FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 37,908
- 43,821
Nimesikia kwamba Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Samiah Sukuhu Hassan hataki kusikia maoni ya wananchi wake juu ya mkataba wenye ukakasi wa ugawaji bure wa Bandari zote za Tanganyika.
Sina shaka habari hizi ni za ukweli, maana nimeona video clip, na it seems aunthentic. Sasa hapa kuna maswali mazito ya kujiuliza, na kuna maoni ya kutoa.
MASWALI.
1.) Je, ni kosa kutoa maoni juu ya utendaji mbovu wa serikali kuhusu mkataba huu? Kwamba ukitoa maoni hasi basi zinakuwa ni kelele? Sisi tunakupigia kelele?
2.) Je, hoja za wananchi (au kelele kama ulivyoamua kuziita) umezisikia vyema? Majibu yake ni yepi, kwanini usijibu hoja za msingi za hao wapiga kelele ili waache kupiga kelele? Au unazipenda hizi kelele?
MAONI
Kama mtu akiziba masikio, namna bora ni kuweka loud speaker na kumsogelea karibu, hadi akimbie yeye.
==========================
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa
1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)
2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?
3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?
4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!
6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Hivi ni kweli Rais wetu kausoma ule mkataba?
==========================
========================
Masikio yanaanza kuzibuka
Waziri Mkuu: Tumesikia mijadala, hofu kuhusu makubaliano ya Bandari. Tumeanza kutoa elimu ya kuwapa faraja Watanzania
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amekiri kuwa ni kweli tangu Bunge la Tanzania liliporidhia azimio la Nchi ya Tanzania kuimarisha mahusiano yake Nchi ya Tanzania na Nchi ya Dubai hasa katika maeneo ya Kiuchumi na Kijamii, kumekuwa na mijadala mingi, maoni, ushauri na hofu za Uwekezaji nchini...
www.jamiiforums.com
===========================
Update: 24/07/2023
Sekretarieti ya Bunge: Kuna mapungufu katika Mkataba wa Bandari na DP World; ukomo wake uwekwe wazi
Kwa furaha kubwa kabisa napenda kuwataarifu wana JF kuwa kwa tukio litakalotokea leo tarehe 24/07/2023, mjadala wa Dp world ndio unafika mwisho, tujipongeze wote tulioshiriki. Ahsanteni sana. ========== Mdau mwingine pia aliandika: Tumelumbana weee, tumeelezana weee, Kuna wale vichwa maji...
www.jamiiforums.com
========================
==========================
Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Hatuungi mkono Mkataba wa Bandari. Sauti ya Watu ni sauti ya Mungu
Tamko hilo limetolewa leo na Padri Kitima. Kwa Mujibu wa Padri kitime ,TEC imeamua kusimama na wananchi kwenye suala la bandari Padri kitime amesisitiza kwa sasa serikali inataka kuligawa Taifa kwenye pande mbili wanaokubaliana na wasiokubaliana,lakini wengi wanaokubaliana wanahofi tu kwa...
www.jamiiforums.com
==========================
Tetesi: - Muda wowote kuanzia sasa Samia ataachana na DP World!
Be the first to know... muda wowote kuanzia sasa Rais Samia atauzima rasmi mjadala unaochukua sura mpya kila siku nao si mwingine bali ni DP World! Vyanzo vyangu toka ndani ya Chama na Serikali vinabainisha joto la mjadala linaelekea pabaya hivyo busara imetumika kufunika kombe mwanaharamu...
www.jamiiforums.com