DC mpya wa Ikungi, Singida atumbuliwa ndani ya masaa 24

DC mpya wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Mwl. Fikiri Avias Saidi uteuzi wake umetenguliwa leo, ameteuliwa ndugu Miraji Mtaturu ambae alikuwa katibu wa CCM mkoani Mwanza.

Ngoma inogile.
Kafanya nini tena au kagundulika ni mwana ukawa?
 
Magufuli ni Mkurupukaji. Lawama zote kwa Chama Cha Majipu (CCM) na JK kwa kutupatia Kiongozi wa namna hii.

Ushauri: Mh. Magufuli, kwa hulka, Silka na tabia yako, watu hawatamani kufanya kazi na wewe. Wanaoendelea hawana mbadala tu. Wakiupata watakuacha pekee yako. Nia yako ni njema lakini badili mbinu za Uongozi.
Mkuu kweli wewe ni jasiri
 
Tuachane na utaratibu wa ku suprise vyeo. Ndugu Kinana aliwahi kukataa nafasi ya Ukuu wa Mkoa wakat wa Jakaya, Jk akasema alijifunza tangu hapo akawa ha consult mtu akitaka kumteua, Prof Muhongo nae awali alikataa mara tatu uteuzi mpaka alipoteuliwa tena bila ya kutaarifiwa awali.
Jamaa aache shuguli zake zinazompatia kipato cha siku moja sawa na pato la DC la wiki nzima tena bila ya kunyenyekea nyenyekea wala kujipendekeza pendekeza
Naona wewe umesahaulika,pole sana mkuu
 
watu hawajajua source ya yeye kuenguliwa watu mnakuja mnasema raisi mkurupukaji,subirini mpewe sababu ndio mtoe comments zenu,msije mkalamba matapishi buree,ndomana wamepewa muda wa kutafakari/kujitafakari,kupata ushauri wakubali uteuzi ama wakatae kabla ya kuapishwa.....
 
Magufuli ni Mkurupukaji. Lawama zote kwa Chama Cha Majipu (CCM) na JK kwa kutupatia Kiongozi wa namna hii.

Ushauri: Mh. Magufuli, kwa hulka, Silka na tabia yako, watu hawatamani kufanya kazi na wewe. Wanaoendelea hawana mbadala tu. Wakiupata watakuacha pekee yako. Nia yako ni njema lakini badili mbinu za Uongozi.
Je kama mteuliwa amekataa nafasi ya DC, hapo nani atalaumiwa
Ebu punguza ushabiki aiseeee...
 
Back
Top Bottom