Dhana ya future Buddha(milefo) katika Buddhism

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,730
729,900
Unaposoma maandiko ya Buddhism kuna mabudda wa aina mbalimbali
Kuna
Sakyamuni Buddha(Sidharta Goutama) Buddha mkuu
Kuan ing pusa(Buddha with a thousand hands
Milefo (future Buddha)
Ni kama aina fulani hivi kama ya utatu mtakatifu kwenye imani za kikristo...hivyo ndani ya Buddhism wanaamini katika ujio wa budha mwingine ambaye atakuja baada ya kalpa kadhaa(kalpa moja ni sawa na ukubwa wa jiwe la maili tano limogolewe kipande kidogo kila baada ya miaka mitano hata liishe)
Ukiichunguza sana hii dhana ya Milefo(Buddha ajaye)haina tofauti na dhana ya ujio wa Kristo kwenye imani za kikristo
Hakuna imani inayokosa utata na huu ni utata kwenye Buddhism pamoja na kujinasibu kusimama kwenye uhalisia na nafsi
Tuna watu wa kuvutika na mafundisho fulani, sio jambo baya jifunze lakini mwisho wa siku baki na msimamo wako mmoja! Hakuna dini inayokosa utata hakuna imani inayokosa ukakasi, ukiwa mtu wa kurukaruka utaishia kuchanganyikiwa
Future buddha/milefo/happy budha ni kitu cha kufikirika...Kalpa pia ni kitu cha kufikirika, jifunze haya mambo penye utata achana napo pasikuzuie kusoma ya mbeleni
 
Nilijiunga kwenye subscription moja HV.......natumiwaga emails na kundi linalojiita budhism.... Linaeleza Sana mambo ya meditation na mambo mengine kibao. Emails zao ni nzuri na wanazituma Mara moja kwa wiki. Waliwahi kunitumia huyo Jamaa lakini mpaka na Leo ndo nimekuja kujua maana yake.
 
Mkuu hao Budda ni viumbe vilivyowahi kuishi kama wanadamu au wao waliumbwa hivyo hivyo mkuu? fafanua kidogo mkuu
 
Yupi huyu Milefo?
 
Ndiyo mkuu!
Happy Buddha mpenda kula inaaminika kuwa kuna wakati utafika watu wote watakuwa na furaha baada ya kujifunza kuielewa na kuikubali Buddhism ndio hapo dunia itakuwa sehemu ya furaha amani na upendo...kimbembe ni huo muda
 
Mkuu hao Budda ni viumbe vilivyowahi kuishi kama wanadamu au wao waliumbwa hivyo hivyo mkuu? fafanua kidogo mkuu
Buddha ni mmoja tu Sidharta Goutama ambaye ndie mwanzilishi wa hii imani hawa wengine wote ni wa kufikirika zaidi kuliko uhalisia
Kuna masanamu mengi ndani ya Buddhism na kila moja lina jina na kazi yake
 
Buddha ni mmoja tu Sidharta Goutama ambaye ndie mwanzilishi wa hii imani hawa wengine wote ni wa kufikirika zaidi kuliko uhalisia
Kuna masanamu mengi ndani ya Buddhism na kila moja lina jina na kazi yake
Kwa hiyo mkuu huyo Sidharta Goutama alikuwa binadamu kama sisi?
 
Kwa hiyo mkuu huyo Sidharta Goutama alikuwa binadamu kama sisi?
Yeah alikuwa mtoto wa mfalme aliyeiahi maisha yake yote ndani ya kasri akipata raha zote mpaka siku moja alipotoka nje ya kasri na kuona mateso ya watu wa kawaida wenye njaa wagonjwa nk
Ndipo alipoamua kutoka nje ya kasri akayaacha yote mema na kuamua kwenda kutafuta chanzo na ukweli wa mateso ya binadamu na suluhu yake
Alifanya meditation kwa miaka saba mpaka alipofunuliwa(enlightenment)ndio akaja na imani hii ya Kibudha
 
Kwa hiyo wanamchukilia kama nani? Mungu au malaika ?
 
Kwa hiyo wanamchukilia kama nani? Mungu au malaika ?
Another contradiction is here...kwao Buddha ni inspirational figure ni mwalimu mkubwa (shifu/master)kiongozi, wanakataa kumuabudu ila kiuhalisia wanamwabudu.. .ni waabudu sanamu Buddhism inapotoka kuwa phylosophia na kuwa imani
Wana ibada pia za ajabu linapokuja swala la imani...ikiwemo ibada ya utajirisho kwa kuchoma pesa live lakini kwa siri
 
Noted mkuu, ndo maana kuna duka moja la hawa wenzetu waasia nilishona kuna kijumba ndani yake kuna sahanmu ina mikono kibaoo
 
Noted mkuu, ndo maana kuna duka moja la hawa wenzetu waasia nilishona kuna kijumba ndani yake kuna sahanmu ina mikono kibaoo
Mabuddhist wengi ndani ya nyumba zao na kwenye biashara hupenda kuweka hizi shrine na kuweka vyakula au chochote kabla hawajatumia wenyewe
 
Nini mtazamo wao kuhusu kifo I,e do they believe in life after death..?...na dhambi kwao ni nini mkuu.
 
Mafundisho ya Budha yapo katika buddhasutra.com. Ukisoma,utaona kwamba it is unlike anything you have ever seen. Anaongea in a very repetitive style. Hiyo ni dharma. Bado ipo vinaya,lakini vinaya in full sijui inapatikana katika website gani.
 
Zipo aina mbili za Budhism. Hinayana na Mahayana. Zinaweza kujadiliwa but now is too late an hour. We can discuss it tomorrow. Sasa hivi tuseme kwamba yule Budha mnene,Ho tai,ndie budhists wanamtazama sanamu yake wanapotafakari kuhusu wealth.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…