Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,732
- 13,485
Utaratibu wa uchinjaji wa Wanyama katika machinjio na maeneo mbalimbali yanayotambuliwa
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi inalinda afya ya jamii kitaifa na kimataifa kwa kusimamia usalama wa afya ya mifugo na mazao yake nchini. Jukumu hili hufanyika kwa kutumia Sheria na Kanuni mbalimbali.
Uchinjaji wa Wanyama nchini unasimamiwa na Sheria mbalimbalia ikiwemo Sheria ya Magonjwa ya Wanyama Na. 17 ya mwaka 2003 pamoja na Kanuni zake za mwaka 2007 (Ante and Postmortem regulations); Sheria ya Ustawi wa Wanyama ya mwaka 2008 (Animal welfare of 2008) na Kanuni zake za 2009.
UTARATIBU WA WANYAMA WANAOCHINJWA
Wanyama wanaopelekwa mnadani (kutoka nyumbani kwenda mnada wa awali) mfugaji anakuwa na utambulisho (barua) toka kwa viongozi wa Kijiji ili kutambulisha kuwa mifugo husika ni ya mhusika na pia ni wa eneo husika hii husaidia kujua uhalali wa umiriki na afya ya mnyama maana magonjwa ya Wanyama wa eneo moja yanajulikana na mtalaamu wa eneo husika.
Wananyama wanaponunuliwa katika minada ya awali, upili au mpakani au kuhamishwa kutoka eneo moja kwenda jingine hukaguliwa na mtaalamu wa afya ya mifugo na kupewa vibali vya afya ya wanyama (Animal Health Livestock Movement Permit) ili kuelekea machinjioni au nje ya nchi.
Kwa wale ambao kituo cha mwisho ni wanapofika Machinjioni wanyama hao hupokelewa na vibali hukaguliwa na kuingizwa kwenye daftari la kupokelea Wanyama na huhitajika kukaa eneo la machinjioni kwa masaa kumi na mbili.
Wanyama hao watafanyiwa mambo yafuatayo kabla ya kuchinjwa: -
Ukaguzi wa awali (Anter mortem inspection)
Ukaguzi huu unalengo la kubaini Wanyama walio wagonjwa, waliokonda na wenye mimba. Wanyama watakaobainika kuwa na moja ya yaliyotajwa hapo juu hutolewa kwenye mnyororo wa chakula (Food chain).
Ukaguzi huo hufanywa na mtaalam anaetambuliwa na Baraza la Veterinari Tanzania kwa kufuata miongozo ya kitaalam (SOPs and Guidelines).
Baada ya ukaguzi wa awali Wanyama hao watakaa masaa 12 kabla ya kuchinjwa wakiwa wanapatiwa maji ya kutosha kwenye vyumba vya kutunzia Wanyama (Lairage) ambapo watapatiwa maji kwa muda wote huo.
Aidha, Muda huu pia unatosha kwa mnyama mwenye vimelea vya magonjwa kuanza kuonyesha dalili za ugonjwa.
Baada ya kukaa kwa muda wa masaa 12 wanyama hao watachinjwa kwa kufuata taratibu zote na nyama itafanyiwa ukaguzi (post mortem inspection) ili kubaini athari zilizopo kwenye nyama hiyo kabla ya kupekwa kwa ajili wa matumizi ya binadamu.
Aidha, mtu anapotaka kuchinja kwa ajili ya matumizi yake nyumbani na familia yake anaweza kuruhusiwa baada ya kumwita mkaguzi wa nyama.
Aidha, upande wa vijijini endapo mtu anataka kutumia nyama kwenye sherehe atatakiwa kumwita mtaalam wa afya za wanyama kwenye maeneo husika na awe anaetambuliwa na Serikali.
Sheria na Kanuni zinakataza uchinjaji wa wanyama wenye mimba na kufanya hivyo mkaguzi atakuwa amekwenda kinyume Sheria na Kanuni hizo.
Uchinjaji wa wanyama hufanyika kwenye sehemu zilizosajiliwa kama machinjio na vijiwe vya kuchinjia- Slaughter Slab.
Mtu akiwezesha au akifanya kinyume na utaratibu wa Sheria na Kanuni hizi anakuwa ametenda kosa na mtaalam atachukua hatua ya kisheria ambapo nyama husika itaharibiwa kwa utaratibu ulioelekezwa kwenye miongozo na mhusika atalipa faini ya Tsh. 1,000,000 au kifungo cha cha miezi sita au vyote.
Andiko la:
Dr. Benezeth lutege Malinda
Kaimu Mkurugenzi Huduma za Mifugo Tanzania
Pia soma
- DOKEZO - Mamlaka ziko wapi? Machinjio ya Vingunguti karibia ng'ombe 100 wanapotea kila siku kwa uzembe wa kuchinja ng'ombe wenye mimba