1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 6,954
- 9,180
Mazuri yote aliyoyafanya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete yameanza kuyeyuka kama dheluji inayokabiliana na tanuri la moto. Dhambi ya madudu ya bandari haiwezi kumuacha Rais Mstaafu, Kikwete. Dhambi hii imeanza kuyafuta yale yote mazuri aliyoyafanya katika utawala wake!
Rais Kikwete amefanya mambo mengi ya maendeleo pamoja na kwamba kwa kiasi kikubwa msingi wake ni mikopo na misaada. Ikumbukwe Mwaka 2005 deni la taifa lilikuwa shilingi trilioni 10. Leo miaka 10 katika utawala wa Rais Kikwete, limefikia karibia Shilingi trilioni 40.
Yaliyotokea/yanayotokea bandarini yanadhihirisha sababu ya ukuaji wa uchumi wetu kushuka chini. Mwaka 2005, uchumi wetu ulikuwa unakuwa kwa asilimia 6.7 lakini leo umeshuka hadi wastani wa asilimia 6.4. Mbaya zaidi hata huu ukuaji wa uchumi haunufaishi wananchi wengi.
Uchumi uliopo siyo uchumi shirikishi ambao utawanufaisha wananchi wengi. Uchumi uliopo unawanufaisha watu wachache ambao msingi wa utajiri wao ni wizi na ukwepaji kodi.
Uchumi hauwezi kukua wakati maelfu ya makontena/bidhaa zinapita bandarini bila kulipiwa ushuru. Bidhaa hizo pia zimechangia sana katika kuharibu soko (negative price distortion) matokeo yake hata viwanda vyetu vya ndani ya nchi vinashindwa kupambana kwenye soko katika usawa . Bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi zinakuwa aghari kulinganisha na bidhaa nyingi kutoka nje kwa sababu zinakuwa hazijalipiwa ushuru.
Athari hii imesababisha viwanda vingi kuwa ni magofu au magodauni ya kupokea bidhaa kutoka nje ambazo nyingi zinakuwa hazijalipiwa ushuru. Kwa nini nihangaike kuzalisha bidhaa hapa nchini wakati ninaweza kuagiza nje ya nchi na kuziingiza nchini bila kulipia ushuru as a result, ninakuwa na uamuzi mpana kwa kuamua bei ya bidhaa ukilinganisha na yule anazalisha hapa nchini.
Kubwa zaidi, kabla ya serikali haijaanza kuwalalamikia wale wamegeuza viwanda kuwa magodauni, lazima nayo pia ijitazame kwa sababu imekuwa ni chanzo cha viwanda vya ndani kushindwa kukabiliana na soko la ndani.
Serikali inatakiwa kwanza itengeneze mazingira sawa katika soko kabla ya kuanza kuwawajibisha waliogeuza viwanda kuwa magodauni.
Jakaya Kikwete alikuta mnakusanya Billioni 250 akawapeleka kwenye trillioni moja za kodi kama hamna cha kumkumbuka basi nyie wepesi wa kusahau na wachoyo wa fadhila!
Wakati huo wa awamu ya tatu ya mzee Mkapa US dola moja ilikuwa sawa na Sh 450 - 600.
Kilo ya nyama ilikua sh 2000.
Sukari 1kg sh. 450- 500.
1 Kg ya Unga wa sembe sh 180 - 200/-
Lita moja ya mafuta ya taa ilikua sh.400- 500.
JK ameondoka madarakani US $ ikiwa sawa na Tsh 1800 - 2200.
Kwa hiyo ukipiga mahesabu ya uwezo wa kulipa madeni wakati wa mkapa na wakati wa JK utagundua kua makusanyo wakati wa JK yalishuka sio kupanda.
Kwa hesabu rahisi ni kwamba wakati wa Mkapa kila sh. 1000/= iliyokusanywa ilikua na uwezo wa kulipa dola 2 kwenye madeni ya nje.
Ambapo mpaka Kikwete anaondoka madarakani Kila sh.4000/= za makusanyo ya pato la nchi ndiyo iliyokua na uwezo wa kulipa dola 2 za kimarekani.
Kwa hiyo ilibidi JK akusanye tsh tril.1.5 ili aweze kuwa sawa na bil 350 za enzi za Mkapa.
Kwa makusanyo ya tr.1 za JK alikua ameshuka sana kutoka na kuzidiwa na wakwepa ushuru kuongezeka kwa kasi huku deni la taifa likipaa na matumizi ya serikali kuwa juu muda wote wa sanaa ya uongozi wake.
Last edited: