa viini macho.Kumbe ht lile bango la kibaguzi haikuwa bahati mbaya? na zaidi wafuasi wa CUF wanapigwa vijembe kama wanaweza nao wapindue! Kweli Africa kujitawala bado sana tunalazimisha tu.
 
Ni vigumu sana kumuelewa Dr Kitine, lakini huo ndio ukweli, siasa za zanzibar zimejaa ulaghai huku ukweli ukifichwa,
Ndugu Yericko Nyerere ukweli ni upi na ulaghai unaofichwa ni upi? Tusaidiane kujua haya mambo kwa faida ya nchi yetu. Ukiondokana na historia iliyopitwa na wakati wananchi wa Pemba na Zanzibar ni watanzania wenzetu sisi watu wa Tanzania bara (Tanganyika).
 
KWA Kweli Ni Aibu Kwa Mtu Ambaye Alikuwa Mkurugenzi Wa Idara Ya Usalama Wa TAIFA, Ndiye Anayezungumza Hayo!! Kwahiyo Uongozi Wa ZANZIBAR Au Wanaotakiwa Kuwa Viongozi, Lazima Wapate Kwa MAPINDUZI!!!?? Sio Kwa Njia Ya Sanduku La Kura!!?? Ama Pemba Ndio "WATWANA "Na Unguja Ndio "MABWANA " Maana Historia Inaonyesha Mabwana Walikuwa Watu Weupe (Wageni) Na Wale Weusi Ndio Watwana (Ambao Ni Wenyeji Waliokuja Miaka Mingi Kabla) !! Mh.KARUME Alijaribu Kuwaweka Karibu, Ili Kuoana, Kuzaliana Na Kuunda Mchanganyiko Wa KINDUGU Wa DAMU!! SASA Leo Inakuwaje Mnabaguana Au Wabaguane!!?? TENA Kwa Kuitana Machotara Na Wengine Ndio Wenye ZANZIBAR Yao Na Wao Ndio Walio Na Haki Ya Kuiongoza ZANZIBAR!!LKN Hao Hao Wanaoitwa Machotara, Wakiwa Ndani Ya CCM Hakuna Shida, Wanaruhusiwa Kuiongoza ZANZIBAR, Ila Akiwa Nje Ya CCM Tu Hafai Kuiongoza ZANZIBAR!!! Kwa Maelezo Ya Kitine, Ni Dhairi Kuwa ZANZIBAR Imeandaliwa Kuongozwa Na CCM Tu Daima Dumu!!! Tamko La Kitine Ni SIRI KUBWA Ya Mpango Mkakati Wa Idara Yake Alivyokuwa Akiongoza, Hivyo Yeye Anaifahamu Mipango Ya CCM Na SERIKALI Yake, Kutokana Na Nafasi Aliyokuwa Nayo!!!! Maana Kama Shida Ni Maalim Seif, Mbona Alipokuwa Ndani Ya CCM Alikuwa Na Nyadhifa Kubwa Tu Ndani Ya Serikari Yake!!!?? Alafu Hili Suala La Kurudi Kwa Huo "USULUTAN "Ktk Visiwa Hivyo, Kwa Vile ZANZIBAR Inaongozwa Na CUF, Ni HOJA Ambayo Haina Mashiko Wala Dalili Za Ushaidi!! Na Kila Anayeongea Hatuonyeshi Dalili Zake, Zaidi Ya Kujenga Dhana Ambayo Haina Uhai!!! HIVI Kipindi ZANZIBAR Ikidai Kujiunga Na OIC Na Kupelekea Mgogoro Wa KIKATIBA Na Kuzua Malumbano Makubwa BUNGENI Kati Wabunge Kutoka ZANZIBAR Na Wale Wa Upande Wa Tanganyika Tena CCM Wenyewe Kwa Wenyewe!!! JE, CUF Ilikuwa Inaongoza ZANZIBAR!!!!?? LEO Hii SHEIN Yuko Kuwait Kuwaomba Waje ZANZIBAR Kuwekeza Na Kujenga USHIRIKIANO Wa KINDUGU Na KIUCHUMI!!! JE, MAALIM SEIF Ndiye Aliyeoko KUWAIT!!!!?? JE, Waarabu Gani Ambao Wanasemwa Na CCM, Kuwa CUF Ikiruhusiwa Kuunda Serikali Chini Ya MAALIM SEIF, Basi Watarejea Tena ZANZIBAR Kutawala!!! HAO Ndio Wanaoitwa Wasomi Na Viongozi Wetu, Hawajui Kuwa Kipindi Kile Cha Ukoloni Mataifa Mengi Ya Kigeni Yalikuja Ktk Bara La Africa ( BARA JEUSI) Kwa Lengo Kuu La Kupata Material, Cheap Labours Na Markets!!! SASA Leo Karne Ya 21, Eti Bado Wakoloni Wale Wale Watakuja Tena Kutaka Kutawala Africa Tena ZANZIBAR!!!? Hebu Zitazame Hizo Nchi Zenye KUTAJWA Kuwa Watarejea Tena Kuitawala ZANZIBAR, Hali Zao Kiuchumi, Kijamii, Kisiasa N.k. HIVI Leo Kweli Zinahitaji Zanzibar Kupata Kipi!!!??? Kama Ni Kuwekeza Hata Leo Wanaweza Kuja Kuwekeza, Maana VIONGOZI Walioko Madarakani Wanawabembeleza Kila Uchao, Waje Kufanya Hivyo!!! Je, Ikishika Uongozi CUF Na MAALIM SEIF, Ndio Waarabu WANAREJEA Kuja KUWATAWALA Wazanzibar, Na Kuleta Yale Ya UTWANA Na UBWANA Tena!!!?? Kwanini Isiwe Kwa Hawa Wazungu Wanakuja Africa Kama Wawekezaji, Kufanya Yale Ya 1890!!!??? NI Propaganda Mfu, Ambazo Hata Wanajitoa Ufahamu Kwa Njaa Zao, Wanashindwa Kuthibitisha!!! KUMBE Sasa Kitine Umetudhihirishia Yale Yaliofanywa Na Jecha Salim Jecha, Ni UTEKELEZAJI Wa MAELEKEZO / MAAGIZO Ya CCM Na Serikari!!! Tunaamini Maneno Yako Yanatoka Ndani Ya Idara Uliyokuwa Ukiongoza Ktk Nyadhifa Nyeti Kabisa!!! Aksante Saanaa!!!
 
Dk. KITINE naona ameongea ukweli lakini hawa Wapinzani wahataki kuelewa uhalisia wa mambo hapa nchini mimi napenda kuwaambia siku zote kuwa Maalim hawezi kutawala Nchi hii hata muda wa Sekunde robo kutokana na Hiostoria ya nchi inavyojieleza Mapinduizi yalifanyika kwa upande mmoja tu wa Unguja na Pemba walipewa tu taarifa kuwa tumeshapinduwa sasa teremsheni bendera ya Bwana na pachikeni hii sasa wao jambo hilo hawakufurahi nalo na kwa kuwa walikuwa wameshazaa nao ndio maana waliona kuwa vigumu sisi kutengana na Waarabu ndio maana hdi leo wanataka warudi hapa nchini kwentu ili waendelee kunyanyasika hawakuyaona Mapinduzi hao na ndio maana hata ukiwaambia kuwa tumefanya mapinduzi basi wao wanakaidi lakini nasema Nchi hii ina wenyewe wala hatowahi kuingoza Seif asahau
 
Kama wanadhani ni rahisi na wajaribu.

We baki unaongea kirahisi rahisi ukidhani dunia ya sasa ni ile ya kupanga vita. Siku hizi kuna ugaidi kaka. Utaona mtu kaja sokoni na kikapu mara kakiacha kama anaongea na simu, chukua dk 10 tu, utasikia mlipuko mkubwa, ukiangalia sio chini ya watu 50 wamepoteza maisha, achia mbali majeruhi. Sitaki kuongea vibaya wenzetu wa pande hizo kujitoa muhanga wala sio kazi. Utabaki umesimamisha majeshi wakisubiri vita kama ile ya Uganda, kumbe mambo hayo yameshapitwa na wakati. Haki ni muhimu, huyo mzee Kitine anapiga siasa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Dr kitine hongera kwa kuwaelimisha kwani , serikali iliyopinduliwa waziri mkuu wake ali toka
 
Usiwajaze wenzako pumba jaribu kuwa mkweli kama ni historia hio Seif asingali pendwa Zanzibar na asingali pata kitu kwa wananchi wa Zanzibar.

Ccm kikuru bila kuingia jeshi la JWTZ basi haishindi na hizo siasa za majungu na unaguzi wananchi wa Zanzibar wameshazishtukizia rabda ndugu zetu wa huko bado hawaja zifahamu.
kwann seif apendwe sn pemba na uko pemba ndo kumejaa chimbuko la waarab na kizazi chao na sio unguja kwa wazawa
 
Back
Top Bottom