Desemba 25: Je, ni siku aliyozaliwa Yesu au twaadhimisha tu kumbukumbu?

Mkristo wa 'KICHINA' 25th Dec SIO BIRTHDAY YA YESU acha kukariri mambo,ni siku ambayo wakristo hukumbuka kuzaliwa kwa Bwana YESU karibia miaka 2000 iliyopita.Ingekuwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa YESU isingetumika neno'karibia miaka...' ingekuwa unatajwa Umri husika wa YESU.Kama huamini kwamba YESU alizaliwa then huna sababu ya kukumbuka tendo hilo,pia unaweza kuchagua tarehe nyingine na mwezi mwingine kama unafikiri kweli Yesu alizaliwa nawe ufanye hiyo kumbukumbu.Wengi hawaelewi kuwa kesho sio bethdey ya yesu...

Kwa hiyo unakiri kwamba Yesu hakuzaliwa tarehe 25-12.
 
okey mie cna comment, najua wote mlio coment hapo juu mna itikad ya kidini huwez ukaponda matakwa ya dini ya mtu mwngne hata kama ni mpagan yanakuhusu?, mnajifanya mmeiva kwny dini kumbe hamna lolote.fanya mambo ya maendeleo mwombe mungu wako akuxaidie cyo uanze kushabkia udin na hasa nyie watu wa upande wa pili.
 
WANAJF;
Nafahamu kwamba wapo wale watakaonibeza lkn hata Biblia inatuambia kwamba siku ile ATAKAPORUDI BWANA WETU YESU KRISTO KUWACHUKUA WATEULE WAKE kwenda nao MBINGUNI, hakutakuwa na sababu Ohooo mimi sikujua wala mimi nilikuwa naambiwa tu Viongozi wangu wa DINI (ambao naamini hata ukiwauliza kuhusu hii Kristmas watakosa Jibu la kukuambia, labda itakuwa ni Propaganda tu zisikokuwa na support ya kwenye Biblia Matakatifu). Na Biblia iko wazi zaidi kwa kusema.


malaika na wachungaji walisheherekea kuzaliwa kwa yesu wakiwa wanajua kazaliwa kwenye zizi la ng'ombe.

luka 2: 11 maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana. 12 Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng'ombe.13 Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema,14 Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.15 Ikawa, malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya, na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika, alilotujulisha Bwana.16 Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini.17 Walipomwona wakatoa habari waliyoambiwa juu ya huyo mtoto.18 Wote waliosikia wakastaajabu kwa hayo waliyoambiwa na wachungaji.19 Lakini Mariamu akayaweka maneno hayo yote, akiyafikiri moyoni mwake.20 Wale wachungaji wakarudi, huku wanamtukuza Mungu na kumsifu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona, kama walivyoambiwa.

mathayo 2:11 Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane.

Guess what!! hata ibrahimu alishekherekea pia.

yohana 8: [FONT=Arial, Helvetica, Geneva, sans-serif]55[/FONT] Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.

sasa dhambi ya kushehereka siku ya kuzaliwa masiha iko wapi na ni wapi alikataza kwenye bibilia kuwa atawahukumu wale watakaosheherekea?

, kilichofanyika hapa ni kuiweka wakfu siku ya tarehe 25 decemba kama siku ya kuadhimisha kuzaliwa kuja kwa masihi ulimwenguni.
 
Mkristo wa 'KICHINA' 25th Dec SIO BIRTHDAY YA YESU acha kukariri mambo,ni siku ambayo wakristo hukumbuka kuzaliwa kwa Bwana YESU karibia miaka 2000 iliyopita.Ingekuwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa YESU isingetumika neno'karibia miaka...' ingekuwa unatajwa Umri husika wa YESU.Kama huamini kwamba YESU alizaliwa then huna sababu ya kukumbuka tendo hilo,pia unaweza kuchagua tarehe nyingine na mwezi mwingine kama unafikiri kweli Yesu alizaliwa nawe ufanye hiyo kumbukumbu.Wengi hawaelewi kuwa kesho sio bethdey ya yesu...
ha ha ha ha ha, thank you for further clarification
 
Ndo maama huwa nasemaga zitapita makanisa yote ila RC litabaki.....point ya msingi ni kwamba 25 dec ni siku kuu ya mungu jua ambayo ilikuwa inasheherekewa na watu wa roman empire miaka mingi ilopita...kwanin 25 dec...ni kwamba...kwa wale waliofika atleast form two katika elimu yao wanaweza kulielewa hili..jua huwa lautosi tropic of kapricon tar 22 dec...katika kipindi iki mwanga huwa hafifu sana katika northen hemisphere hivyo wanaamini kuwa mungu jua amezidiwa nguvu na mungu wa giza....ila inapofika tar 23 24 mpaka 25 mwanga huwa unaanza kuongezeka katika maeneo hayo kwa vile jua huwa linaanza tena kurudi kuelekea juu hivyo wanasema mungu jua kashinda na ameregain his power....ukiangalia siku ambazo jua huwa limeadimika kule ni almst siku tatu...ni siku izo izo ambazo yesu nae alikuwa kaburin kabla ya kufufuka...kwanini katholic litasimama daima...bible kama inavoonekana leo ni kazi ya kanisa katoliki...miaka ya 1200 kuna mijadala mizito ilifanyika na kanisa katika kuamua vitabu vipi viwepo na vipi visiwepo kwa sababu moja au nyingine...ndo maana chanzo kikubwa cha mafundisho ya wakatoliki ni kotoka kwenye bible...roho mtakatifu na from mapokeo...mapokeo yanainclude vile vitabu ambavyo havijakuwa cooporated kwenye bible..makanisa mengine hawavijui wanategemea bible tu ilioundwa na wakatoliki..think deep...unadhani mtume mkubwa kama petro hana maandiko yake kuhusu yesu...mpaka injili ije kuandikwa na luka na marko ambao hawakuwai kukutana na yesu hata kwa bahati mbaya....petro ana maandiko yake abt yesu..na mitume wengine pia ila kanisa limeyahifadhi kwa sababu mbalimbali...kuna mwenye swali

Hili ndio jibu; X mas ni sikukuu ya kipagani!
 
such google and write why utapata mawazo kwa other great thinkers ila 25 ni siku inaambatana na sikuku za anasa,ulevi na dhambi at one the countries in asia usiniulize ni ipi,pili alizaliwa kipindi cha hali ya hewa ipi?afu mwisho kwanini siku hiyo watu wajae bar,kumbi za starehe na si kanisani ?just fanya research i want to think more
 
MIMI NI MKRISTO NINAYE-AMINI KWAMBA YESU ALIZALIWA NA BIKIRA MARIAM, AKAISHI DUNIANI KWA KIPINDI CHA MIAKA 33, AKAUAWA NA KUZIKWA NA ILIPOFIKA SIKU YA TATU ALIFUFUKA NA KWASASA YESU MBINGUNI NA ATAREJEA TENA KUWACHUKUA WALE WALIO WATEULE WAKE KWENDA NAO MBINGUNI KAMA BIBLIA INAVYOSEMA.

HII HABARI YA WEWE SIYO MKRISTO AU WA KICHINA KWASABABU YA SWALI AMBALO HATAHIVYO BADO HAMJALIJIBU; JE NI KWANINI TUNASHEHEREKEA KILA MWAKA 25 DESEMBA KAMA SIKU YESU ALIYOZALIWA? JE HAYA YANAPATA SUPPORT TOKA WAPI WKT KWENYE BIBLIA TAKATIFU HAYAPO? -ungenijibu katika hilo ungekuwa umenisaidia sana, kama una evidence ya kwenye Biblia, otherwise unajaribu kukwepa ukweli kwamba tunasheherekea Matakwa ya Kibinadamu na wala si mpango wa Mungu; kwani vipaumbele vyote muhimu katika ukombozi wa Mwadamu (kazi aliyokuja YESU Duniani kuifanya) vyote vipo kwenye BIBLIA TAKATIFU.

Nafahamu kuna watu hawapendi kujadili mambo ya kiimani kwasababu zao mbali mbali lkn lililojema ni lipi? na ni kwanini tunaruhusiwa kuwa na BIBLIA TAKATIFU na kushauriwa kukisoma? Je kama wote tungekuwa wavivu au kutopenda kusoma Biblia Takatifu, Je Waakristo Waprotestant wangekuwepo leo hii bila Martin Luther kufanya jitihada na Kusoma Biblia na kuelewa yaliyomo?

Mimi nafikiri tusibezane kwa maneno ya kejeli ktk mambo muhimu kama haya; wewe kama una facts za kutufanya tushehereke leo Desemba 25 kama sikukuu ya Kuzaliwa Yesu Kristo, tupe hizo facts zinazotoka kwenye BIBLIA TAKATIFU.

Halafu pia, neno la Mungu lina utaratibu, na hasa Ukristo, hivyo huwezi kunishawishi kwamba ni suala la mtu yeyote kujisikia ni lini na siku gani anasheherekea Kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Hiyo dhana ya uhuru huo unautoa wapi kwenye Biblia takatifu? Labda unishawishi kwamba wewe Biblia haikuhusu, na kama ndivyo basi hili swala nalo halikuhusu; kwani hili suala ni kwa wale WAKRISTO AMBAO BIBLIA TAKATIFU NDICHO KITABU KITAKATIFU na taratibu na Msingi wa Imani yao ipo kwenye Biblia Takatifu.

NB; H1N1 na Mwafrikahalisi; tafadhali rejea mada yangu hapo juu na uone kiini cha hoja yangu.

Kama wewe ni Mkristo wa kweli basi katika maandiko yako ungeandika BWANA YESU na sio YESU tu kama ulivyofanya........ni wasio na imani naye hutomtambua kuwa ni BWANA
 
Leo nimeona ni vema nitoe majibu ya swali lililoulizwa na wakristo wengi juu ya chanzo cha sikukuu ya Krismas ya tarehe 25 Desemba.

Swali:
Ni nini Chanzo cha sikukuu ya Krismass ya tarehe 25 Desemba? Je ni kweli Yesu alizaliwa tarehe hiyo?

Jibu:
Wakristo wengi wanaamini kuwa Yesu hakuzaliwa tarehe 25 December, kwa sababu Mariamu alipata uja uzito kati ya Mwezi wa sita (Juni) mwishoni. Hivyo kama kawaida ya binadamu, ujauzito unachukuwa miezi tisa ili mtoto azaliwe, hivyo ni wazi Yesu alizaliwa majira ya mwezi wa Februali. Ila hakuna Andiko la Biblia wala Historia iliyoweka kumbukumbu ya tarehe ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

Kwenye Biblia tunaikuta tarehe 25 December, kuwa ni sikukuu iliyokuwa inasherehekewa na wapagani wa Babeli ambako Waisraeli walichukuliwa mateka. Hivyo sikukuu ya 25 Desemba ilikuweko kabla ya Kuzaliwa Yesu, na ilikuwa sikukuu ya wapagani wa Babebli wakisherehekea kuzaliwa kwa Mtoto wa Mungu JUA aliyeitwa TAMUZ.

Kulikuwa na Mfalme wa babeli aliyeitwa , na mke wake ambaye pia aliitwa Malkia wa Mfalme jina lake aliitwa baada ya Mfalme Nimrudi kufariki, Mke wa mfalme akabeba mimba nje ya Ndoa. Ili kuficha kitendo hicho cha mke wa mfalme kubeba mimba wakati mume wake amefariki, akatunga UONGO kuwa Mume wake HAKUFA ila alibadilika kuwa Jua (SUN), hivyo mionzi ya Jua wanayoiona ndiyo iliyomdunga Mimba. Wababeli kwa kuwa walikuwa waabudu mizimu waliamini Uongo huo na kuanza Kuliheshimu Jua (SUN) kama Mungu wao.

Usiku wa kuamkia Tarehe 25 Desemba, Semiramis akazaa Mtoto aliyemwita TAMUZ, ambaye baba yake ni Mungu Jua. Imani yao ilienda mbali zaidi hadi kuamini kuwa tendo la Semiramisi kuzaa na Mungu jua yeye pia ni Mungu Mke na Mtoto wao Tamuz akaitwa Mungwa Mwana. Kuanzia kipindi hicho wapagani wa Babeli tarehe 25 mwezi wa 12, waliweka sherehe kubwa ya kuzaliwa kwa Mungu Mwana Tamuz.

Biblia inatoa maelezo juu ya jambo hilo la kufanya sherehe ambayo mfalme aliitumia kufungua baadhi wafungwa, kama msamaha wakati wa sikukuu - Yeremia 52:31 "Hata ikawa, katika mwaka wa thelathini na saba wa kuhamishwa siku ya ishirini na tano ya mwezi, chake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, akamtoa gerezani."

Nabii Yeremia aliandika kitabu hicho zamani kabla ya Yesu kuzaliwa, taifa la babeli lilikuwa na Desturi ya kuweka huru wafungwa katika siku hii ya Kuzaliwa kwa Tamuz tarehe 25 Desemba. Enzi hizo haikuwa inaitwa Krismass huenda iliitwa Tamuz'Mass.

Baada ya Yesu kuzaliwa, hapakuwa na Sikukuu ya Krismass hata mitume hawakuwahi kusherehekea sikukuu hii, bali tunaona baada ya miaka mingi kupita karibia zaidi ya miaka 300 Mfalme Constatino wa Dola ya Kirumi aliyekuwa anaabudu JUA alimua kuwa Mkristo, lakini hakutaka kuacha Desturi za kuifanyia sherehe miungu yake. Hivyo akaamuru sherehe ya kuzaliwaMungu Mwana Tamuz iendelee kusherehekewa ila wakristo waambiwe kuwa ni siku ya kuzaliwa Yesu Kristokinachoitwa "The Compact History of Roma cathoric church" kinaeleza juu ya tangazo la Mfalme Constantino kwa wakristo kuanza kuadhimisha sikukuu za kipagani ikiwemo Ibada ya JUA ya siku ya Kwanza (SUN-DAY) badala ya Ibada ya Siku ya SABA, historia inaeleza kuwa alitoa maagizo hayo akiwa bado mpagani (Kabla ya kubatizwa), tangazo hilo lilitolewa mwaka 325AD.

Historia inasema, ilikuwa ni mwaka ndipo kanisa lilipoamua kwamba, ya kuwa na sikukuu ya kipagani mjini Rome ?€? au The Birthday of theinvincible/unconquered Sun, iliyosherekekewa tarehe , sasa tarehe hiyo iwe si kwa kuzaliwa jua, bali iwe siku ya kuzaliwa mwana (son) wa Mungu - Yesu Kristo. Kwa mara ya kwanza kanisa lilikuwa linaendesha Misa tu, lakini baadaye mtindo wa sherehe za kipagani ikaingizwa hadi leo inaendelea ikitawaliwa na Vinywaji (Vileo), Vyakula na starehe za kila namna.

MASWALI YA CHANGAMOTO:

1. Kwa nini Mungu hakuona haja ya kuwa na siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo? Hata hakuiweka wazi tarehe na siku ya kuzaliwa kwa Yesu?

2. Ilikuwaje Mitume na Kanisa la awali hawakuwa na wazo hilo la sherehe ya Krismasi?

3. Kwanini wakristo walazimishwe kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa Yesu katika tarehe ya Kuzaliwa Mwana wa Mungu JUA? Na mfalme ambaye wala hakuwa Mkristo wakati huo?

4. Kwa nini wakristo wasiweke Tarehe ya kwao ambayo inaendana na mwezi hata kama Tarehe haijulikani? Make miezi tisa kutoka June ni February / March.

MUNGU AWABARIKI WOTE MNAPOENDELEA KUTAFAKARI JUU YA UKWELI HUU UNAOTUSAIDIA KUKUA KIROHO.



Ev. Eliezer Mwangosi

Eliezer.mwangosi@yahoo.com
 
HISTORIA FUPI YA KRISMASI.

Krismasi (pia Noeli) ni sikukuu ambako Wakristo wengi husheherekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
Kwa kawaida husheherekewa tarehe 25 Desemba katika Ukristo wa magharibi na tarehe 6 Januari katika ule wa mashariki.
Kuna majina mawili yaliyo kawaida kwa Kiswahili kwa ajili ya sikukuu hii.

Krismasi inatokana na neno la Kiingereza lenye maana ya "Christ`s Mass" yaani misa au ibada ya Kristo.

Noeli inatokana na Kiingereza "Noel" (au "Nowell") ambako imepokewa kutoka lugha ya Kifaransa "noël". Hilo ni ufupisho wa Kilatini "Natalis (dies)", "(siku ya) kuzaliwa".

Historia ya Krismasi

Tarehe halisi ya kuzaliwa kwake Yesu haijulikani kwa sababu utamaduni waWayahudi wa wakati ule haukuwa na sherehe au kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa.

Lakini baadaye Ukristo ulienea katika Dola la Roma kati ya mataifa yaliyokuwa na kawaida ya kuzingatia siku ya kuzaliwa. Hivyo ilijitokeza hamu ya kusheherekea pia sikukuu ya kuzaliwa kwake Kristo. Ndiyo asili ya sikukuu ya Krismasi.

Tangu mwanzo wa karne ya 3 BK kuna kumbukumbu ya waandishi mbalimbali waliojadili tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo.

Habari za kwanza kabisa za makadirio ya tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu zinapatikana kutoka Misri mnamo mwaka 200. Mwandishi MkristoKlemens wa Alexandria alilalamikia udadisi wa wataalamu kadhaa wa Misri waliodai kwamba wamekadiria tarehe hiyo katika mwezi Mei, wengine katika Aprili. Alisema pia kuwa kikundi cha Kikristo cha wafuasi wa Basilides huko Misri walisheherekea Epifania pamoja na kuzaliwa kwake Yesu tarehe 6 Januari.

Labda kadirio la tarehe ya 25 Desemba pia lina asili katika Misri. Kuanzia mwaka 200 (kwa mara ya kwanza katika maandishi ya Sixtus Julius Africanus) tunasikia kwamba wataalamu wa Misri walifikiri tarehe 25 Machi ilikuwa tarehe ya kufa kwake Kristo na pia siku ya utungaji mimba wake. Kwa kuongeza miezi tisa ya mimba inajitokeza 25 Desemba kama tarehe ya kuzaliwa.

Inaonekana tarehe 25 Desemba ilijitokeza wakati huo. Kuna taarifa ya mwaka 204 kutoka Ipolito wa Roma kwamba tarehe 25 Desemba ilikuwa sikukuu ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo.

Krismasi na sikukuu ya Sol Invictus

Wataalamu mbalimbali walidai kwamba Kanisa lilipachika sikukuu ya Kristo kwenye tarehe hiyo kwa nia ya kuchukua nafasi ya sikukuu ya jua kama mungu "Sol invictus" (yaani "Jua lisiloshindika").

Lakini pengine mambo yalikwenda kinyume, yaani kwamba Makaisari walianzisha sikukuu hiyo, halafu wakaipanga tarehe ya Krismasi ili kushindana na Ukristo uliokuwa bado chini ya dhuluma ya serikali yao.

Aliyeingiza sikukuu ya "Kuzaliwa Jua" (Mitra) huko Roma ni Eliogabalus (kaisari kuanzia 218 hadi 222). Baadaye Aurelianus akaithibitisha rasmi mwaka 273, hatimaye ikahamishiwa tarehe 25 Desemba.

Wakati wa Licinius (308-324) sikukuu hiyo ilikuwa ikiadhimishwa bado tarehe 19 Desemba.

Kutoka Roma, uliokuwa mji mkuu wa Dola la Roma, sherehe ya 25 Desemba ilienea kote katika Ukristo.

Wakristo wengi husheherekea tarehe 25 Desemba (Wakatoliki na sehemu ya Waprotestanti naWaorthodoksi). Kati ya Waorthodoksi kuna tarehe nyingine, hasa 6 Januari kutokana na tofauti katikakalenda.

Habari za Krismasi katika Biblia

Habari za Krismasi kama sherehe hazipatikani katika Biblia kwa sababu zilizotajwa hapa juu.

Lakini hasa vitabu viwili vya Agano Jipya vina habari za kuzaliwa kwake Yesu, yaani Injili za Mathayo na Luka.

Mathayo anasimulia habari hizo katika mlango wa kwanza kuanzia aya 18 na katika mlango wa pili.

Bikira Maria alipata mimba wakati alipokuwa mchumba wa Yosefu. Yosefu alitaka kumwacha lakini aliambiwa na malaika aanze kuishi naye na kumkubali mtoto kama wake kwa kumpa jina "Yesu".

Mamajusi kutoka mashariki waliwatembelea na kuwaletea zawadi kwa sababu waliona nyota ya pekee iliyokuwa kwao alama ya kuzaliwa kwa mfalme mpya katika Uyahudi ikawaongoza hadi Yerusalemu. Lakini walipompitia mfalme Herode Mkuu, huyo alikasirika akimwogopa mfalme mpya. Hata hivyo aliwaelekeza Bethlehemu kadiri ya utabiri wa nabii Mika.

Yosefu alipata tena ujumbe kutoka kwa malaika akaondoka na mtoto na Maria kukimbilia Misri kabla ya askari wa Herode hawajaweza kumuua Yesu.

Baada ya kifo cha Herode walirudi kutoka Misri lakini hawakuenda tena Bethlehemu bali kuhamia Nazareti katika mkoa wa Galilaya.
Katika Injili ya Luka

Katika taarifa ya Luka (mlango wa 1 na 2) Maria alipokea huko Nazareti ujumbe wa malaika mkuu Gabrieli kwamba atapata mimba na mtotowa pekee.

Yosefu na Maria walikwenda Bethlehemu kwa sababu ya sensa iliyowataka kwenda katika mji asili wa ukoo wa Yosefu. Hapo Yesu alizaliwa katika hori la kulishia wanyama; wachungaji mabondeni walitangaziwa na malaika habari hiyo wakaja kumwona mtoto.

Baada ya kuzaliwa wazazi walimpeleka Yesu Yerusalemu katika hekalu kufuatana na sheria ya Agano la Kale (Kitabu cha Kutoka 13,2; 13,15) halafu wakarudi kwao Nazareti.

Kama kawaida, imani na liturujia ya Kikristo zinaitikia haja za binadamu.

Mojawapo ni kukutana na watu wa kupendeza kwa wema wao.

Kipindi cha Noeli kinatimiza haja hiyo, kwa kuwa kinaadhimisha kuzaliwa kwa mtu mpya kabisa ambaye anatuvutia kwa wema wake na ambaye tukimuona tumemuona Mungu, tena tukimpokea tunazaliwa upya kama wana wa Mungu.

"Leo amezaliwa kwa ajili yenu Mwokozi, ndiye Kristo Bwana".

Tunapoadhimisha Noeli tangazo hilo la malaika kwa wachungaji linatufikia sisi. Si kujidanganya, kana kwamba Yesu angezaliwa leo, wala hatukumbuki tu tukio la zamani, bali fumbo la kuzaliwa Bwana linatufikia leo katika liturujia na kutuletea neema zake. Hivyo tunaweza tukazaliwa upya kwa kushiriki kuzaliwa kwa kichwa chetu.

Liturujia inashangilia hivi, "Lo! Mabadilishano ya ajabu! Mwana wa Mungu anakuwa mtu kusudi mtu awe mwana wa Mungu!". Tena si binadamu tu, bali viumbe vyote vinapata heshima mpya kwa Neno wa milele kujifanya kiumbe.

Desturi za Krismasi
Sherehe ya Krismasi imekuwa sikukuu muhimu sana katika tamaduni za mataifa yaliyoathiriwa na Ukristo. Kuna desturi nyingi zilizojitokeza katika karne zote za kusheherekea Krismasi. Sehemu ya desturi hizi zimeenea pia nje ya nchi za asili na hata kutumiwa na watu wasiofuata imani ya Kikristo.

1. Pango la Noeli:
- Pango la Noeli lililoanzishwa na Fransisko wa Asizi mwaka 1223 kijijini Greccio (Italia) na kuenea kila mahali kama sanaa inayoonyesha kwa njia mbalimbali jinsi Yesu alivyozaliwa.

2. Mapambo ya krismasi:
- Ni hasa nuru na taa za pekee. Alama za nyota kwa kukumbuka nyota iliyopeleka mamajusi hadi Bethlehemuinawekwa ndani na nje ya nyumba na maduka.

3. Mti wa Krismasi:
- Ni ishara ya pekee ya Krismasi yenye asili katika Ujerumani kusini-magharibi ya karne ya 16 hivi. Asili yake iko katika maigizo yaliyosimulia hadithi za Biblia na mti wa Paradiso unaohusiana na masimulizi ya dhambi la kwanza na ujumbe wa Kristo kamamwokozi anayekuja kuondoa dhambi hilo. Kutoka maigizo ya kanisani ishara ya mti uliopambwa matunda uliingia katika nyumba za Wakristo ambako ulipambwa zaidi kwa matunda, keki tamu na pipi kwa watoto. Umekuwa mapambo ya nyumbani kwa majira ya Krismasi. Tangu Krismasi kuwa nafasi muhimu kwa uchumi kuna pia maduka mengi yanayoweka miti hii na katika mazingira ya kibiashara uhusiano wake na mti wa Paradiso umesahauliwa mara nyingi.

4. Zawadi za Krismasi
- Martin Luther alitaka kuongeza umuhimu wa Krismasi kwa Wakristo ambao wakati wake walikuwa na desturi ya kuwazawadia watoto kwenye siku ya Mtakatifu Nikolasi tarehe 6 Desemba, wiki 2 kabla ya sikukuu. Hapo Luther alipendekeza kuhamisha zawadi kwa watoto kwenda siku ya kuzaliwa kwake Yesu ili wamkumbuke zaidi Yesu kuliko mtakatifu huyo. Hapo alirejea zawadi zilizopelekwa kwa Yesu na mamajusi kutoka mashariki kufuatana na taarifa ya Injili ya Mathayo mlango 2.

Desturi ya kuwazawadia watoto kwenye sikukuu hii ilienea hadi kuwa desturi ya kupeana zawadi kati ya watu wa kila umri. Katika karne ya 20 desturi ilienea kiasi cha kuwa nafasi muhimu ya biashara. Katika nchi nyingi mwezi wa Desemba umekuwa mwezi wa mapato makubwa kushinda miezi mingine. Hata katika miji mikubwa ya nchi kama Dubai au Japani ambako Wakristo ni wachache desturi ya kupeana zawadi imeenea na mapambo ya Krismasi katika maduka yanataka kuwahamasisha wateja kununua zawadi za majira.

4. Baba Krismasi / Baba Sara Noeli
(Chanzo cha habari hii ni WIKIPEDIA)
Kuhusu Pango la Noeli, Baba Krismasi (Father Christmass), pamoja na baadhi ya mapokeo si Wakristo wote wanakubaliana na hayo mapokeo ingawa wengi huadhimisha kwa kukukumbuka kuzaliwa kwake Kristo Yesu Bwana na Mwokozi wetu.
Je! Nini hasa maana ya siku hii katika maisha yetu ya leo?

Krismasi maana yake ni ishara ya wokovu wa mwanadamu. Krismasi haimaanishi kula, kunywa, kuvimbewa, wala kupumzika majumbani pamoja na familia zetu. Krismasi - Ibada ya Yesu (kuzaliwa kwa Bwana Yesu) ni ishara ya WOKOVU kwa wanadamu. Krismasi ni ishara ya UKOMO WA DHABIHU ZA WANYAMA ambao walitumika kuleta utakaso kwa watenda dhambi. Krismasi ni ishara ya UPENDO MKUU wa Mungu kwa watu wake waliopotea; kwa maana amewapatia msamaha wa dhambi bure. Krismasi ni ishara ya ushindi dhidi ya Shetani na majeshi yake kwa maana Yesu ni Bwana wa mabwana, Jemedali wa vita, Mungu mwenye nguvu, Mungu wa miungu, Mfalme wa amani, na Ndiye Alfa na Omega, Mweza wa yote.

Biblia Takatifu inasema kwamba:

"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye..." - Yn 3:16-17

Kuzaliwa kwa Bwana Yesu ni ishara ya WOKOVU katika maisha yetu sisi tumwaminio. Japokuwa tarehe rasmi ya kuzaliwa kwake Yesu haijulikani kwa uhakika; bali jambo la muhimu ni kufahamu kuwa Bwana Yesu alizaliwa ili atuokoe sisi wanadamu na kuturejeshea uhusiano mwema kati yetu na Mungu wetu.

Habari hizi za wakovu tunazipata kwa wale wachungaji waliotokewa na malaika wa Mungu na kuwaambia kwamba:

"...leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana." - Luka 2:11.

Yesu ni Mwokozi wetu; Wokovu huu maana yake ni UTAKATIFU, UZIMA, USHINDI, AFYA, UTAJIRI, MAFANIKIO, NGUVU, UTAWALA, na kila jema litokalo kwa Bwana Mungu ni letu kupitia utakaso wa damu ya Yesu Kristo. Amekuja kutuokoa na kutupatia uzima wa milele. Kama wewe haujampokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako; kamwe usiache nafasi hii ikupite bure. Tamka maneno haya machache yanayobadirisha maisha yako tangu utakapoyakiri kwa kinywa chako kwa imani.

Sema;

"Bwana Yesu, nakuhitaji katika maisha yangu. Pekeyangu mimi pasipo Wewe siwezi kuishi maisha yampedezayo Mungu. Yesu naomba tangu sasa uwe Bwana na Mwokozi wangu, nisamehe dhambi zote nilizozitenda, naomba unitumie kwa ajili ya utukufu Wako; tangu sasa na siku zote daima. Asante Yesu kwa kuniokoa. Amina."

Sala hiyo fupi imekufanya uwe mwana wa Mungu. Kwako wewe uliyeamini na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yako tangu sasa katika jina la Yesu Kristo. Amen.

Nakutakia sikukuu njema ya Krismasi, Yesu azaliwe ndani yako na mapenzi ya Mungu yatimie kwako, katika jina la Yesu Kristo.

Amina
 
Safi sana mkuu,kumbe wakristo mnaanza kujitambua,umetoa hoja nzito ambazo hata popo hawezi kuzitengua.
 
Back
Top Bottom