Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,786
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson ametangaza kifo cha Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Dk Shogo Mlozi.
Spika Tulia ametangaza kifo hicho leo Alhamisi June 13, 2024 kabla ya kuanza kwa kikao cha 46 cha mkutano wa 15 wa Bunge la 12 Bungeni Jijini Dodoma ambapo amesema taarifa zaidi zitatolewa baadaye.
Dkt. Tulia amesema ““Leo asubuhi tumepokea taarifa kwamba Mh. Dkt. Shogo Richard Mlozi ambaye tulimchagua kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki hatunae tena, hii ni taarifa ya awali tutakapopata taarifa za ziada tutawataarifu tusimame kaa dakika moja tumpe heshima zake za mwisho”
Pia soma Mhe. Dkt. Shogo Mlozi Ashiriki Semina ya EALA Women Caucus Bujumbura