Upepo sio-ipo vyema sana!!Wamedondosha nyingine (WAGOSI) inaitwa UPEPO SIO
My favorite duo of all time na probably the most socioconscious emcees I've ever come across.
Kaveli anzisha thread ya wagosi wakaya tafadhari.
"Taratibu Jamani haya!!!
Tutaonana wabaya haya!!"
Moja ya mashairi ya Wagosi wa kaya.!!Heshima kwao.
"Kila Mkiugua mwaenda kutibiwa Ulaya-Ulaya Ulaya tupeni hela nasi tukatibiwe ulaya"
Mpaka sasa manesi wananyodo kibao.Tehe tehe!!''Tunaanza na manesi, nyie manesi mna nyodoo... '' hahaha
-Kaveli-
Respect bruh, hawa jamaa nilinunua album yao ya NYETI long time sana.In my music library, all tracks za Wagosi Wakaya nimeziplace kwenye 'most favorite' folder. Hawa wakongwe nyimbo zao zote hadi leo hii ni asali.... hazichoshi kusikiliza. Huwa nafurahi na kucheka sana nikiwatch ule wimbo wa 'BAO', walitumia sanaa ya kipekee sana kwenye huo wimbo.
Yes, wagosi are amongst of best conscious emcees in Tz. Too bad they got no 'avenue' in mainstream. daah
Salute to you mkuu Konsciouz, nitaanda thread ya hawa wakongwe.
-Kaveli-
Wimbo mzuri sana!!!
Kiufupi sekta nyingi Tanzania ufanyaji kazi wao ni uozo mtupu...WaTanzania tuwavulimivu sana lakini uvulimivu huu unachangiwa kwa kiasi kikubwa na Woga!!
"Passport bongo kuipata imekuwa kama kitu cha almasi"
Dr. Aliamua kuwavulia uwoga hawa(wizara ya uhamiaji).
Upepo sio-ipo vyema sana!!
"Upepo sio unapoelekea ukienda Mbio,,
Kadi ya mchango ukinipa ukiondoka minatupa,,
Upepo huu sio wabaridi ni wamoto kabisa"
Wagosi wa kaya hawa wakongwe wapo vizuri.
Hakika bongo ukiwa mpagania haki na msimamo usioyumba na uwoga ukaweka zero...utafia gerezani kwa kesi za kusingiziwa ama uishi kama Morgan na Mugabe.''...Kila mtanzania ana haki ya kuwahi na passport, licha ya kupata Passport sio kama kitu cha bahati,
Passport bongo inapatikana sana kwa manati, kupata passport lazima ukate zaidi ya laki walahi,
elfu 50 ndo haki lakini utakata zaidi ya laki...'' ''passport bongo kuipata imekuwa kitu cha almasi''
Naipenda sana hii pini... kuanzia beat, melody, na ujumbe. Huwa nabonyeza 'replay' nikifika kwenye huu wimbo. That's conscious hipHop, to voice out for the community. Too bad nyimbo kama hizi hazina nafasi kwenye media zetu, muda wote mapenzi & bata ndo zinasikika kwahewa.
UHAMIAJI: Hela/Rushwa, Urasimu, Ubabaishaji. YES, mpaka leo hii hiyo ndiyo UHAMIAJI yetu halisi.
-Kaveli-
Walikuwa wanapazaa sauti na kusaidiana na watu wanyonge wasio na uwezo wakuanika uozo na utendaji mbovu wa sekta hizi za bongo.
Mahaba yalimuzidia sana(chama) huyu kijana wa Tanga R.o.m.a mkatoliki.Nafikiri Roma aliwapenda sana hawa jamaa na akataka afuate msimamo wao wa kuikosoa serikali. So sad serikali imemuwahi Roma. Wagosi watabaki kuwa wakosoaji pekee wa serikali wasio yumbishwa na upepo wa kisiasa
Nitaupateje huo wimbo Mkuu!!Na hiyo ndiyo mojawapo ya 'essence' za uwepo wa HipHop. To voice out for the people. HipHop lives coz ni utamaduni ambao unazungumzia na ku-voice out juu ya maisha ya kila siku ya mwanadamu, hasa hasa kulisemea tabaka la oppressed community. HipHop ni platform ya kusema na kufichua matatizo mbali mbali yanayowagusa watu wanyonge/masikini. HipHop ni forum inayoelimisha na kuonya juu ya matatizo mbali mbali yanayoiathiri jamii yote kwa ujumla.
Mkuu, ili uelewe vyema ninachokisema, tafuta pini moja iitwayo 'MUDA WA VITENDO' by G-Solo. Ukiucheki/Ukiusikiliza huo wimbo, ndo utapata kuelewa vizuri dhima kuu ya hip-hop (conscious one) kwenye jamii. G-Solo alinyonga sana kwenye hiyo ngoma. Alitumia (sampling) beat kutoka kwenye track ya mtoni iitwayo 'THE G CODE' by Scarface.
-Kaveli-
Muziki wa kuikombaa Jamii au fikra au kukemea maovu ni watu wachache wanapenda...wengi wapo kwa anasa Mkuu.hahahahaa, juzi nimeisikia hiyo 'UPEPO SIO' nikasema kama ningekuwa na uwezo fulani wa kufanya jambo kwenye music industry ya bongo, ningehakikisha I bring Wagosi back on top, through media na public concerts. Hawa jamaa huwa inaniuma sana kuona umri unawatupa bila kufaidi kabisa matunda ya vipaji vyao.
Leo hii eti Hamorapa anapewa 'extravagant' promo na anajulikana sana kwa mitaa kuliko Dr John nor Mkoloni. Bullshitt !!
-Kaveli-
Mahaba yalimuzidia sana(chama) huyu kijana wa Tanga R.o.m.a mkatoliki.
Mahaba ya kitu chochote ya kikuzidia unakuwa kama bendera faata upepo,angekuwa neutral hii ingemsaidia sana tena sana.
Baadhi ya Mashairi!!
"Mtoto wangu nyundo mbili jela kwa kuvuta bangi yupi anastahili kifungo yeye au swahiba wa kikwete"-hii Ndio Tanzania.
"Nakomba pesa zote kisha nasepa kama lowasa"-mechi za ugenini.
"Kombe linaelekea monduli"-viva Roma viva.
Alisaidia sana kwa baadhi ya vijana kuamuka katika masuala ya kitaifa na kuyaongea mambo yagiza yanayofanywa na Serikali(JAPO baadhi ya wasanii walikuwa wanadai anaimba taarifa ya habari) kiufupi ujasiri anao.
"Minasikiasikia ufisadi
wanavyongezeka ndiyo wananipa midadi"