DC Moshi kukosa kura za CCM awaangushia hasira maafisa elimu kata kwa kuwahamisha vituo vya kazi wote bila malipo

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
14,255
23,946
Kasheshe la DC MOSHI Bw. ABBAS KAYANDA, huko Kilimanjaro kupata pigo la kukosa kura za CCM limechukua sura nyingine.

Baada ya gazeti la mwananchi kumrusha hewani DC wa moshi kwa kukosa kura ndani ya chama cha mapinduzi, amewaangushia maafisaelimu kata na kuwahamisha wote vituo vyao vya kazi bila malipo na bila kusikilizwa.

Kilio hicho kimekwenda mbali zaidi kwa DC huyo anajua wazi kuwa mkeka ujao jina lake halitakuwepo ila amefanya makusudi ili liwalo na liwe huko maafisaelimu wakishiriki kuwahanyia unyama huo walimu ambao ni watumishi watiifu ndani ya ccm na serikali yao tukufu.

Tulivyo jaribu kuwasiliana na ofisi ya elimu mkoa wa kilimanjaro walikiri kusikia uhamisho huo ila wakasema mkoa kama mkoa hawakushirikishwa katika zoezi la kuhamisha waratibu elimu hao .

Pamoja na DC kukosa kura ndani ya chama cha mapinduzi, amezua tena sintofahamu hata kwenye idara za afya kwani ameitisha kikao cha kutaka kuwahamisha vituo ya kazi madaktari wote wa vituo vya afya ndani ya wilaya ya moshi.

Sasa CCM isipokaa macho na DC wa moshi kuna hatari ya chama hicho tawala kukosa majimbo mwaka 2025 kwani anayo chuki kubwa sana na ccm baada ya kukosa kura na sasa chuki hiyo amehamishia kwa watumishi wa Umma na mwisho atahamishia chuki hiyo kwa wananchi wanyonge.
 
Moshi. Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Abbas Kayanda ameshindwa kung'ara kwenye uchaguzi wa CCM Wilaya ya Moshi vijijini katika nafasi ya Ujumbe wa mkutano mkuu Taifa baada ya wajumbe kumbwaga.

Uchaguzi huo wa Wilaya ambao ulimalizika jana Ijumaa Septemba 30, 2022 usiku, katika nafasi ya Mjumbe wa mkutano Mkuu wa CCM Taifa, mbali na Kayanda, pia walikuwepo wakuu wa wilaya watatu wa zamani, ambapo Raymond Mushi na Betty Machangu nao wameangukia pua, huku Regina Chonjo akichomoza kwa kuchaguliwa.

Msimamizi wa uchaguzi huo Ibrahim Mjanakheri amewatangaza wajumbe wa mkutano mkuu Taifa kutokea Moshi vijijini ambao wameshinda kuwa ni Leonard Waziri aliyepata kura 644, Regina Chonjo kura 587 na Prosper Tesha kura 517.

Amewataja wagombea walioshindwa uchaguzi huo na kura zao kwenye mabano kuwa ni Abas Kayanda (423), Betty Machangu (398), Ally Bady (323), Raymond Mushi (201), Brayton Shayo (68)na Ruwaichi Kaale (28).

Kwa nafasi ya mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Moshi Vijijini, msimamizi wa uchaguzi amemtangaza Cyril Mushi aliyekuwa akitetea nafasi hiyo, kushinda kwa kupata kura 919, dhidi ya Esther Kway aliyepata kura 29 na Abel Massawe kura 77.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Mwenyekiti Mushi amesema tayari imepatikana timu ya ushindi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 na uchaguzi mkuu 2025 na kiwataka wanachama wa chama hicho kuungana na kuwa wamoja ili kufanikisha hilo.

Aidha Mushi ameonya viongozi na wanachama wa chama hicho kutotumia mitandao ya kijamii kuchafua chama na kueleza kuwa hawatamvumilia wala kumfumbia macho mtu wa namna hiyo.

"Hatutamvumilia mtu yoyote ambaye atajaribu kuvuruga umoja wetu ndani ya chama, tutapambana naye. Wapo watu wanatuchafua kwenye mitandao, naomba niseme sitaruhusu shughuli za chama zifanyike kwenye mitandao, lazima kila mmoja ambaye ni mwanachama wa CCM aheshimu katiba ya chama,” amesema.
 
Hata hivyo maafisaelimu Moshi manispaa wamenyanyaswa na afisaelimu msingi ambaye amehamishiwa huko Kwa rushwa
 
Back
Top Bottom