Dodoma: Ukandamizaji wa polisi waanza BAVICHA

Sioni umuhimu WA kuwapeleka kizimbani hao
Wazuiliwe police ikibidi hata mwezi
Maana hawana adabu
 
Waachwe kama mwezi ili wajionee hali ilvyo ndani ya mahabusu yetu na wakitoka watueleze mapungufu yaliyomo ili maboresho yafanyike.
Wasiwe na haraka ya kuomba dhamana, ni mapema sana, kuomba dhamana kwani hao ni makamanda tunaowategemea mstari frontline.
 
Sioni umuhimu WA kuwapeleka kizimbani hao
Wazuiliwe police ikibidi hata mwezi
Maana hawana adabu
Ndio akili ndogo hizi,watanzania tuna safari ndefu!Cha kwanza ambacho kingefanyika ni kutoa elimu kwa wapumbavu kama wewe!
 
Ndio akili ndogo hizi,watanzania tuna safari ndefu!Cha kwanza ambacho kingefanyika ni kutoa elimu kwa wapumbavu kama wewe!

Kuna mpumbavu zaidi yako
Kama huna Elimu ni wewe na hasara kwa mzazi wako
 
Kuna ******** zaidi yako
Kama huna Elimu ni wewe na hasara kwa mzazi wako
Sioni uhusiano wa elimu ambayo unasema unayo na comment yako!Kiufupi wewe hujaelimika!Au vinginevyo ni njaa ndio zinakufanya uwe hivyo!
Wewe ni hasara!
 
JESHI la polisi mkoa wa Dodoma limedaiwa kuingia katika ukandamizaji na uonevu baada ya kushindwa kuwafikisha mahakamani viongozi wa wakuu wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) ndani ya saa 24 kama sheria inavyotaka, anaandika Dany Tibason, Dodoma.

Badala yake jeshi hilo limemsingizia mwendesha mashitaka wa serikali kwa madai kwamba alikosekana kuandaa hati ya mashitaka na kulazimika kuiandika upya jambo lililosababisha kuchelewa kwa muda wa kuwapeleka watuhumiwa mahakamani.

Kauli hiyo ilitolewa Lazaro Mambosasa Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma, alipokuwa akijibu maswali ya mwandishi wa habari hizi kwa kutaka kueleza ni kwanini watuhumiwa hao hawakuweza kufikishwa mahakamani kama alivyokuwa amehaidi yeye wakati akizungumza na waandishi wa habari kuwa watuhumiwa hao wangefikishwa mahakamani siku ya jumatatu.

“Hao watuhumiwa hawatafikishwa leo watafikishwa kesho,na kilichosababisha kutofikishwa mahakanani ni kutokana na mambo ya kisheria kidogo ambayo yanatokana na mwandaaji wa mashitaka ambaye ni mwanasheia wa serikali.

“Sisi kila kitu tulishamaliza na mahojiano tulisha maliza lakini mwandaji wa mashitaka aliandaa hati ya mashitaka(chaji) lakini alikosea na kulazimika kuirudia na ndipo muda ukawa umepita na ndiyo sababu ya kutoweza kuwafikisha mahakamani.

“Kuhusiana na suala la dhamana kesi hiyo haina dhamana tusubiri huko huko mahamani” alisema Mambosasa.

Kuhusiana na tukio la watumuhiwa hao kutenganishwa katika mahabusu alisema kuwa hilo ni jambo la kawahida kwa watu wenye kesi inayofanana kutenganishwa na jambo hilo halina tatizo yotote.

“Ni jambo la kawaida sana kwa watu waliokamatwa kwa kosa moja ili uweze kufanya mahojiano ni lazima uwatenganishe na jambo hilo siyo kwao tu ni jambo la kawaida kwa watu wote” alisema Mambosasa.

MWANAHALISIONLINE limeambiwa kuwa viongozi hao wakiwa rumande jeshi la polisi liliwafanyia upekuzi katika vyumba vyao walipofikia Katika nyumba ya kulala wageni ya Drive Inn, waliwatenganisha watuhumiwa hao kwa kuwapeleka katika selo ya Chamwino Ikulu iliyopo wilayani Chamwino.

Waliopelekwa katika selo ya Chamwino ni Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa Patrobas Katambi,Mjumbe wa Baraza Kuu BAVICHA,Joseph Kasambala na Mwenyekiti wa BAVICHA mkoa wa Mbeya George Tito, huku Katibu wa BAVICHA taifa Juliusi Mwita akiwa ameachwa katika kituo cha polisi cha kati.

Viongozi hao ambao walikamatwa tangu siku ya Ijumaa kuamkia jumamosi wiki iliyopita hadi jana jumatatu wameendelea kusota rumande kwa kukosa dhama.

Vingozi hao walikamatwa wakiwa katika wakiwa katika Bar ya Cape Town wakiwa wanapata chakula na vinywaji huku wakiwa wamevalia fulana ambazo lilikuwa na ujumbe ambao ulikuwa ukisomeka Mwl .Nyerere Demokrasia inakanyagwa huku mbele kukiwa kuna maandishi ambayo yalikuwa yameandikwa kuwa AMANI = HAKI.

Kwa upande wake Kaimu wa Mwenyekiti wa BAVICHA , Taifa, Patrick Ole Sosope,alisema amesikitishwa na kitendo cha jeshi la polisi mkoa wa Dodoma kushindwa kuwafikisha mahakamani viongozi hao huku wakirushiana mpira kati ya jeshi hilo na mwanasheria wa serikali.
Weka lock up hao wazururaji peleka wakapalilie mashamba ya zabibu ili walipie chakula cha sero... safi sana leo hata mzee wa kubadilishia gia angani amewakana.
 
Back
Top Bottom