Tetesi: Dr. Dau kufikishwa mahakamani. Yasemekana kahojiwa TAKUKURU

Status
Not open for further replies.
Sasa ni wazi masaa na dakika za Dr. Dau (Mkurugenzi mstaafu wa NSSF) kukaa uraiani zinahesabika, baada ya jana Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kumhoji "kumfanyia interogation" kwa zaidi ya masaa 4. Hii inatokana na unadhirifu wa zaidi ya Billion 179 uliofanyika chini yake akiwa ni DG wa NSSF..

Dr. Dau anashitakiwa kwa makosa zaidi ya 5 ikiwemo ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka, kinyume na sheria ya PCCA No. 11/2007...

NB: Asante Rais Magufuli kwa kuamua kupambana na mafisadi na majizi, waliotuibia kwa zaidi ya miaka 10.
Ka tuhuma nzito tulizoziona mitandaoni na kwenye vyombo vya habari, it was just a question of time.
Lakini Dr Dau hakuwapeke yake, lazima kuna walio nyuma yake na walimuidhinishia ufisadi huu na kwa vyovyote wamefaidika sana na ufsadi huu.
Kiwanja kisicho na kitu kulipwa Tshs milioni 800 ni kufuru hata kwa Mwenyezi Mungu!!
 
Nasubir wapinzan waje waendelee kusema kwamba mafisad yanayotumbuliwa ni vipele...nasubir na Dr dau aitwe kipele/kidagaa tu kwenye ufisadi

Tunataka atugusie na wahusika walioiba ESCROW na kuchukua mapesa viroba pale STANBIC.

Na pia kuhojiwa na TAKUKURU siyo dawa tunapenda wafirisiwe ili kufidia.
 
Sina tatizo na kila Mtuhumiwa kupelekwa mahakamani maana hiyo sehemu ya mtu kujietetea !
Lajini anayedhani magifuli ni Mtakatifu na anaweza kukata Tawi alilokalia anajidanganya !
Kuhusu Lowassa anayesubiri kupelekwa mahakamani kwa issue ya Richmond anajidanganya !

Labda atanguliw Yeye kikwete

Mawaziri waliotajwa bungeni na makatibu wakuu !

Hapa Mbwembwe !!
 
Kama nawaona watetezi Wa dau sipati picha akipanda mahakamani hiyo siku sijui uzi wake jf itajuaje
 
Kazi ipo ,mwaka huu kuna watu watajinyonga tu. Maana mibuyu inadondoka . Lakini nina hofu na mzee wa kuzungusha mikono ,sijui watamfikia?
Majipu mengi hapa ni yaliyoota miaka mitano mpaka saba nyuma, na sio ya kukuibia wewe au mimi bali mali za umma. Yeye hakuwa kwenye system kipindi hicho, sana sana 'kitanzi' chake ni richmond lakini hilo TL alishamtaja mwenyewe pale Morogoro wakati wa kampeini.
Falsafa ya JPM huenda ikawa imekaa vizuri maana kupanga ni kuchagua. Angelianza na maisha bora kwa wananchi alafu baadae akawakamata mafisadi au ndio hivi anaanza na mafisadi kwanza theni maisha bora yanafuatia.
 
Hakuna aliye na ubavu kuhusu sakata la Radda..Escrow...Richmond...nk..nk..nk. sembuse sakata la Dr.Dau.Tuandike tu humu jf na yaishie humuhumu.
 
Sasa ni wazi masaa na dakika za Dr. Dau (Mkurugenzi mstaafu wa NSSF) kukaa uraiani zinahesabika, baada ya jana Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kumhoji "kumfanyia interogation" kwa zaidi ya masaa 4. Hii inatokana na unadhirifu wa zaidi ya Billion 179 uliofanyika chini yake akiwa ni DG wa NSSF..

Dr. Dau anashitakiwa kwa makosa zaidi ya 5 ikiwemo ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka, kinyume na sheria ya PCCA No. 11/2007...

NB: Asante Rais Magufuli kwa kuamua kupambana na mafisadi na majizi, waliotuibia kwa zaidi ya miaka 10.

Kwa Hili Mimi Namuunga Mkono Na Miguu, Magufuli, Ila Nitajaribu Kuwasiliana naye, Ni Kuhusu Msimamo tu, Siasa za Kulindana na Kung'anga'nia Madaraka, Kujua Kuwa CCM itashinda Liwalo na Liwe, Ndio hasa Iliyojenga Mazingira ya Kuwepo Mijizi. Yaani Tanzania ilikuwa Imeoza Kabisaaaaa! Naomba tu Magufuli akubali Kuondoa siasa chafu, Mungu amlinde "Kumbe kuimba watatawala Milele, sio Kutumikia bali kwao ni fursa ya(sio wote) kupora na kutafuna nchi kama Mazimwi na Mapunguani" Hii Inatisha!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom