Don Carlo Ancelotti, Kocha pekee mwenye record zake UEFA

Mnyunguli

JF-Expert Member
Dec 21, 2020
1,772
4,457
Naam kama ilivyokuwa kwa Cristian Ronaldo(Cr7) bingwa mara 5 wa UEFA champions league akiwa kama mchezaji hadi kupelekea kupewa jina la utani KING OF UEFA basi ndivyo kwa Don carlo kwake imekuwa ni kocha pekee aliyechukua kombe hilo mara sita.Yes mara nikimaanisha mara mbili akilibeba kombe hilo kama mchezaji na mara nne akilibeba kombe hilo kama kocha.

Kuhusu haiba yake ya utulivu na kuto panic Don Carlo aliulizwa kwanini unaonekana hupendi kushangalia kwa mizuka akijibu ameshakutana na matokeo mengi sana ya kushangaza kwenye soka

Don Carlo mwenye miaka 64, umri wake na ujuzi anaoonesha kwenye soka hakika ni mambo tofauti kabisa kwani amekuwepo katika vipind viwili tofauti vya soka la zamani ni hili soka la siku hizi linaloitwa modern football.Makocha wengi wa umri wake wameshatundika daruga na kwenda kulea wajuu zao lakini mkongwe Carlo yeye kwake imekuwa tofauti bado yupo sana kuwafundisha makocha vijana mbinu magic za soka.

Muitaliano huyu na kocha bora dunian mwaka 2006/07 na 2013/14 ameendelea kuonesha makali yake kwa kuchukua taji la laliga msimu huu huku akiwa kapoteza mechi moja pekee na pia kuiwezesha team yake ya Real Madrid kuingia fainal dhidi ya Borussia Dortmund wababe kutoka ujerumani hivyo kuwa na record ya kuingia fainal 6 za UEFA na katika kuwa bingwa katika fainali 4 kati ya tano alizocheza.

Carlo ancellot anabaki kuwa ndie kocha pekee aliyefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kwenye league bora zate ulaya nikimaanisha England akitwaa EPL mara moja na Chelsea, Spain Kitwaa LaLiga mara mbili na Real Madrid,Italy akitwaa Seria A mara moja na Acmilan, France akitwaa ndoo mara moja na PSG na ujerumani huku pia alikinoa kikosi cha Bayern Munich na kufanikiwa kutwaa taji moja la ligi

Don Carlo kocha asiye na mashaka na mbinu zake na kocha mtilivu sana awapo uwanjani ni miongoni mwa makocha saba duniani walifanikiwa kuchukua UEFA kama mchezaji na kama kcha

1.Don carlo kama mchezaji Ac milani 1989 na 1990,kama kocha2003 na 2007 akiwa Ac milan na 2014 na 2022 akiwa na miamba ya jijin spain real madrid

2.Miguel Muñoz 1956,1957,1958 kama mchezaji wa Real madrid na 1960 na 1966 kama kocha Real modrid

3.Giovani Trapattoni 1963 na 1969 kama mchezaji Ac milan na kama Juventus kama kocha 1985

4.Johan Cruyff kama mchezaji wa Ajax 1971,1972 na 1973 na kama kocha wa kikosi cha Barcelona 1992

5.Frank Rijikaard kocha huyu fundi wa soka la kutwala mpira alicheza pamoja na Don carlo alitwaa UEFA kama mchezaji 1989,1990 akiwa Ac milan na 1995 akiwa na akax na kama kocha 2006

6.Pep Guardiola kama mchezqji 1992 na kama kocha 2009,2011 dhidi ya Barcelona na 2023 chini ya Man city.

7.Zinedine Zidane kama mchezaji wa Real madrid 2002 na kama kocha 2016,2017 na 2018.

Mataji mengine ambayo done Carlo yapo kwenye kabati lake ni 1.4X UEFA SUPER CUP WINNER,
2.2X SPANISH CUP,
3.2X SPANISH SUPER CUP,
4.2X German super cup winner
5.1x ITALY SUPER CUP WINNER
6.1X English SUPER CUP WINNER
7.1X ENGLISH CUP WINNER
8.1X ITALY CUP WINNER
9. 1X ENGILISH FA CUP WINNER
10.3X FIFA WORLD CUP WINNER

Tuzo binafsi kubwa.
1.1x UEFA kocha bora wa mwaka
2.2x kocha bora wa mwaka
3.2xKocha bora duniani

Usichojua ni kwamba haya yote ni sawa na upande mmoja wa shilingi kuhusu Don Carlo.

Kwangu Don Carlo atabaki kuwa kocha bora wa muda wote kwa mbinu zake za kumuheshimu mpinzani na kufukuza mwizi kimyakimya.

NB.Nimetest mitambo leo fani ya uandishi sio mchezo inahitaji utulize kichwa/Ndonga.
images (20).jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom