Deni la taifa lapaa na kufikia trilioni 40, uchumi wazidi kudorora

Huku biashara nyingi zikiyumba na kuleta wasiwasi wa vyanzo vya mapato ya kodi, ajira nyingi zikipotea, wadau wengi wa nje ya nchi na ndani wakikisoa staili hii ya uongozi usiotaka kuhojiwa wala kukosolewa, deni la taifa limezidi kupaa na kufikia trilioni 40
athari zitokanazo na nchi kushindwa kulipa deni lake ni pamoja na kushushwa thamani ya pesa ya nchi hiyo, huku ikiwa haikopesheki tena, na kama itakuwa haizingatii utawala bora na wa demokrasia hata misaada na uwekezaji itakuwa haipati tena

2eaffb7d8a88a3a8703b3399d754f1c6.jpg
Wenyewe wana lumumba wanashangilia na kupongeza, kweli hii nchi tunaelekea kuzimu
 
kama hayo unayoyasema ni ya kweli tunataka tuone uhalisia wa huo ukuaji wa uchumi kwa maisha ya mtanzania. huo wimbo wa "uchumi unakua" ni za miaka mingi na ni propaganda za kisiasa wakati hali halisi ni kuwa umasikini wa mtanzania unaongezeka. wewe unapoambiwa kila mwananchi anadaiwa shs laki 9 ya deni la taifa bado tu unasema uchumi unakua! be realistic.


Kwa nini unalilisha maneno? Siyo mimi niliyesema kwamba uchumi unakuwa bali ni wataalumu wa kiuchumi na nimekupa link hapo sasa kama wewe unapingana nao una haki ya kufanya hivyo lkn pia ni vizuri ukaja na takwimu zako ambazo zinakinzana na hizo!
 
Seen lakini kumbuka TRA wanavuka malengo ya Makusanyo kila Mwezi hizi ni Dalili kwamba awamu ya Tano kuna ufisadi kuliko hata awamu ya nne .
Hilo ni swala la msingi kulihoji,lkn tutalihoji kupitia wapi?
 
Unamaanisha nini unaposema Uchumi unazidi kudorola? Uchumi wetu unakuwa kwa zaidi 7% na sisi ni wa Pili wa ukuaji kasi wa uchumi Afrika baada ya Ivory Coast na hii kulingana na UN, WB,IMF sasa huko kudorola unamaanisha nini labda?
Utaendelea kuwa ngazi ya wakubwa na kipaza sauti cha walaji
 
Unajua awamu hii mpaka sasa washakopa Trilioni ngapi ?
Katika miezi hii sita? Lete takwimu!
Kukopa sio issue. Matumizi ya mkopo ndiyo issue. Ukikopa ukatengeneza reli Standard Gauge kuna tatizo gani kwa mfano?
Tatizo ni Kukopa ilizitumike kwenda kubembea Jamaica!
 
Kila Mtanzania anadaiwa Milion moja!! hata yule mtoto ambae hajazaliwa deni lake linamngoja
 
nipe hizo indicator za kukua kwa uchumi wa 7%
mimi indicator za kudorora zipo kama vile biashara nyingi kudorora sasa hivi, watu kupunguzwa kazi, hisa za soko la dsm kudoda na mauzo yamepungua kwa 77% sasa
ukipinga kuwa hakuna economic shock yoyote sasa hivi nitakuona mshabiki tu asiye na thamani ya ku argue na mimi
hizo za IMF ni prediction tu ambazo hubadilika
Mkuu nakushauri wachana na huyo mtu maana anachojua ni kuandika alichoelekezwa kuandika
 
Sasa si unachobisha ni nini? Leta basi na wewe data zako za leo tuone uchumi unakuwa kwa asilimia ngapi kwa sasa kama wao wamekosea!
hukuoba nimekuambiwa kuwa hisa kwenye soko la Dsm zimeshuka kwa 77% au hujui hiyo inamaanisha nini?
 
Kama ni hivyo hata mimi naweza kukwambia kwamba kwa mujibu wa TRA mapato Bandarini yameongezeka!
mapato kuongezeka ni kutokana na kukusanya kodi ambayo ilikuwa haikusanywi, kodi hiyo inatokana na biashara zilizochipua awamu iliyopita na sio awamu hii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom