DC Mpanda aagiza Mgodi wa Madini ufungwe kutokana na mlipuko wa Kipindupindu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,814
13,580

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi, Jamila Yusuf amesitisha shughuli za uchimbaji madini katika Mgodi wa Lumuka uliyopo Kijiji cha Dirifu, Manispaa ya Mpanda kutokana na mlipuko wa Ugonjwa wa Kipindupindu uliozuka katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Agizo hilo amelitoa mara baada ya kutembelea eneo la Lumuka lenye machimbo ya dhahabu ambapo idadi kubwa ya watu waliothirika na kipindupindu wanatoka katika machimbo hayo.

Ukaguzi huo umefanyika baada agizo la Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko kumtaka Katibu Tawala wa Mkoa huo na Wakuu wa Wilaya kuchukua hatua kali ya kudhibiti ugonjwa huo.

PIA SOMA:
 
Back
Top Bottom