Dkt. Philip Mpango, Mungu ni mtenda miujiza, anaweza kuponya na ana nguvu. Maombi ni silaha inayopaswa kuheshimiwa

Mganguzi

JF-Expert Member
Aug 3, 2022
1,453
3,517
Nilimsikia isdor mpango akikemea jambo kuhusu viongozi wa dini. Namuunga mkono. Alienda mbali zaidi kwa kusema viongozi wa dini Wanawaaminisha watu kwamba mungu anaweza kuponya magonjwa yao ama kutatua shida zao kupitia maombi na kwamba wanaongopewa na kutoa onyo kwa viongozi wa dini.

Nampongeza kwa kutoa kauli ya kwanza lakini kwamba watumishi wa mungu wana waaminisha watu kupona kupitia maombi amekosea. Biblia ndivyo inavyosema mtaweka mikono kwa wagonjwa nao watapata afya Marko 16:17-18, (wakisha kufanya yote haya wakafukuza Pepo wengi, wakawapaka mafuta wagonjwa wengi na kuwaponya Marko 6:13)na mtu wa kwenu akiwa hawezi na awaite wazee wa kanisa nao wataweka mikono juu yake na kumpaka mafuta nae atapata uponyaji)

Hivyo ni vielelezo vidogo tu kumwambia ndugu Philip kwamba Mungu anaponya, Mungu anaweza kufukuza Pepo wa umaskini na kuondoa laana za watu, hata kushika mic unaweza ukashindwa mungu akitaka. Ipo saa inakuja mambo yatageuka mtaenda kuwatafuta hao hao watumishi mnaosema ni wezi na wanajilimbikizia mali. Mlitaka watumishi wawe maskini?

Kwanini nyinyi mnalipana mishahara mikubwa na posho kibao kwa pesa za haohao maskini na kutembelea mashangingi na misafara ya magari kwa pesa za hao hao maskini? Leo mnawaonea huruma maskini wanapotoa sadaka kanisani kwanini msiache kuwalipisha Kodi kama mnawapenda maskini wa nchi hii? Mnachukua Kodi hata mchicha leo unasema maskini wanaibiwa na maaskofu?

Imani potofu hazijaanza leo tangu na tangu hata dini na makanisa yakifungwa yote Bado Imani potofu zitakuwepo! Msiwaite watumishi kwa ujumla wao kwamba ni matapeli kamateni hao mnaodhani ni matapeli wadunguliwe mashtaka sio kukejeli mungu na Imani za watu.

- Dkt. Mpango: Wahubiri wa dini wanajilimbikizia mali
 
Hao viongozi wa dini wakiumwa wanaenda kutibiwa mahospitalini na bima kubwa kubwa tuu afya. Ni vipi wasijiponyeshe?.
 
Matapeli wamejaa huko kutumia Ujinga na Umaskini wa wabongo.....
Uko sahihi sana chief! Hata hivyo, usiyaruhusu haya mawazo yako manyonge bila ya kufanya utafiti kuthibitisha hiki usemacho

Bila utafiti unaothibitisha bayana ya jambo, huna budi kulipinga mkuu

Mimi naamini Mungu yupo na anaponya wenye mwelekeo wake na siyo watu dizaini yenu
 
Hao viongozi wa dini wakiumwa wanaenda kutibiwa mahospitalini na bima kubwa kubwa tuu afya. Ni vipi wasijiponyeshe?.
Kwani daktari akiumwa anajiponyesha? Kwani viongozi wa dini Kuna mahali wamezuia watu wasiende kutibiwa mahospiralini ? Au unadhani hao wanaoenda kuombewa hawajui kwamba Kuna hospital ??
 
Kwani daktari akiumwa anajiponyesha? Kwani viongozi wa dini Kuna mahali wamezuia watu wasiende kutibiwa mahospiralini ? Au unadhani hao wanaoenda kuombewa hawajui kwamba Kuna hospital ??
Ina stress sana, Kunywa maji kisha upumzike
 
Uko sahihi sana chief! Hata hivyo, usiyaruhusu haya mawazo yako manyonge bila ya kufanya utafiti kuthibitisha hiki usemacho

Bila utafiti unaothibitisha bayana ya jambo, huna budi kulipinga mkuu

Mimi naamini Mungu yupo na anaponya wenye mwelekeo wake na siyo watu dizaini yenu
Umewahi kuniona sehemu yoyote ukaijua dizaini yangu ? Wa dizaini yako wapoje mkuu tuelekeze
 
Mwamposa akiugua anaenda kutibiwa marekani, masanja akiugua chap aghakhan yeye na familia yake, wewe ukiugua akakuwekee mikono ati utapona,. Ujinga uliokothiri
 
Mwamposa akiugua anaenda kutibiwa marekani, masanja akiugua chap aghakhan yeye na familia yake, wewe ukiugua akakuwekee mikono ati utapona,. Ujinga uliokothiri
Kwa hiyo huko aghakhan ndio Kuna mungu wako ? Au unaiona aghakhani na muhimbili ndio Pepo yako ,ni wangapi wanaenda aghakhan na India na wanarudi maiti sema nini upagani utakuua nahiyo mikobazi yenu
 
Mwamposa akiugua anaenda kutibiwa marekani, masanja akiugua chap aghakhan yeye na familia yake, wewe ukiugua akakuwekee mikono ati utapona,. Ujinga uliokothiri
Kwa hiyo huko aghakhan ndio Kuna mungu wako ? Au unaiona aghakhani na muhimbili ndio Pepo yako ,ni wangapi wanaenda aghakhan na India na wanarudi maiti sema nini upagani utakuwa na mikobazi
 
Kwa hiyo huko aghakhan ndio Kuna mungu wako ? Au unaiona aghakhani na muhimbili ndio Pepo yako ,ni wangapi wanaenda aghakhan na India na wanarudi maiti sema nini upagani utakuua nahiyo mikobazi yenu
Mbona watu wanaombewa na wanakua maiti kama kesho yake
 
Mbona watu wanaombewa na wanakua maiti kana kesho yake
Kifo kipo popote kama siku yako imefika lakini akili isiwategemee wanadamu kuliko mungu ! Kuna mahali elimu na uwezo wa mwanadamu unafika mwisho ! Hujawahi kuuguza mgonjwa hospitali wakasema tumeshindwa mludisheni nyumbani ? Inawezekana hujawahi kuugua au kuuguza ile kisawa sawa namuomba mungu akuonjeshe uugue mpaka uchakae ila usife ili uje siku Moja ukiri kwa kinywa chako kuwa mungu ni mkuu
 
Kifo kipo popote kama siku yako imefika lakini akili isiwategemee wanadamu kuliko mungu ! Kama mahali elimu na uwezo wa mwanadamu umefika mwisho ! Hujawahi kuuguza mgonjwa hospitali wakasema tumeshindwa mludisheni nyumbani ? Inawezekana hujawahi kuugua au kuuguza ile kisawa sawa namuomba mungu akuonjeshe uugue mpaka uchakae ila usife ili uje siku Moja ukiri kwa kinywa chako kuwa mungu ni mkuu
Tumesema watu wakiugua waende hospital kutibiwa sio kwenda kuwekewa mikono na wapigaji eti watapona
 
Tumesema watu wakiugua waende hospital kutibiwa sio kwenda kuwekewa mikono na wapigaji eti watapona
Imani ndio tatizo lako ila nimemuomba mungu akuonjeshe machungu ya hospital ! Uone waliohospital wanavyotoloka kwenda kuombewa naomba hili mwaka huu kwako ili hicho kiburi kiishe
 
Imani ndio tatizo lako ila nimemuomba mungu akuonjeshe machungu ya hospital ! Uone waliohospital wanavyotoloka kwenda kuombewa naomba hili mwaka huu kwako ili hicho kiburi kiishe
Unamuomba nani huyo wakunionesha? Hakuna wa kukuombea upone maradhi au upate kazi Wala utajiri hayupo, huyo anaekuombea anakua anakutapeli mchana kweupe
 
Na wanaotoroka hospitali kwenda kuombewa wanakua wamechanganyikiwa, au ugonjwa unakua upenda kichwani
 
Back
Top Bottom