EJOSMAT
Member
- Jan 7, 2016
- 32
- 19
Mdudu anaetafuna mbao na kutoa milio kama msumeno unakata mbao badae unakuta mbao zinayoa unga ni mdudu hatari sana jamii ya mende wa mbao. Mdudu huyu hutaga mayai yake kwenye nyuso za mbao, mayai yake huwezi kuyagundua kwani yana asili ya maji maji. Baada ya hapo mayai huzama ndani ya mbao nakubadilika kupitia hatua za ukuaji za mdudu(insects)akiwa katika hatua ya lava hapa anakua kama mnyoo na meno mawili makubwa magumu sana kama yale ya mchwa hapa ndio wanaanza kushambulia mbao wakiwa ndani na huwezi kuona tundu walipoingia maana waliingia katika hali ya majimaji.Kuna waliosema Mafuta ya taa ama diesel... kuzipaka mbao huko darini. Hii ni tiba?
-Kaveli-
Hatua hii ndio hatari zaidi kwani ndio hatua ambayo mdudu huyu hula hivyo kufanya uharibifu mkubwa wa mbao zako iwe ni furniture au dari ya nyumba yao Italian na kua kama mabua tu kwani utakuta mbao zinavunjika na kumwaga unga wa njano. Baadae mnyoo hugeuka hatua za mwisho na kua mdudu kamili hapo sasa hutoka nje kama mdudu kamili na ndipo utaona tundu lake alipotoka ila hatua hii uharibifu utakua umekamilika. Akishatoka kama ni jike ataanza kutaga mayai tena upya na kurudia mzunguko uleule.
Kwanini wanakula mbao?
Wadudu hawa wanakula mbao ambazo 1.hazina dawa
2Hazijakomaa(laini)
3.Hazijakauka vizuri
Wauzaji wengi wa mbao sikuhizi sio waaminifu watakwambia mbao zina dawa kumbe wamezipaka maji ya rangi kupunguza gharama au kama wameweka dawa warakua wamezichovya tu juu juu ili kuziwahisha sokoni hawana muda wakupika maelefu ya mbao kwenye maji yanayo chemka dawa. Hivyo wengi huchimba shimo na kuweka dawa kidogo bila kufatauwiano wa dawa na maji na kisha wanachukua mbao moja moja wanafanya kuichovya na kutoa kama wanabatiza vile. Hivyo sio rahizi kumzuia mdudu huyo anaekula kuanzia ndani ya mbao.
Namna ya kumdhibiti mdudu huyu
Kama ilivyo kwa wadudu wengi ngozi yao imetengenezwa kwa matirio isiyoweza kuhimili baadhi ya kemikali ndio maana ukimwagia nyoka mafuta ya taa ataanza kuchubuka chubuka.
Hivyo mafuta jamii ya petrol yanasaidia sana kuangamiza wadudu hawa yaani
Petrol, diesel, .mafuta ya taa na hata oil chafu.
Njia ya kutumia mafuta ya taa ikichanganywa na turpentine kwa uwiano maalumu ni nzuri.
Angalizo: baadhi ya mafuta ni hatari kwani yanasapoti uwakaji wa moto pia
Na baadhi ya mafuta yanaharufu kali hasa unapopata ndani ya nyumba yako na mengine yana haribu rangi ya mbao na samani ndani ya nyumba yako kama yatadondokea. Japo unaweza kutumia kumdhibiti mdudu huyu wakutafuna mbao
Dawa nduzi ambayo nimeitumia kwa nyumba kadhaa zenye shida hizi na hata kwenye furniture zenye wadudu hawa au kuzilinda zilizobaki zisishambuliwe tena na wadudu hawa ni dawa zenye kiambata sumu cha pareto hapo utakua umemshinda kabisa mdudu huyu na utafurahia nyumba na furniture zako
:Kumbuka si kila dawa ya kuua mdudu inaweza kuwaangamiza wadudu hawa
Kama hujapata utatuzi na ungependa kuwasiliana nasi tutafute kwa simu/whatsapp 0717 040 837 . Engineer Mkuuu